Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dr. Benjamin L, MD.
1 Februari 2024, 12:15:44
Je, ni dawa zipi hupaswi kunywa na maziwa, na unapaswa kunywa maziwa muda gani?
Muingiliano wa dawa huweza kutokea endapo dawa itatumiwa pamoja na dawa nyingine, chakula, virutubishi au wakati mwingine uwepo wa ugonjwa Fulani.
Miongoni mwa vyakula ambavyo huwa vina muingiliano na dawa ni maziwa pamoja na mazao yake kama mtindi, siagi nk.
Kwanini haupaswi kunywa dawa na maziwa kwa pamoja?
Madini ya kalisiamu na maginisiamu yaliyo katika maziwa yanapokutana na dawa hutengeneza kampaundi ambayo hushindwa kufyozwa kutoka kwenye matumbo kuingia kwenye damu. Hivyo kupunguza upatikani wa dawa katika damu na kusababisha uwezo wa dawa kupungua.
Je, ni dawa zipi ambazo hupaswi kunywa pamoja na maziwa?
Haushauriwi kunywa dawa zifuatazo pamoja na maziwa
Ciprofloxacin
Doxycycline
Mecaptopurine
Je, ni muda gani sahihi wa kunywa maziwa ikiwa unatumia dawa zenye muingiliano na maziwa?
Unashauriwa kunywa maziwa masaa mawili hadi matatu kabla au baada ya kunywa dawa.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
1 Februari 2024, 12:37:56
Rejea za mada hii
Food-Drug Interactions – PMC. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3191675/. Imechukuliwa 01.02.2024
Table: Some Drug-Food Interactions. MSD Manuals. https://www.msdmanuals.com/home/multimedia/table/some-drug-food-interactions. Imechukuliwa 01.02.2024
Doxycycline and Dairy: Can Milk, Yogurt Affect. Healthline. https://www.healthline.com/health/doxycycline-and-dairy.