Mwandishi:
Dkt. Mangwella S, MD
Mhariri:
Dkt. Charles W, MD
20 Oktoba 2021, 17:10:51
G spoti inapatikana wapi?
G spoti kwa mwanamke ni sehemu inayopatikana sentimita 5 hadi 5 kutoka nje ya tundu la uke, sehemu hii ni mahali ambapo tezi jike hupatikana na huwa karibu sana na mrija wa mkojo. Kusisimuliwa vizuri kwa sehemu hii husababisha hisia kali za raha kufika kileleni kirahisi.
Kwa maelezo ya ki-anatomia, eneo G ni sehemu ya uke inayopatikana juu ya ukuta wa periniamu, milimita 16.5 kutoka sehemu ya juu ya tundu la mkojo na hutengeneza pembe ya nyuzi 35 na mpaka wa pembeni wa mrija wa mkojo. Mkia wa eneo G unapatikana milimita 3 kutoka kwenye mpaka wa pembeni wa mrija wa mkojo wakati kichwa chake hupatikana milimita 15 kutoka kwenye mpaka wa pembeni wa mrija wa mkojo. Angalia picha kwa maelezo zaidi.
Mwanaume pia ana G spoti ambayo inapatikana kwenye kuta za tezi dume, hivyo kufanya tezi dume kuitwa G spoti kwa mwanaume.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
20 Oktoba 2021, 17:10:51
Rejea za mada hii
Hines TM. The G-spot: a modern gynecologic myth. Am J Obstet Gynecol. 2001; 185: 355-358.
Gräfenberg E.The role of the urethra in female orgasm. Int J Sexol. 1950; 3 (Available at:): 145-148. http://www.DoctorG.com/Grafenberg.htm. Imechukuliwa 20.10.2021
Davidson JK, et al. The role of the Grafenberg spot and female ejaculation in the female orgasmic response: an empirical analysis. J Sex Marital Ther. 1989; 15: 102-120.
Zaviacic M, et al. Update on the female prostate and the phenomenon of female ejaculation. J Sex Res. 1993; 30: 148-151