Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dr. Benjamin S, MD
6 Februari 2024 10:21:29
Ninaweza kushiriki ngono na mwenza wangu baada ya muda gani ikiwa mimba imetoka?
Hakuna muda maalumu wa kushiriki ngono baada ya mimba kutoka hii ni kwasababu hali ya utayari wa kushiriki ngono kimwili na kiakili hutofautiana kati ya mtu na mtu.
Unaweza kuanza kushiriki ngono endapo unahisi uko tayari kiakili, kimwili na afya yako iko katika hali nzuri.
Hata hivyo unapaswa kuzingatia mambo haya kabla ya kuanza kushiriki ngono
Jadili na mwenza wako na hakikisha nyote mko tayari kuanza kushiriki ngono
Subiri walau wiki 2 baada ya mimba kutoka ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi katika kizazi
Hakikisha damu haitoki ukeni
Tumia uzazi wa mpango ikiwa hauitaji kebeba ujauzito mwingine hivi karibuni
Wapi utapata maelezo zaidi?
Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii bofya hapa  https://www.ulyclinic.com/vidokezo-vya-kiafya/muda-wa-kusubiri-ngono-baada-ya-kutoa-mimba
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
6 Februari 2024 15:55:41
Rejea za mada hii
POST-ABORTION- Clinical Practice Handbook for Safe Abortion. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304195/. Imechukuliwa 06.02.2024
POST-ABORTION CARE - Counselling for Maternal and Newborn Health Care: A Handbook for Building Skills.NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304195/. Imechukuliwa 06.02.2024
After abortion care: Self-care and recovery. Medical News Today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/322533. Imechukuliwa 06.02.2024