Kuhisi mapigo ya moyo kubadilika baada ya kula
​
Imeandikwa na madaktari wa ulyclinic
​
​
Utanguliza
​
Kuhisi Mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo baada ya kula (kwenda kasi/ kwa haraka au kwenda taratibu) husababishwa na moyo kuruka au kuongeza pigo. Mtu anaweza kuhisi mapigo ya moyo yanaenda ndivyo sivyo kifuani, shingoni au kooni ambapo hupata hisia za kugongagonga au kupwita pwita. Hali, magonjwa na matumizi ya vyakula na dawa mbalimbali huweza kusababisha mapigo ya moyo kwenda kasi kama dawa, mazoezi makali na kula chakula aina Fulani. Mapigo ya moyo kwenda kasi pia husababisha mapigo ya mishipa ya damu kwenda haraka haraka.
​
Mapigo ya moyo kwenda kasi mara nyingi hayamaanishi kuwa kuna tatizo kwenye mwili au kuna ugonjwa mkubwa unaoendelea ndani ya mwili. Hutakiwi kuwa na hofu au kuhangaika kutafuta tiba, cha msingi fanya uwezavyo kujikinga na kisababishi mfano acha kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu(sukri kwa wingi), vyakula vyenye karafuu, kahawa na baadhi ya dawa, jaribu kufanya mazoezi na kuvuta hewa kwa kina zaidi.
​
Endapo mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo yanaambatana na dalili za kuishiwa pumzi, kizunguzungu, maumivu ya kifua au kuzimia, unatakiwa kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
​
​
Visababishi
​
Vitu au mambo yanayoweza sababisha mapigo ya moyo kwenda kasi vinaweza kuwa vya aina kadhaa , vingine vinauhusiano na moyo, kutokuwa na mahusiano na moyo au kutojulikana kabisa. Sababu zisizo husiana na moyo ni;
​
-
Hisia kali kama huzuniko au sononeko
-
Kufanya kazi za kuutumikisha mwili kwa haraka sana
-
Vyakula vyenye karafuu, nikotini, pombe na dawa za kulevya kama kokeini
-
Magonjwa kama ugonjwa wa upungufu wa homoni ya thyroid, kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu, upungufu wa damu, shinikizo la chini la damu, na kuishiwa maji mwilini.
-
Matumizi ya dawa kama dawa ya kuongeza au kupunguza hamu ya kula, dawa za pumu, dawa za kuponya kuponya mafua, dawa za kutibu moyo na dawa za kutibu upungufu wa homoni ya thyroid
-
Matumizi ya dawa za mitishamba na mizizina dawa za kuongeza virutubisho mwilini n.k
-
Kuwa na kiwango cha madini kisicho cha kawaida
​
Baadhi ya visababishi vya mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo ni magonjwa ya moyo, mfano mshituko wa moyo, magonjwa ya mishipa ya moyo ya koronari, kuferi kwa moyo, magonjwa ya milango ya moyo, magonjwa ya kuta za moyo.
​
Endapo umepata shida na unajua kisababishi ni vema ukaepuka. Na kama shida yako huijulikani kisababishi ni vema kuongea na daktari wako ili upate uchunguzi zaidi.
​
Baadhi ya maelezo ya undani kuhusu visababishi vya mapigo ya moyo kwenda kasi yameandikwa hapa chini;
​
Kuendelea kusoma kuhusu visababishi na matibabu bonyeza hapa kwa kutumia email yako kisha usome
​
ULY CLINIC Inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
​
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 09.07.2020