top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

14 Oktoba 2021, 10:45:42

Ninaweza kupata mimba nikitumia norethisterone kuzuia kuingia piriodi kwa muda?

Ninaweza kupata mimba nikitumia norethisterone kuzuia kuingia piriodi kwa muda?

NDIO!

Unaweza kupata mimba kama unatumia norethisterone kwa lengo la kuzuia period kwa muda. Dozi ya kuzuia kupata damu ya hedhi mara nyingi hutumika kati ya siku 3 hadi 7 kisha utaacha kutumia dawa. Unapaswa kutumia kondomu kama utatumia dawa hii kwa lengo la kuzuia hedhi kwa muda maana unaweza kushika ujauzito usiotarajiwa.


Hata hivyo kama noreshisterone itatumika kila siku kwa dozi ya siku 21 au 28, itazuia kutungishwa kwa ujauzito. Muda wa kuzuia kubeba ujauzito unategemea utatumia dawa kwa muda gani.


Wapi utapata maelezo zaidi

Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Norethisterone na kuzuia ujauzito katika makala zingine ndani ya tovuti kwa vichwa vya habari vya;

  1. Je itachukua muda gani kushika ujauzito baada ya kuacha kutumia norethisterone?

  2. Dawa norethisterone

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

Imeboreshwa,

1 Aprili 2025, 08:53:23

Rejea za mada hii

  1. Bryant, G et al. “Is norethisterone a lifestyle drug? Health is not merely the absence of disease.” BMJ (Clinical research ed.) vol. 320,7249 (2000): 1605.

  2. Dean, Joshua et al. “Norethindrone is superior to combined oral contraceptive pills in short-term delay of menses and onset of breakthrough bleeding: a randomized trial.” BMC women's health vol. 19,1 70. 28 May. 2019, doi:10.1186/s12905-019-0766-6

bottom of page