Mwandishi:
WAMJW
Mhariri:
ULY CLINIC
9 Oktoba 2021, 11:21:17
Je, Azuma ni dawa sahihi ya kutibu COVID-19? Je, inatumika kama kinga au kama tiba?
COVID-19 ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona. AZUMA ni dawa ya kuua bakteria (antibiotiki) sio virusi. Hata hivyo, mpaka sasa hivi hakuna dawa iliothibitishwa kutibu COVID-19. Lakini hata hivyo, mapafu ya mgonjwa wa COVID-19 yanaweza pia kushambuliwa na bakteria na kusababisha madhara zaidi. Hivyo basi, ili kupunguza haya madhara, AZUMA nia mojawapo ya dawa ambazo mgonjwa wa COVID-19 hupewa na daktari hospitalini kulingana na hali ya mgonjwa ilivyo.
Kumbuka, matumizi holela ya dawa za antibiotiki kama AZUMA bila ushauri wa Daktari ni hatari kwani unaweza kupelekea kuibuka kwa usugu wa vimelea kwenye dawa.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
9 Oktoba 2021, 12:27:57
Rejea za mada hii