Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dr. Mangwella S, MD
6 Februari 2024, 05:09:12
Je, kama nimejifungua mara 2 kwa upasuaji kuna uwezekano wa kujifungua kawaida kwa ujauzito unaofuata?
Majibu ya swali hili yanaweza kuwa ni ndio au hapana, hii ni kwasababu visababishi vya kujifungua kwa upasuaji huweza kujirudia au kutojirudia, au kuwa na visababishi vya lazima ambavyo ni lazima kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa mara nyingine.
Ni wakati gani unaweza kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji?
Unaweza kujifungua kawaida endapo;
Umekaa miaka 2 au zaidi kabla ya kubeba ujauzito mwingine
Sababu iliyopelekea kujifungua kwa upasuaji haijiruidii.
Baadhi ya sababu hizo ni mtoto kuchoka, kutoka damu ukeni kabla ya uchungu, mtoto kulala vibaya nk.
Ni wakati gani hauwezi kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji?
Hautaweza kujifungua kawaida endapo;
Umejifungua kwa upasuaji mara 2 au zaidi kwani huongeza hatari ya kuchanika kwa kizazi
kuchanwa kwenye sehemu ya kiwiliwili cha mji wa uzazi (mchano T’ na ‘J)’ kutoa mtoto au vimbe za fibroid kwenye sehemu hii ya kizazi
Endapo kisabababishi cha upasuaji kwenye ujauzito uliopita kipo kwenye ujauzito huu
Kumbuka
Wanawake waliowahi kujifungua kwa upasuaji mara 1 wanaweza kujifungua kawaida endapo visababishi vya upasuaji katika ujauzito uliopita havitajirudia, na baadhi yao huitaji upasuaji wa dharura ikiwa mwenendo wa leba si mzuri.
Mara tu upatapo ujauzito unapaswa kuanza kliniki ya ujauzito.
Usijaribu kujifungulia nyumbani au katika kituo ambacho hakina huduma za dharura za upasuaji.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
6 Februari 2024, 10:13:27
Rejea za mada hii
Vaginal Birth After Cesarean Delivery. Medscape. https://emedicine.medscape.com/article/272187-overview?form=fpf. Imechukuliwa 05.02.24
Vaginal Birth After Cesarean Delivery – StatPearls. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK507844/. Imechukuliwa 05.02.24
Choosing the route of delivery after cesarean birth – UpToDate. https://www.uptodate.com/contents/choosing-the-route-of-delivery-after-cesarean-birth. Imechukuliwa 05.02.2024