Mwandishi:
Dkt. Sospeter B, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda S, MD
20 Novemba 2021, 18:45:03
Je, vidonge vya majira yenye vichocheo viwili vinaweza kutumika kwa wagonjwa wa kisukari?
Vidonge vya majira yenye vichocheo viwili havipaswi kutumika kwa wanawake wenye kisukari chenye sifa kati ya zifuatazo;
Kisukari cha zaidi ya miaka 20
Dalili za uharibifu wa mishipa ya fahamu
Dalili za uharibifu wa mishipa ya damu
Dalili za uharibifu wa macho
Dalili za uharibifu wa figo
Dalili za uhalibifu wa neva
Nini unapaswa kuzingatia
Usitumie vidonge vya majira yenye vichocheo viwili, unapaswa kushirikiana na mtaalamu wa afya kuchagua njia nyingine ya uzazi wa mpango isiyo na kichocheo estrojeni na isiwe sindano yenye projestini.
Kwanini usitumie?
Vidonge vya majira yenye vichocheo viwili licha ya kutosababisha kisukari, huwa na madhara kwenye ugonjwa wa kisukari. Tafiti zinaonyesha kuwa estrojeni inayopatikana kwenye vidonge hivi huongeza kiasi cha sukari mwilini na upinzazi wa kichocheo cha insulin kudhibiti kiwango cha sukari.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
20 Novemba 2021, 18:52:56
Rejea za mada hii
OB-GYN. Diabetes & Birth Control. https://obgyn.coloradowomenshealth.com/health-info/birth-control/medical-conditions-birth-control/diabetes. Imechukuliwa 20.11.2021
Gourdy P. Diabetes and oral contraception. Best Pract Res Clin Endocrinol Metab. 2013 Feb;27(1):67-76. doi: 10.1016/j.beem.2012.11.001. Epub 2012 Dec 19. PMID: 23384747.
Diabetes.co.uk. Contraceptive Pill and Diabetes. https://www.diabetes.co.uk/diabetes-contraceptive-pill.html. Imechukuliwa 20.11.2021
Gourdy P. Diabetes and oral contraception. Best Pract Res Clin Endocrinol Metab. 2013;27:67–76.
International Diabetes Federation (IDF) IDF Diabetes Atlas. 6th ed. International Diabetes Federation; 2013. https://www.idf.org/sites/default/files/EN_6E_Atlas_Full_0.pdf. Imechukuliwa 20.11.2021
Dunlop AL, et al. The clinical content of preconception care: women with chronic medical conditions. Am J Obstet Gynaecol. 2008;199(6 Suppl B):S310–S327.
OBGYN. Diabetes & Birth Control. https://obgyn.coloradowomenshealth.com/health-info/birth-control/medical-conditions-birth-control/diabetes#. Imechukuliwa 20.11.2021