Kipimo cha mimba kwenye mkojo huanza kuonesha uwepo wa mimba baada ya muda gani?
Kipimo cha mimba kwa kutumia mkojo hupima uwepo wa homoni hCG ambayo huzalishwa kwa wingi wiki kadhaa baada ya kukosa hedhi. Huchukua takribani siku 14 tangu kukosa hedhi kipimo kuweza kuonesha ujauzito.
Ingawa kikohozi kikavu ni dalili mojawapo ya maambukizi ya HIV, hutakiwi kuhofu endapo una dalili hii na umejianika kwenye kihatarishi kwa kuwa kinaweza kusababishwa na sababu zingine.
Unashauriwa kutoshiriki ngono wakati unatumia PEP ili kujikinga na maambukizi mapya pamoja na kumkinga mwenza wako dhidi ya maambukizi, ikishindikana, tumia kondomu.
Je, wamsaidiaje daktari kutambua ugonjwa kwa dalili?
Ili kutengeneza mawasiliano mazuri ya kutambua, kuchunguza na kukupa matibabu yanayoendana na shida yako, unapaswa kuelezea vema dalili kuu na dalili ambata.
PID hutibika na kuisha kabisa endapo itagunduliwa mapema na kutibiwa kwa dawa sahihi. Hata hivyo matibabu hayaondoi madhara na uharibifu wowote uliokwisha tokea kwenye mfumo wa uzazi kutokana na ugonjwa.
Kunguni ni mdudu anayejipatia chakula kwa kufyonza damu ya binadamu. Japokuwa hana madhara makubwa mwili, huweza kusababisha mzio kwenye ngozi kwa baadhi ya watu.
Unaweza kuambukizwa VVU kwa kung'atwa na mwathirika?
Maambukizi ya VVU yanaweza kutokea endapo kidonda cha kung'atwa kimekutana na majimaji, damu, shahawa, ute wa uke, uume au njia ya haja kubwa kutoka kwa mwathirika.
Vipo visa vichache vilivyoripotiwa kusababishwa na njia hii kiasi cha kuonekana kuwa na hatari kidogo ya maambukizi. Uambukizaji kwa njia hii hutegemea mambo mbalimbali baina ya mwathirika na anayeambukizwa