top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, MD

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

11 Oktoba 2021, 19:18:53

Mwanamke aliehalibikiwa ujauzito anaweza kupata ujauzito mwingine ndani ya miezi 6?

Mwanamke aliehalibikiwa ujauzito anaweza kupata ujauzito mwingine ndani ya miezi 6?

Ndio!

Hili ni moja ya swali wanawake wengi wanauliza kwa daktari.


Tafiti mpya zinaonyesha kuwa hakuna faida ya kusubiria muda upite baada ya mimba kutoka ndio ubebe ujauzuti mwingine.


Wanawake waliopata tatizo la mimba kutoka endapo watapata mimba nyingine mapema iwezekanavyo, ujauzito huo huwa na matokeo mazuri kutokuwa na hatari ya kupata madhara ya ujauzito huo ukilinganisha na wanawake waliosubiria mpaka baada ya miezi sita kupita.


Kwa wanawake ambao ujauzito umetoka na wanatamani kupata ujauzito, wanaweza kupata ujauzito mwingine mapema na wanapaswa kupewa moyo kuwa ujauzito unaweza kuwa na matokeo mazuri hivyo kutokuwa na wasiwasi. Hata hivyo wanapaswa kupata ujauzito pale wanapokuwa tayari kimwili na kiakili


Ni haraka kiasi gani ubebe mimba?


Haifahamiki ni kwa haraka kiasi gani unapaswa kubeba ujauzuito baada ya ujauzito mwingine kutoka, mashirika mbalimbali ya afya yanashauri muda tofauti tofauti mfano Shirika la afya duniani linashauri kusubiria angalau miezi 6 kupita na wengine wanashauri muda wa miezi 18 kupita.


Taarifa mpya za tafiti zinaonyesha muda gani mzuri?


Tafiti mpya zinaonyesha kuwa wanawake waliopata mimba chini ya miezi 3 baada ya ujauzito kutoka walipata matokeo mazuri na hatari kidogo ya madhara kwenye ujauzito kuliko waliosubiria muda wa mitatu au zaidi. Unaweza kupata ujauzito katika kipindi chochote unapokuwa tayari baada ya ujauzito kutoka lakini kusiwe na sababu ya hatari kama vile maambukizi kwenye mfuko wa kizazi.


Madhara ya kusubiria kwa muda mrefu


Wanawake waliosubiria kwa muda wa miaka miwili au zaidi walipata madhara ya;


  • Mimba kutungwa nje ya mfuko wa kizazi

  • Mimba kutoka

  • Kujifungua kwa upasuaji

  • Kujifungua njiti

  • Kujifungua mtoto kabla ya wakati


Wanawake gani wanapaswa kusubiria kwa muda mrefu zaidi kabla ya kupata ujauzito mwingine?


Wanawake wanaopaswa kusubiria kwa muda mrefu zaidi kabla ya kupata ujauzito mwingine ni wale wenye dalili ya maambukizi, wanapswa kupata matibabu kabla ya kupata ujauzito ili kupunguza hatari ya mimba kutoka.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

11 Oktoba 2021, 19:18:56

Rejea za mada hii

  1. Schliep, Karen C et al. “Trying to Conceive After an Early Pregnancy Loss: An Assessment on How Long Couples Should Wait.” Obstetrics and gynecology vol. 127,2 (2016): 204-12. doi:10.1097/AOG.0000000000001159

  2. Sundermann, et al. “Interpregnancy Interval After Pregnancy Loss and Risk of Repeat Miscarriage.” Obstetrics and gynecology vol. 130,6 (2017): 1312-1318. doi:10.1097/AOG.0000000000002318

  3. Davanzo, et al. “How long after a miscarriage should women wait before becoming pregnant again? Multivariate analysis of cohort data from Matlab, Bangladesh.” BMJ open vol. 2,4 e001591. 20 Aug. 2012, doi:10.1136/bmjopen-2012-001591

  4. After a Miscarriage: Getting Pregnant Again Pregnancy Loss. http://americanpregnancy.org/pregnancy-loss/after-miscarriage-getting-pregnant-again/. Imechukuliwa 11.10.2021

  5. World Health Organization Report of a WHO technical consultation on birth spacing, Geneva Switzerland 13-15 June 2005. http://www.who.int/maternal_child_adolescent/documents/birth_spacing.pdf. Imechukuliwa 11.10.2021

  6. Zhu BP, et al. Effect of the interval between pregnancies on perinatal outcomes. N Engl J Med. 1999 Feb 25;340(8):589-94. doi: 10.1056/NEJM199902253400801. PMID: 10029642.

bottom of page