Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dr.Adolf S, MD.
1 Februari 2024, 13:30:05
Je, nitajuaje kama mtoto ameanza kushuka kwaajili ya kutoka?
Katika wiki za mwisho za ujauzito mtoto huanza kushuka kuingia katika nyonga ya uzazi tayari kwa kuzaliwa.
Hatua hii ni muhimu sana japo haimaanishi kuwa leba itaanza mara moja. Mjamzito ni vema kufahamu dalili na viashiria vya mtoto kushuka katika nyonga.
Dalili za mtoto kushuka
Zifuatazo ni dalili na viashiria vya mtoto kushuka katika nyonga;
Kukojoa mara kwa mara
Kuhisi mgandamizo mkubwa kwenye nyonga
Kushindwa kutembea vema
Kuhisi maumivu ya via vya uzazi, kiuno na mgongo
Kukosa haja kubwa au kutoka kwa shinda
Kuongezeka kwa ute ukeni
Kupungua au kupotea kwa hali ya kupumua kwa shida
Kupungua au kupotea kwa dalili za kiungulia
Kupata bawasili
Tumbo la ujauzito kuonekana limeshuka
Nini cha kufanya
Unaweza kuendelea kufanya mazoezi ya kuanzisha uchungu ili kumsaidia mtoto kujiweka vema anaposhuka, na pia kuuandaa mwili wako kwa hatua ya leba.
Kumbuka
Kushuka kwa mtoto haimaanishi uchungu utaanza mara baada tu ya kushuka
Dalili tajwa hapo juu haziwezi kutokea endapo mtoto hajageuka na kutanguliza kichwa
Muda wa mtoto kushuka hutofautiana kati ya mjamzito mmoja na mwingine, kwani wajawazito wengine huanza kuona dalili siku kadhaa kabla ya leba kuanza na wengine masaa machache kabla ya leba au baada ya leba
Mtoto huwahi kushuka kwa ujauzito wa kwanza
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
1 Februari 2024, 13:30:05
Rejea za mada hii
What You Should Know About Head Engagement in Pregnancy. WebMDhttps://www.webmd.com/baby/head-engagement-in-pregnancy-what-is-it. Imechukuliwa 06.01.2024
How You Can Tell If Baby Is Engaged: Meaning, Symptoms, More. Healthline. https://www.healthline.com/health/pregnancy/baby-engaged#signs-and-symptoms. Imechukuliwa 06.01.2024