top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Mambo ya kufanya ili kutoacha kuendelea kufanya mazoezi

Kuzingatia programu ya zoezi la aerobic

Kama ilivyo shida kumaliza dawa ulizoandikiwa na daktari, kuzingatia program ya zoezi la aerobic inaweza kuwa changamoto pia. Mara nyingi kizuizi kikubwa ni ukosefu wa muda kutokana na kazi na changamoto za  familia. Wakati unaona huna mda wa kufanya mazoezi, inashauriwa hivi

  • Kutumia siku ya kazi kwa ajili ya kutembea - Ili kuanza siku na mazoezi, weka gari lako mbali na kazini kwako na utembee dakika 10 kwenda kazini kwako. Wakati wa kula chakula cha mchana, tembea dakika 5 kwenda chakula kilipo kutoka kazini, na dakika 5 kurudi kazini kwako kutoka kwenye chakula. Masaa ya kazi yanapoisha, tembea dakika 10 mpaka ulipopaki gari lako ili uchukue na kwenda nyumbani. Kisha endelea kufanya hivi, siku zako zitakuwa zina pendeza.

  • Fanya mazoezi mwishoni mwa wiki - Ikiwa huwezi kufanya zoezi kwenye siku za wiki, fanya mazoezi mwishoni mwa wiki. Kutembea safari ya dakika 75 Jumamosi na Jumapili inaonekana kuleta faida za kiafya sawa sawa na kufanya mazoezi siku za wiki. Hata hivyo, ni jambo la busara kuanza kutembea taratibu hatua kwa hatua kwa dakika 75 ili kuepuka majeraha katika maungio ya mwili na matatizo mengine (kwa mfano, msuguano, namalengelenge kwenye maungio ya mwili). Pengine unaweza kuanza kutembea dakika 30 kila mwishoni mwa wiki mfululizo na kuongeza dakika tano kila wiki mpaka kufikia dakika 75.

  • Kuongeza kiwango cha kufanya mazoezi - Unapata manufaa sawa sawa kwa kupunguza siku za mazoezi kwa kuongeza nguvu zaidi kwenye mazoezi kwa siku unazoweza kufanya mazoezi. Mfano ukifanya mazoezi makali kwa mda wa dakika 25 kwa siku tatu za wiki tu huwa sawa na mtu anayefanya mazoezi ya wastani kwa mda wa dakika 30 siku tano za wiki.

  • Pata rafiki wa kufanya naye mazoezi - Tafuta mtu anaye jishughulisha au kujiunga na mazoezi ya kikundi kama ukikosa. Hii hukufanya kupenda mazoezi na kuwa ni suala la kawaida la kujifurahisha na huongeza uwezekano wa kuendelea kufanya mazoezi. Kujiunga na kikundi cha mazoezi (kama vile kundi la kutembea au kucheza tenisi au kuendesha baiskeli) hutoa faraja sana kwa mtu anayefanya mazoezi. Hata hivyo, kujiunga na kikundi huweza kuleta gharama zaidi endapo unalipia kuwa katika kikundi hiko mfano gym n.k

  • Mazoezi ya nyumbani - Kwa baadhi ya watu, mpango wa mazoezi ya nyumbani huhitajika kufanyika endapo mda mfupi wa mazoezi unahitajika. Kama una uwezo wa kutumia baiskeli ya nyumbani au treadmill bila kuendesha kusafiri kwenda kwenye mazoezi huwa ni suluhisho kubwa. Hata hivyo, vifaa vya mazoezi vyenye ubora vinaweza kuwa ghali sana na mara nyingi shauku ya awali ya kutumia vifaa hivyo hupungua na mtu huweza acha mazoezi mwisho wake.

  • Tumia programu za video(picha mjongeo)- Njia nyingine ya kuwasaidia watu kufanya zoezi la kawaida la aerobic ni kutumia programu ya DVD au video. Programu hizi huweza kuwa za yoga aumazoezi ya  aerobics, Hata hivyo, watumiaji wanapaswa kuhakikisha kuwa programu iliyochaguliwa inafaa kwa kiwango cha afya na malengo yao, na imeundwa vizuri na maelekezo sahihi kuhusu mbinu za zoezi.

  • Kujiunga na mazoezi au kufanya mazoezi na mtaalamu wa Mazoezi - Kujiunga na mazoezi ya GYM au kufanya kazi na kocha mwenye ujuzi wa mazoezi au mtaalamu wa afya inaweza kuwa na manufaa sana kwa baadhi ya watu wanaojitahidi kufuata programu ya mazoezi. Mashirika kadhaa ya wataalamu, huzalisha wataalamu wenye ustadi na vyeti vya ustadi. Mtaalamu mwenye ujuzi anaweza kukusaidia kuunda mfumo wa zoezi unaofaa hali yako ya afya na malengo yako, huku akikupa mwongozo juu ya mbinu sahihi ili kukusaidia kuepuka kuumia n,k. Gym licha ya kuwa sehemu salama na ya kuvutia kwa mazoezi, inaweza pia kutoa fursa ya kukutana na watu wengine wanaofanya mazoezi na hukufanya  kukufurahisha zaidi, na kusababisha kuzingatia mazoezi zaidi. Endapo huwezi hudhuria GYM unaweza kutumia mbinu zingine zilizoongelewa hapo juu

Toleo la 2

Imeboreshwa 4/12/2018

bottom of page