Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dr. Adolf S, MD
31 Januari 2024, 05:07:45
Je, inachukua muda gani kwa kipimo cha mimba cha mkojo kuonesha mimba?
Kipimo cha mimba kwenye mkojo hutumika kutambua ujauzito mwanamke anapokosa hedhi. Kipimo hiki hutumiwa na wanawake wengi kwa kuwa hakihiitaji kufanywa na mtaalamu, na pia hupatikana kwa urahisi.
Kipimo hupima uwepo wa homoni ijulikanayo kama human chorionic gonadotropin (hCG), ambayo huzalishwa baada ya yai lililotungishwa kujipandikiza katika mji wa mimba.
Kipimo cha mimba kwenye mkojo huonesha ujauzito muda gani baada ya kukosa hedhi?
Homoni hCG huanza kuzalishwa siku ya 6 baada ya yai lililotungishwa kujishikiza katika mji wa mimba, na huchukua siku 7 hadi 10 mwili kuzalisha kiwango cha kutosha kuweza kutambulika kwa vipimo vya sasa kwenye mkojo.
Kwa ujumla inachukua hadi siku 14 au zaidi baada ya kukosa hedhi kipimo kuonesha uwepo wa ujauzito kwa mwanamke mwenye mzunguko unaoeleweka.
Kumbuka
Ili kupata matokeo ya uhakika ya ujauzito pima kuanzia wiki 2 baada ya kukosa hedhi
Tumia mkojo wa kwanza unapoamka kwani huwa na kiwango kikubwa cha homoni hCG
Muda wa kipimo kuonesha majibu chanya ya ujauzito hutofautiana kulingana na urefu wa mzunguko wa hedhi
Kulingana na teknolojia kukua kuna vipimo vyenye uwezo wa kugundua ujauzito mapema zaidi, hata hivyo ni vema kusubiri kwa muda ili kuwa na uhakika zaidi
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
31 Januari 2024, 05:07:45
Rejea za mada hii
Devices for Home Evaluation of Women’s Health Concerns – Medscape. https://www.medscape.com/viewarticle/571895_3. Imechukuliwa 04.01.2024
Should you take a pregnancy test? 5 Signs and When to Take It. Healthline. https://www.healthline.com/health/pregnancy/five-signs-to-take-pregnancy-test. Imechukuliwa 04.01.2024
How and when to take a pregnancy test. Medical News Today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/316463. Imechukuliwa 04.01.2024