top of page

Mwandishi:

Dr. Adolf S, MD

Mhariri:

Dr. Benjamin S, MD

30 Januari 2024 11:56:35

Kuna aina ngapi za seli mundu?

Je kuna aina ngapi za seli mundu?

Seli mundu ni kundi la maradhi ya kurithi ya chembe nyekundu za damu ambayo humpata mtu yoyote anayezaliwa na wazazi wenye vinasaba vya seli mundu.

Aina za seli mundu

Kuna aina nyingi za seli mundu, zifuatazo ni aina kuu za seli mundu ambazo hutegemea vinasaba vilivyorithiwa kutoka kwa wazazi.

HbSS

Ni aina ya seli mundu inayopatikana kwa mtu aliyrithi vinasaba S vya seli mundu kutoka kwa wazazi wote. Aina hii hujulikana pia kama Seli mundu ya upungufu wa damu na ni aina yenye dalili kali za ugonjwa.

HbSC

Ni aina ya seli mundu inayotokea mtu anaporithi kinasaba S kutoka kwa mzazi mmoja na kinasaba C kutoka kwa mzazi mwingine. Aina hii huwa na dalili za wastani za ugonjwa

HbS beta thalassemia

Ni aina ya seli mundu inayotokea kwa mtu anaporithi kinasaba S kutoka kwa mzazi mmoja na kinasaba beta thalassemia (ambacho kina aina mbili) kwa mzazi mwingine. Aina hii huwa na dalili kali za au za kawaida kulingana na aina ya kinasaba Beta thalassemia kilichorithiwa.

HbAS

Aina hii ya seli mundu hutokea kwa mtu anaporithi kinasaba S kutoka kwa mzazi mmoja na kinasaba A ambacho hakina ugonjwa kutoka kwa mzazi mwingine.

Mtu huyu huwa hana dalili yoyote licha ya kubeba ugonjwa wa seli mundu ambao atarithisha kwa watoto wake.

Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu seli mundu?

Soma zaidi makala ya seli mundu kwenye mada ya seli mundu.


ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

30 Januari 2024 12:40:14

Rejea za mada hii

  1. What is Sickle Cell Disease? Centers for Disease Control and Prevention (.gov). https://www.cdc.gov/ncbddd/sicklecell/facts.html. Imechukuliwa 03.01.2024

  2. Sickle Cell Trait – StatPearls – NCBI Bookshelf.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537130/. Imechukuliwa 03.01.2024

  3. Sickle Cell Anemia: Types, Symptoms, and Treatment. Healthline. https://www.healthline.com/health/sickle-cell-anemia#types. Imechukuliwa 03.01.2024

bottom of page