top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

 

Makundi ya vyakula

​

Utangulizi

​

Kuna aina tano za makundi ya vyakula, aina hizo humwongoza mtumiaji kupata afya njema ya mwili na kiakili pia. Vyakula vimewekwa kwenye makundi  ma 5 kwa sababu kila kundi huwa na virutubisho na madini yanayookaribia kufanana kwenye kundi hilo. Kwa mfano, virutubisho muhimu vilivyo kwenye maziwa, mtindi n.k mbadala wake wa kundi hili ni pamoja na madini ya kalisiamu na protini, wakati kundi la matunda ni chanzo kizuri cha vitamini, hasa vitamini C  ingawa inaweza kupatikana katika vyakula vingine vya kusindikwa.

 

Ili kukidhi mahitaji ya virutubisho muhimu kwa afya nzuri, unahitaji kula chakula kutoka kwenye kila kundi katika makudi matano ya chakula na kila siku na kwa kiasi  kinachopendekeza na wataalamu wa afya. 

​

Si lazima kula chakula kutoka katika kila kundi  katika kila mlo. Unaweza kutumia makundi matatu au zaidi ilimradi kwa wiki uwe umegusa makundi yote ya chakula. Ni muhimu pia kutumia aina mbalimbali ya vyakula ndani ya kila kundi moja katika makundi hayo matano kwa sababu vyakula mbalimbali hutofautiana kiasi cha viinilishe ilivyonavyo. Kwa mfano, katika kundi la mboga na kunde, mboga zenye rangi ya njano kama vile karoti na maboga huwa na kiasi kikubwa cha vitamini A kuliko mboga nyingine.
 

Makundi matano ya chakula katika makala hii ni pamoja na

 

1. Matunda

 

Aina mbalimbali za matunda hulimwa na hupatikana katika nchi za Afrika mashariki na Duniani kwa ujumla na hupatikana kwa msimu karibia mwaka mzima. Kuchagua matunda kutokana na msimu huleta thamani na ubora zaidi. Kula matunda kutokana na msimu wa matunda kunaongeza matumizi ya matunda aina nyingi zaidi kwa mlo wako katika mwaka mzima na kwa bei nafuu. Kama vile matumizi ya mboga za majani, kula matunda ya rangi tofauti huchangia kupata aina tofauti ya madini na virutubisho kwa ajili ya afya yako.

  

Matunda kutokana na kundi lake

​

  • Matunda kama vile pome  apple(tufaa) na peasi

  • Matunda jamii ya machungwa kama vile machungwa, mandarini na zabibu

  • Matunda jiwe  kama vile mapera, cherri, persiko, nektarini na skwash

  • Matunda hari kama vile ndizi, papai, maembe, mananasi na tikiti 

  • Matunda mengine kama vile matunda ya pasheni

 

Mboga mboga

 

Kundi la mboga pamoja na safu nyingi ya mboga na mazao yake, ikiwa pamoja na zile zilizosindikwa au  kuhifadhiwa kwa njia ya makopo, kukaushwa, mboga mfumo wa kimiminika au juisi ni kundi muhimu katika afya ya binadamu.

 

Kundi hili limegawanyika katika makundi madogo yenye virutubisho sawa, ambayo ni mboga za majai ya kijani, nyekundu na rangi ya machungwa, mboga zenye wanga, mboga za maharage na mbaazi. Madhumuni ya makundi haya madogo ni kukuongezea kula aina mbalimbali za mboga kutokana na virutubisho vyake.

 

Wanawake na wanaume hutumia kiwango sawa cha mboga za majani?

 

Hakuna utofauti kati ya wanawake na wanaume katika matumizi ya mboga hizi hivyo wanawake hula kiasi sawa na wanaume. Wanawake na wanaume hushauriwa kutumia vikombe viwili na nusu kwa siku, hawa ni wale walio kati ya umri wa miaka 19 hadi, wakati watu wazima zaidi ya miaka 50 lazima kupunguza ulaji wao wa kila siku kwa nusu kikombe

​

Soma zaidi kuhusu mboga za majani kwa kubonyeza hapa.

 

Vyakula vyenye protini

 

Nyama, kuku, samaki, dagaa, mayai, karanga, mbegu, bidhaa za soya na maharage, mbaazi huunda kundi la chakula chenye protini . Ingawa kunde na maharage zipo katika kundi la vyakula vyenye nyuzinyuzi vyakula hivi huwa ni chanzo cha vyakula vyenye protini. Inashauriwa kula nyama ya kuku na nyama kutoka kwenye samaki na vyakula vingine kama vinavyopatikana kwenye mimea ili kuongeza afya ya mwili wako kwa kutokula nyama nyekundu kama za wanyama wa kufugwa au wa polini.

 

Vyakulavya wanga (Nafaka)

 

Vyakula vya nafaka ni vingi vilivyotengenezwa kutokana na ngano, shayiri, mchele, mtama na mahindi. Nafaka mbalimbali zinaweza kupikwa na kuliwa nzima, kusagwa kuwa mfumo wa  unga na kupika aina mbalimbali ya vyakula kama mkate, ugali, uji, vitumbua, ama maandazi kwa ajili ya kifungua kinywa.


Vyakula vya nafaka  vinaweza kuvunjwa katika makundi manne madogomadogo. Kama vile

 

  • Mikate 

  • vifungua kinywa, uji wa shayiri, ngano, biskuti

  • Nafaka - Mchele, shayiri, mahindi, mtama, uwele n.k

  • Bidhaa nyingine – kama Pasta, keki, popcorn, unga n.k

​

Vyakula vya nafaka hutupatia wanga. Soma zaidi kuhusu vyakula vya wanga kwa kubofya hapa

 

Maziwa

 

Kundi la maziwa ni kundi lenye vyakula na mazao yake zikiwemo  bidhaa za maziwa na huwa na kiwango kikubwa cha madini ya kalsiamu. Maziwa ya mgando, jibini zaidi na bidhaa zote zenye maziwa ni sehemu ya kundi la chakula cha maziwa. hata hivyo maziwa ya soya pia huwa ni sehemu ya kundi la maziwa licha ya kukosa madini ya sodiamu kwa wingi, pamoja na maziwa ya soya siagi ya maziwa huhesabika pia katika  kundi la maziwa, Maziwa huwa muhimu na ni chanzo kizuri cha madini  kalsiamu. Inashauriwa kutumia maziwa au bidhaa za maziwa zenye mafuta kidogo kuzuia kupata kiwango kikubwa cha mafuta yenye lehemu mbaya (kolestro). Watu wa makamo ya kati na wanaofanya kazi wanashauriwa kutumia vikombe vitatu vya chai ya maziwa kwa siku

​

Je kuna makundi mengine ya vyakula?

​

Ndio, baadhi ya vitabu vimeelezea makundi ya vyakula kuwa ni matatu (3), ambayo yamegawanywa kulingana na kazi zinavyofanywa na vyakula hivyo ndnai ya mwili.

 

Makundi hayo matatu  ni;

​

  • Vyakula vinavyoupa mwili nguvu- Hivi ni vyakula vyote vyenye wanga mfano nafaka  mbalimbali na mazao yatokanayo na nafaka  mfano mahindi, mihogo, mtama, uwele na vyakula vingine kama viazi n.k

  • Vyakula vinavyojenga mwili- vyakula vyote vyenye protini kama samaki, nyama, maharagwe n.k

  • Vyakula vinavyoupa mwili joto- vyakula vya mafuta, mfano mafuta, karanga, siagi, n.k 

​

​

Nifanye nini ili kuishi maisha bora bonyeza hapa kusoma

​

​

ULY CLINIC inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na Tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile inayodhuru afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri wa chakula na tiba kwa kubonyeza hapa

​

 

Imeboreshwa mara ya mwisho, 29.06.2020

​

Rejea za mada hii

​

1. Eatfor health. gov.au. Five food types. https://www.eatforhealth.gov.au/food-essentials/five-food-groups. Imechukuliwa 29.03.2020

​

2. Maswali na majibu kutoka kwa daktari lishe wa ULY clinic kutokana na mswali yaliyoulizwa sana

​

3. 2015-2020 Dietary Guidelines for Americans. U.S. Department of Health and Human Services and U.S. Department of Agriculture. https://health.gov/dietaryguidelines/2015/guidelines. Imechukuliwa 29.03.2020

​

4.Duyff RL. Carbs: Sugars, starches, and fiber. In: Academy of Nutrition and Dietetics Complete Food and Nutrition Guide. Toleo la 5. New York, N.Y.: Houghton Mifflin Harcourt; 2017.

​

5. Encyclopedia of food. Toleo namba 1.  ISBN 9780122198038, 9780080530871.

bottom of page