Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
12 Agosti 2023 17:44:45
Je, kuna kipimo maalumu cha PID
Hakuna kipimo cha utambua kama una PID. Utambuzi wa sasa mara nyingi hutokana na historia ya kitabibu inayochukuliwa kwako sambamba na uchunguzi wa awali wa mwili pamoja na vipimo vingine. Mara nyingi unaweza usitambue kuwa una PID kwa sababu dalili huwa za wastani au kutotokea kabisa. Hata hivyo endapo zitatokea hujumuisha;
Maumivu kwenye tumbo la chini ya kitovu
Homa
Kutokwana uchafu wenye harufu mbaya ukeni
Hisia za kuungua wakati wa ngono
Kutokwa na damu ukeni wakati wa ngono
Pain in your lower abdomen;
Hisia za kuungua wakati w akukojoa
Kutokwa na damu katikati ya vipindi vya hedhi
Mambo ya kukumbuka
Mbali na dalili hizi kuashiria PID, unapaswa kupata uchunguzi wa daktari ili aweze kutambua kama ni PID au ugonjwa mwingine na kupata matibabu sahihi.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Pata maelezo zaidi katika makal aya PID sehemu nyingine katika makala zifuatazo
Je PID inatibika
Ugonjwa wa PID
Majadiliano na wataalamu wa afya PID
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
12 Agosti 2023 17:44:45
Rejea za mada hii
American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Pelvic Inflammatory Disease. ACOG Patient Education Pamphlet, 1999.
Westrom L and Eschenbach D. In: K. Holmes, P. Sparling, P. Mardh et al (eds). Sexually Transmitted Diseases, 3rd Edition. New York: McGraw-Hill, 1999, 783-809.