Mada hii imezungumziwa kwenye maeneo haya
​
Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic
Maotea sehemu za siri-Genital warts
Maana
​
Maotea sehemu za siri ni aina mojawapo ya ugonjwa wa zinaa unaotokea si kwa nadra sana na huambukizwa kwa njia ya zinaa. Nusu ya wanao jihusisha na ngono mara kwa mara haswa isiyo salama hupata maambukizi ya virusi hawa kwenye kipindi fulani katika maisha yao. Wanawake wana patwa sana na maotea haya kuliko wanaume.
Kama jina lilivyo maotea haya hudhuru sehemu za siri zilizo na umande kwenye maeneo ya siri. Maotea haya huweza kuonekana kama kitu mwinuko mdogo mrefu au kuwa na umbo la uwa lililosambaa. Kwa watu wengi huwa na umbo dogo sana na kuonekana kwa shida.
Kama maotea yanayoweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, maotea sehemu za siri husababishwa na maambukizi ya kirusi cha Human papilloma (HPV). Baadhi ya aina ya virusi hawa huweza kusababisha saratani za aina nyingi kama saratani ya shingo ya kizazi. Kuna chanjo pia ya kuzuia kupata baadhi ya virusi hawa wa HPV.
Pata tiba kutoka kwa madaktariw a ulyclinic popote ulipo, wasiliana nasi sasa kwa tba na ushauri kwa kubonyeza hapa au kupiga simu kwa namba zilizo chiniya tovuti hii
​
Endelea kusoma kuhusu, Dalili, Visababishi, Vihatarishi, Madhara, Vipimo na uchunguzi, Matibabu, Chanjo, Pata Tiba Kutoka Hapa ULY CLINIC popote ulipo.
​