top of page
-
Kikohozi cha ukimwi kikoje?Ingawa kikohozi kikavu ni dalili mojawapo ya maambukizi ya HIV, hutakiwi kuhofu sana endapo una dalili hii. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kikohozi kikavu kama vile; kucheua tindikali, ugonjwa wa sinazi, maambukizi ya chlamydia au mwitikio wa mwili kwenye hewa ya baridi na sababu zingine. Jambo la msingi utatakiwa kufanya ni kuonana na daktari wako endapo kikohozi kitaendelea kwa muda mrefu kwa uchunguzi.
-
UKIMWI au VVU husababisha kikohozi kikavu?Ndio! Maambukizi ya VVU au UKIMWI unaweza kusababisha kikohozi kikavu. Hii ni kwa sababu VVU hupunguza uwezo wa mwili kupambana na maambukizi na magonjwa mengine ambayo huathiri mfumo wa hewa na kuleta dalili ya kikohozi kikavu. Kusoma zaidi kuhusu dalili za ukimwi bofya linki inayofuata https://www.ulyclinic.com/foramu/majadiliano-na-wataalamu/dalili-za-ukimwi-ni-zipi au https://www.ulyclinic.com/ukimwi
-
Je kikohozi kikavu kwa mgonjwa wa VVU hudumu kwa muda gani?Dalili za ukimwi zinaweza kutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, vivyo hivi kutokea na kupotea kwa kikohozi kikavu hutegemea kinga ya mwili ya mtu dhidi ya maradi, hivyo huweza kudumu kwa muda wa wiki chache hadi miezi kadhaa na kwa baadhi ya watu kikohozi huwa hakiishi haswa endapo mgonjwa yupo kwenye hatua za mwisho za maambukizi ya VVU/UKIMWI.
-
Kikohozi kibichi ni dalili ya UKIMWI?Ndio! Endapo kinga ya mwili ni dhaifu kutokana na maambukizi ya VVU, na kutotumia dawa, mwili hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ya mfumo wa upumuaji. Anayeishi na maambukizi ya VVU anaweza kupata magonjwa ya mfumo wa hewa kama Nimonia n.k ambayo hupelekea dalili za kikohozi kibichi n.k Soma majibu zaidi kwenye makala ya dalili za ukimwi kwenye mfumo wa hewa.
-
Je ukiwa unatumia PEP unaweza shiriki ngono na mpenzi wako?Kama itashindikana kutoshiriki ngono wakati unatumia PEP, unashauriwa kutumia kondomu ili kumkinga mwenza wako dhidi ya maambukizi ya VVU. Mambo mengine unayoshauriwa kuepuka ni kushiriki vifaa au sindano ya kudunga dawa za kulevya. Maelezo zaidi unaweza kupata kwa mtaalamu wa afya katika kituo cha afya karibu nawe au kuwasiliana na daktari wa ULY CLINIC kupitia mawasiliano chini ya tovuti.
-
Dalili za ukimwi kwenye ulimi ni zipi?Virusi vya UKIMWI huathiri kinywa na ulimi hivyo kuleta dalili mbalimbali ambazo kwa baadhi ya watu huwa ni dalili ya awali. Dalili za UKIMWI kwenye ulimi ni pamoja na; Utando mweupe kwenye ulimi mithiri ya uji au pamba au kama maziwa mazito- hii ni kutokana na kuzaliana kwa kasi kwa fangasi wanaoishi ndani ya kinywa. utando huweza kuonekana pia kwenye kwenye kona, sakafu na paa la kinywa na huleta hisia za kuwa na pamba kinywani na kupotea kwa ladha. Endapo utando utakwanguliwa huwa unatoka. Mabaka meupe kwenye mikunjo na kingo za ulimi. Mabaka hayo yanaweza kujitenga mithiri ya nywele nyeupe, hata hivyo huweza tokea eneo lolote lile la ulimi. Kutokea kwake hakuambatani na dalili ya maumivu na huwa hayatoki hata yakikwanguliwa. Kisababishi huwa ni kuamka kwa maambukizi ya kisuri cha Epistein Bar (EBV). Vidonda homa mdomoni kutokana na maambukizi ya virusi vya Hepes simplexx 1 na 2. Ingawa vidonda hipi huonekana sana kwenye midomo, pia huweza kutokea kwenye ulimi na ndani ya kuta za kinywa kwa wagonjwa wa UKIMWI. Mabaka meusi kwenye ulimi. Mabaka haya hufanyika sana kwa watu wenye asili ya afrika, ingawa hutokea sana kwenye kuta za kinywa, mabaka haya pia huweza kuonekana kwenye ulimi. Ulimi huonekana kuwa na mabaka ya kahawia kuelekea nyeusi au meusi, inaweza kuwa baka moja au mengi. Hii inaweza kusababishwa na Virusi vya UKIMWI au dawa zinazotumika kupambana na maambukizi ya VVU Kuota kwa Chunjua, hii husababishwa na maambukizi ya human papillomavirus (HPV) ambacho huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kubusiana. Chunjua huweza kuwa na mwonekano wa rangi nyeupe au pinki isiyokolea au kijivu na huweza kuwa na mwonekano pia kama wa ua lililochanua
-
Vifaa vya kupima UKIMWI ni vipi?Vifaa vya kupima UKIMWI (Vitambuzi) kwa muda mfupi ni; SD- bioline Unigold
-
Virusi vya UKIMWI huishi muda gani?Virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa saa 1 hadi siku 42 ikitegemea mambo yafuatayo wingi wa virusi, wingi wa damu, joto, unyevu kwenye hewa na mwanga wa jua. Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi kwenye sindano ya tundu Virusi vinaweza kuishi muda mrefu zaidi kwenye sindano ya kuchomea dawa endapo joto na hali ya hewa havibadiliki badiliko. Mfano endapo sindano imewekwa kwenye jokofu, virusi vilivyo kwenye sindano vinaweza kuishi hadi siku 42 Endapo sindano hii ipo kwenye joto la mazingira, virusi vya UKIMWI vinaweza kuishi muda wa siku 7. Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye manii/shahawa Mara baada ya mbegu za kiume kutoka nje ya mwili, huanza kufa mara moja kutokana na kupigwa na hewa pamoja na joto la mazingira. Hivyo inachukua saa1 hadi 2 kuwa havina uwezo wa kuambukiza endapo mbegu hizo zimekauka kabisa. Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye damu iliyokwenye mazingira Asilimia 90 hadi 99 ya virusi hufa ndani ya masaa kadhaa baada ya damu au majimaji kupigwa na hewa, mwanga wa jua na kukauka katika joto la mazingira. Muda wa virusi vya UKIMWI kuishi Kwenye maji Virusi vya UKIMWI endapo vitawekwa kwenye maji huchukua muda wa masaa nane kupoteza uwezo wake wa kuambukiza (hufa). Hata hivyo ndani ya masaa 2 kwenye maji, ni asilimia 10 tu ya virusi vinawez akuishi na muda unavyoongezeka, idadi a virusi huwa 0 baada ya masaa 8.
-
Bei ya kipimo cha UKIMWI ni shilingi ngapi?Kipimo cha UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma za afya za serikali ni bure, hata katika baadhi ya hospitali binafsi zinazopokea masaada wa vipimo. Kwenye hospitali za kulipia huduma, bei ya kipimo hiki inaweza kuwa kati ya shilingi elfu 1 hadi 10.
-
Kupima UKIMWI kwa kutumia simu?Kwa sasa hakuna tekinolojia yenye uwezo wa kupima UKIMWI kwa kutumia simu. Vipimo vya UKIMWI ni vya kutumia damu, mate pamoja na kitambuzi cha UKIMWI kama SD bioline, Unigold n.k Hata hivyo unaweza kutumia huduma za ULY CLINIC au zingine kupata majibu ya KIPIMO kwenye simu endapo utakuwa umeacha sampuli ( umechukuliwa sampuli) na huna muda wa kuubiria majibu.
-
Jinsi ya kupima UKIMWI kwa kutumia mate?Jinsi ya kupima UKIMWI kwa kutumia mate; Chukua kichukua sampuli ya mate kisha pitisha kwenye fizi za juu na chini mara moja ili kukusanya sampuli kisha Weka sampuli yako kwenye kipimo, sehemu ya kuweka sampuli Endapo sampuli ni ya kutosha, haina haja ya kuweka bafa ( endapo sampuli ni kidogo weka matone 2 ya bafa Subiri sampuli itembee kwenye kipimo Soma majibu ya kipimo ndani ya dakika 15 Tafiti zinaonyesha, matumizi ya mate inaweza kuwa njia mbadala ya kutumia damu. Majibu ya kipimo cha UKIMWI kwenye mate inaweza kugundua kwa asilimia 99. Endapo una kipimo maalumu cha kutumia mate, pitisha kichukua sampuli mara moja kweney fizi za juu, kisha fizi za chini na kisha kiunganishe kwenye kipimo chako na soma majibu ndani ya dakika 20. Kumbuka: Kupima UKIMWI Kwa kutumia mate inahitaji uwe na kipimo ambacho kimetengenezwa kupima uwepo antibodies za VVU kwenye mate, endapo utatumia kipimo kisicho sahihi unatoa uwezekano wa kupata majibu yasiyo sahihi.
-
Mistari mitatu kwenye kipimo cha UKIMWI humaanisha nini?Mistari mitatu kwenye kipimo cha UKIMWI humaanisha kuwa una maambukizi ya kirusi cha UKIMWI namba 1 na 2 Kuna aina mbili za Virusi vya UKIMWI, Kirusi cha UKIMWI 1 Hupatikana duniani kote Huongoza maambukizi kwa binadamu Maambukizi huelekea ugonjwa wa UKIMWI haraka zaidi Kirusi cha UKIMWI 2 Ni nadra sana kuambukizwa kwa binadamu Maambukizi huchelewa kuelekea kwenye ugonjwa wa UKIMWI Hupatikana sana afrika magh'aribi. Hivyo endapo mistari mitatu itaonekana kwenye kipimo cha SD bioline, hii inamaanisha una maambukizi ya Virusi vyote viwili.
-
Vipimo vya UKIMWI vinapatikana wapi?Vipimo vya UKIMWI vinapatikana kwenye vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na Kituo cha ushauri nasaha (CTC), hata hivyo unaweza kupata vipimo hivi kwa kununua kwenye baadhi ya maduka ya dawa moto (pharmacy). Endapo unahitaji kupima maambukizi ya VVU, fika kituo cha ushauri nasaha au kituo cha afya karibu nawe kwa kupima bure.
-
Kuna aina ngapi ya virusi vya UKIMWI?Kuna aina mbili za Virusi vya UKIMWI, Kirusi cha UKIMWI 1 na Kirusi cha UKIMWI 2 Kirusi cha UKIMWI 1 Hupatikana duniani kote Huongoza maambukizi kwa binadamu Maambukizi huelekea ugonjwa wa UKIMWI haraka zaidi Kirusi cha UKIMWI 2 Ni nadra sana kuambukizwa kwa binadamu Maambukizi huchelewa kuelekea kwenye ugonjwa wa UKIMWI Hupatikana sana afrika magh'aribi. Soma zaidi kuhusu virusi vya UKIMWI kwa kubofya hapa
-
Ukinywa magnesium unaweza kunywa pombe?Kunywa magnesium citrate husaidia watu wenye haja ngumu kupata choo laini au kuharisha. Endapo utachanganya pombe na dawa hii, hali ya kuharisha itazidi pamoja na maudhi mengine yanayotokana na dawa ya magnesium citrate ambayo ni; 1. Maumivu ya tumbo 2. Kuunguluma kwa tumbo 3. Kichefuchefu na kutapika 4. Kuzidi kwa kiwango cha magnesium kwenye damu 5. Kubadilika kwa madini ndani ya damu kama vile madini ya sodiamu, kalisiamu na potasiamu
-
Faida za madini ya zinc wakati wa ujauzito ni zipi?Kunywa vidonge vya zinki au kupata zinc kutoka kwenye chakula huwa na faida nyingi kwa mama mjamzito. Madini ya zinc yameonekana kupunguza kwa kiasi kujifungua kabla ya umri kufika, lakini haizuii matatizo mengine kama kuzaliwa na uzito mdogo. Wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa na wajawazito huwa na upungufu kiasi au wastani wa madini ya zinc. Faida zingine za madini ya zinc kwa mjamzito ni; 1. Kuimairhsa kinga ya mwili 2. Kusaidia uzalishaji wa seli 3. Kutengeneza protini 4. Kuponya majeraha 5. Kusaidia umeng'enyaji wa wanga 6. Kuimarisha ladha na harufu ya chakula
-
Je mama mjamzito anaweza tumia vidonge vya kuongeza madini ya zinki?Ndio! Kazi kuu ya zinc ni kufanya seli zizalishwe, utengenezaji wa protini muhimu na ukuaji, hii inamaanisha kuwa madini haya ni muhimu sana wakati wa ujauzito. Kwa vile wakati wa ujauzito kunakuwa na upungufu wa madini na vitamini muhimu kama zinc, madini chuma, foliki acid n.k kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mama na mtoto aliyepo tumboni, mama mjamzito anapaswa kupata anapazwa kupata madini na vitamini hizo kutoka kwenye vyakula au vidonge.
-
Upigaji punyeto mara kwa mara huchangia mbegu za kiume kutoka na damu?Hapana! Kutokwa na damu kwenye mbegu za kiume huitwa kwa lugha ya kitiba 'hematospermia', hufahamika pia kama 'damu kwenye bao', ni dalili inayotokea sana kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka 40. Kutokea kwa dalili hii huwatia hofu wanaume wengi, hata hivyo visababishi huwa si vya hatari mara nyingi na dalili hupotea bila matibabu. Kutokana na tafiti, kupiga punyeto au masterbation si kisababishi cha damu kwenye mbegu za kiume bali kuna sababu zingine zinazopelekea. Soma kvisababishi vya kutokwa na damu kwenye mbegu za kiume kwa kubofya linki chini ya maelezo haya 1. https://www.ulyclinic.com/damu-kwenye-mbegu-za-kiume
-
Ni nini husababisha kutokwa na damu kwenye shahawa?Damu kwenye shahawa kwa lugha tiba hufahamika kwa jina la 'hematospermia' ni dalili ya shida fulani kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume. Hata hivyo mara nyingi kisababishi huwa hakifahamiki. Baadhi ya visababishi vya kujirudia rudia kutoa shahawa zilizochanganyika na damu ni matatizo kwenye mfumo wa mkojo au uzazi kama; 1. Maambukizi kama magonjwa ya zinaa n.k 2. Madhaifu ya kiuumbaji 3. Uvimbe 4. Majeraha 5. Kutolewa tezi dume 6. Madhara ya matibabu kama kuwekewa mpira njia ya mkojo n.k 7. Magonjwa ndani ya mwili 8. Ngono haribifu kama kufunga au kuingiza vitu ndani ya uume au tezi dume
-
Dawa nzuri ya taifodi ni ipi?Dawa yoyote ile inayofahamika kutibu taifodi ni nzuri isipokuwa endapo bakteria ana usugu na dawa hiyo! Taifodi ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria mwenye jina la Salmonela typhi, au salmonella paratyphi kwa baadhi ya watu. Dawa nzuri ya kutibu typhoid ni ile ambayo inauwezo wa kuua vimelea hawa. Endapo bakteria amekuwa sugu kwenye dawa, basi ni vema ukafanya kipimo cha kuotesha bakteria na kutambua dawa gani inafaa kinachotwa kwa jina jingine la 'Culture na Sensitivity test' Kusoma zaidi kuhusu dawa zinazotibu taifodi bofya linki inayofuata; 1. https://www.ulyclinic.com/dawa-za-kutibu-taifod
-
Dawa zenu nazipataje?ULY CLINIC inatoa huduma ya ushauri na tiba kupitia njia mbalimbali; Endapo unatumia huduma za mtandaoni au upo mbali na Arusha, dawa zetu unaweza kupata kwa njia ifuatayo; 1. Kutumiwa kwenye basi endapo dawa haipatikani sehemu ulipo 2. Kuandikiwa cheti ili ununue sehemu ulipo 3. Kupewa dawa mkononi endapo upo karibu na clinic yetu Endapo unahitaji kujiunga na huduma za ushauri na dawa mwaka mzima jiunge kwa kubofya linki inayofuata chini. Maelezo ya namna ya kujiunga na gharama vimeandikwa kwenye linki hii. 1. https://www.ulyclinic.com/copy-of-ushauri-dawa-bure-mwaka-mzi
-
Dawa iitwayo TINIDAZOLE inatibu nini?Tinidazole ni dawa ya kutibu maambukizi ya protozoa, inayotumika kutibu magonjwa mbalimbali ikiwa yenyewe au pamoja na mchanganyiko na dawa zingine. Magonjwa yanatibiwa na dawa hii yenyewe aukuchanganywa na dawa zingine ni; -Trichomoniasis( moja ya ugonjwa wa zinaa) -Giardiasis -Amebiasis (amiba) -Vaginosis kutokana na bakteria (BV)
-
Dawa ya amoxicillin inatibu nini?Dawa ya amoxicillin watu wengine huita kama amoxilini huwa na uwezo wa kutibu magonjwa yafuatayo; - Nimonia kwa watu wazima - Jipu kwenye jino - UTI - Maambukizi kwenye masikio ( otitis) - Nimonia kwa watoto - Maambukizi ya bakteria kwenye ngozi - Maambukizi ya bakteria kwenye koo na kinywa - Maambukizi ya bakteria kwenye njia za hewa ( Bronchitis) Licha amoxicillin kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa hayo, dawa hii hutibu magonjwa yaliyoorodheshwa endapo yamesababishwa na bakteria wafuatao; - H. influenzae - N. gonorrhoea, - E. coli - Pneumococci - Streptococci, na - Strain kadhaa za Staphylococci. Ili kufahamu dawa inayokufaa ni vema ukawasiliana na daktari wako kujua ugonjwa ulionao unasababishwa na bakteria gani na endapo dawa hii bado ina uwezo wa kutibu katika eneo unaloishi ( yaani endapo bakteria hawajawa sugu kweye dawa). Epuka matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari ili kuepusha usugu wa vimelea kwenye dawa.
-
Dawa za kutibu minyoo ni zipi?Dawa zinazotumika kutibu minyoo ni; Albendazole Diethylcarbamazine Ivermectin Levamisole Niclosamide Praziquantel Tiabendazole Kusoma zaidi kuhusu dawa za minyoo ingia kwenye linki kwa kubofya hapa
-
Nina ujauzito wa mapacha wa wiki 33, nimechoka sana je ni dalili za kujifungua?"Kuchoka sana ni dalili ya kuelekea kujifungua endapo inaambatana na dalili za awali za kujifungua ambazo ni; 1. Kupungua kwa kimo cha mimba ( kushuka kwa mtoto) 2. Kufunguka kwa shingo ya kizazi 3. Maumivu ya tumbo la chini yanayoongezeka 4. Hisia za kulegea kwa maungio ya mwili 5. Kuharisha 6. Kutoongezeka uzito 7.Uchofu mkali kupitiliza na wakati mwingine inafuatiwa na kupata nguvu nyingi 8. Majimaji ya ukeni kubadilika rangi 9. Kupasuka kwa chupa ya uazi Endapo una ujauzito mapacha na una wiki 33 na unapata dalili hizi, ni vema kuwahi hospitali kwa uchunguzi na tiba kwani kwa wiki hizi mapafu yamtoto bado hayajakomaa na unahitaji kupewa matibabu sahihi kunusuru afya ya mtoto na wewe. Si lazima uwe na dalili zote, lakini inatakiwa uwe na dalili nyingi ili kuweza kusema unakaribia kujifungua.
-
Kusinyaa kwa ini husababishwa na nini?Visababishi vikuu vya ini kusinyaa vinavyofahamika kutokana na tafiti mpaka sasa ni; Unywaji wa kupindukia wa pombe Ugonjwa wa ini mafuta Ugonjwa sugu wa homa ya ini (kutokana na maambukizi ya virusi vya homa ya ini B au C) Kusinyaa kwa ini, kwa ligha tiba 'cirrhosis', ni tatizo linalotokea endapo ini limeonekana kuwa na urefu chini ya sentimita 7 na kuwa na makovu mithiri ya nundu. Hata hivyo hatua za mwanzo za ini kusinyaa huanza na kuvimba kwa ini ndipo kusinyaa hufuata. Soma zaidi makala ya kusinyaa kwa ini kwa kuandika 'Ini kusinyaa' kwenye kiboksi cha 'Tafuta chochote hapa...'
-
Majibu ya vipimo vya damu kwa ini lililosinyaa yakoje?Majibu ya vipimo vya msingi vya ini lililosinyaa ni; Kuongezeka zaidi kwa kiwango cha kimeng'enya cha Alanine aminotransferase (ALT) – hii hutokea kwa kila kisababishi cha kusinyaa kwa ini Kuongezeka kwa kiwango cha kimeng'enya cha Aspartate aminotransferase (AST) – hii hutokea kwa kila kisababishi cha kusinyaa kwa ini Kiwango cha kimeng'enya cha Alkaline phosphatase (ALP) –Mara nyingi huwa cha kawaida au kuongezeka kiasi kidogo. Kiwango cha jumla cha bilirubin – Kemikali inayozalishwa na ini tu, mara nyingi huwa cha kawaida au au kuongezeka kiasi kidogo. Hata hivyo endapo kusinyaa kwa ini kupo hatua za mwisho, kiwango cha Bilirubin huongezeka mara dufu Kiwango cha protini Albumin –protini inayotengenezwa na ini, mara nyingi hupungua Majibu mengine ya vipimo vya ini lililosinyaa ni; Kipimo cha jumla ya chembe nyeupe za damu (CBC) – huweza kuagizwa fanyika kuchunguza chembe ulinzi na chembe sahani za damu. Mara nyingi chembe sahani za damu huwa hupungua kwa wagonjwa wenye ini lililosinyaa. Muda wa damu kuganda (Prothrombin time( (PT/INR) – kwa sababu vigandisha damu vingi hutengenezwa na ini, muda wa damu kuganda huongezeka( damu inachelewa kuganda) kwa wagonjwa wenye ini lililosinyaa. Maelezo ya ziada Ini lililosinyaa kwa kuwa haliwezi kufanya kazi yake ipasavyo( inategemea limesinyaa kwa kiasi gani) siku zote huwa na dalili zingine zinazoonekana kwenye vipimo. Vipimo vya damu vinavyofanyika na majibu yake kwa mgonjwa mwenye ini lililosinyaa husomeka kama ilivyoeleewa hapo juu.
-
Visababishi vya kifo kwa mgonjwa wa ini lililosinyaa ni nini?Kutokana na tafiti zilizofanyika (PUBMED), visababishi vya kifo kwa wagonjwa wenye ini lililosinyaa ambavyo vilionekana kwa kuwafuatilia wagonjwa wa ini lililosinyaa kwa miaka 16 vilivyoorodheshwa hapa chini; - Kuferi kwa ini ( asilimi 24 ya vifo) - Kuvuja kwa damu mfumo wa umeng'enyaji chakula ( asilimia 14 ya vifo) - Kkuvuja kwa damu na ini kuferi kwa pamoja (Asilimia 13 ya vifo) - Saratani ya ini ( Asilimia 4 ya vifo) - Magonjwa mengine ya ini ( asilimia 2 ya vifo) - Maambukizi mwilini ( asilimi 7 ya vifo) - Magonjwa ya moyo ( asilimi 22 ya vifo) - Saratani nje ya ini ( asilimi 9 ya vifo) - Visababishi vingine visivyohusiana na ini ( asilimi 5 ya vifo)
-
Hatua za ini kusinyaa ni zipi?Kuna hatu nne zinazofahamika mpaka sasa za ini kusinyaa, hatua hizo na maelezo kwa kila hatua ni; Hatua ya kwanza: Sehemu tu ya ini limesinyaa, dalili chache huonekana na ini huwa na uwezo wa kufanya kazi zake kufidia sehemu ya ini iliyofeli. Hakuna madhara. Hatua ya pili: Hutokea na kuonyesha dalili ya kuzidi kuongezeka kwa shinikizo la damu kwenye ini na kupasuka kwa mishipa ya damu ya umio( inayosababisha kupata choo cheusi au kutapita damu). Hatua ya tatu: Huonekana kwa maji kukusanyika kwenye tumbo na kusababisha mwonekano wa tumbo lililovimba, ini huwa na makovu mengi zaidi, na mgonjwa hupata madhara makubwa hata ini linaweza kufeli kabisa. Hatua ya nne: Hatua hii ni tishio kwa maisha ya mgonjwa, ini huwa lipo kwenye hatua ya mwisho ya kufeli na ili mgonjwa aendelee kuishi ni lazima apandikizwe ini jingine.
-
Hatua dalili za ini lililosinyaa ni zipi?Kuna hatua dalili mbili za ini lililosinyaa ambazo ni; - Kusinyaa bila dalili Hatua hii ni ngumu sana kutambua kama ini limesinyaa kwa sababu mgonjwa huwa hana dalili yoyote na huendelea na maisha yake kama kawaida. Hii ni kwa sababu sehemu ya ini iliyo nzima hujitahidi kufanya kazi ili kutoonyesha mapungufu. - Kusinyaa na dalili Hatua hii huwa mbaya wakati wote kwa sababu mapungufu ya ini huanza kuonekana na dalili zote za ini kusinyaa huanza kuonekana na ukali huonekana kwa jinsi siku zinavyokwenda. Dalili hizo ni pamoja na kuvilia damu ndani ya umio, kuvimba tumbo na mwili, kuongezeka kwa shinikizo la damu la ini n.k
-
Kipimo tambuzi cha ini kusinyaa ni kipi?Mpaka sasa, kipimo tambuzi ambacho ulimwengu wote unakitumia ni kipimo cha histoloji ya tishu za ini: Kipimo hiki hufanyika kwa kukata kinyama kwenye ini kisha kwenda kukitazama kwenye hadubini, hufanyika na mtaalamu wa patholojia. Kinachoangaliwa na muundo wa ini ambao huwa umeharibika na huonyesha uwepo wa manundu yaliyozungukwa na tishu ngumu za makovu. Wagonjwa wanaopaswa kufanya kipimo hiki ni wale ambao hawana dalili za ini kusinyaa, hakuna faida za wagonjwa walio na dalili kufanya kipimo hiki kwani vipimo vingine vya awali vinatosha na kipimo hiki hakitabadili matibabu au hatua za ugonjwa.
-
Kipimo cha ultrosound huonyesha nini endapo ini limesinyaa?Kipimo cha Ultrosound huonyesha dalili zifuatazo kuashiria ini limesinyaa; - kuta za Ini kuwa na manundu nundu - Kuvimba kwa bandama - Kuonekana na mishipa mchepuko ya damu- ( damu kupita kwenye mishipa isiyo ya awali) - Kuvimba kwa upande wa kushoto wa ini - Kusinyaa kwa upande wa kulia wa ini - Maji ndani ya kuta za tumbo
-
Kusinyaa kwa ini huwa endelevu?Ndio! Kusinyaa kwa ini huwa endelevu pale tu endapo kisababishi kinaendelea kuwepo, hii imaanisha kuwa endapo kisababishi kimefahamika na kundolewa, mfano endapo ksiababishi ni pombe na pombe ikaachwa, au ni virusi vya hepatiti B na C na mtu akapata matibabu sahihi, kusinyaa husimama na wakati mwingine ini hujaribu kurudisha umbile la mwanzo, haswa endapo kuna sehemu ya ini ambayo bado haijaathiriwa na makovu.
-
Mgonjwa wa ini lililosinyaa anaweza ishi muda gani toka amegunduliwa?Wastani wa umri wa kuishi kwa mgonjwa mwenye hatua za mwisho za kusinyaa kwa ini kutokana na tafiti ni takribani miezi sita (6) hadi miaka miwili (2) na hii hutegemea pia madhara yaliyojitokeza. Endapo hakutafanyika upandikizaji wa ini, umri wa kuishi hufikia au kuzidi asilimia 50 ya umri wa mtu kuishi kwa wagonjwa wenye ini lililosinyaa kwa sababu ya pombe. Umri wa kuishi huwa mkubwa zaidi ya miaka 12 endapo hakuna madhara makubwa ambayo yameshatokea. Mambo ya msingi kufanya endapo tatizo limegunduliwa katika hatua za awali na una kisukari au ugonjwa wa obeziti ni kupunguza uzito na kudhibiti kisukari ili kupunguza mafuta kwenye ini haswa endapo kusinyaa kumesababishwa na ini mafuta.
-
Endapo nimetumia dawa za kutoa mimba na nimetokwa na damu siku moja tu ikakata nitajuaje kuwa mimba imetoka?Endapo umetumia dawa za kutoa mimba, na umetokwa na damu siku moja ikakata, kipimo pekee na cha haraka cha kufahamu mimba imetoka au la ni kwa kupiga Ultrosound tu. Kipimo mkojo kuangalia uwepo wa homoni ya HCG kitaendelea kusoma kuwa una mimba hata kama mimba imetoka mpaka baada ya wiki mbili kupita toka mimba imetoka hivyo usifikirie kufanya kipimo hiki au kipimo cha HCG kwenye damu. Kipimo cha kuangalia homon HCG kwenye damu ambacho huwa hakifanyiki wkenye maabara ndogo, kitaonyesha kuwa kiwango cha homon kwenye damu kinapungua kwa jinsi siku zinavyoenda, hii ni ishara ya kuwa mimba imetoka. Hata hivyo itachukua muda kufahamu kwa sababu mtaalamu lazima afanye kipimo zaidi ya kimoja ambavyo atafanya kwa utofauti wa wiki moja hadi tatu.
-
Dalili za mimba kutoka baada ya kutumia dawa ni zipi?Endao umetumia dawa za kutoa mimba, dalili za mimba kuwa imetoka kwa ujauzito ulio ndani ya miezi miwili ni; - Kupata maumivu makali ya tumbo yanayoambatana na kuumwa kwa kiuno. Maumivu hupungua lakini huendelea kwa wiki mbili za kwanza - Kutokwa na mabonge ya damu ikifuatiwa na kutokwa na damu ya kawaida kwa muda wa takribani wiki moja hadi mbili ( baadhi huendelea kutokwa na damu hadi kufikia hedhi inayofuata). Wasiliana na daktari endapo damu itaendelea kutoka - Kuwa na vipindi vya maumivu ya tumbo, na kutokwa na bonge la damu wiki kadhaa baada ya mimba kutoka
-
Kichomi kifuani husababishwa na nini?Hali na matatizo yafuatayo vinaweza kuwa visababishi vya kichomi kifuani; • Wasiwasi uliopitiliza na mshiko wa hofu • Matatizo ya kifua na upumuaji • Mgandamizo, kuteguka kwa misuli au maumivu ya mifupa ya kifua • Prikodio kachi Sindromu (SKS) • Kucheua tindikali Visabaishi vinavyohusiana na moyo pamoja na mishipa ya damu Anjaina Perikadaitiz Mayokadaitiz Kadiomayopathi Kuchanika kwa mshipa mkuu wa damu Shambulio la moyo Magonjwa mengine yasiyohuasiana na moyo; Mkanda wa jeshi Degedege la misuli ya kifua Mawe kwenye kibofu cha nyongo Michomo ya kongosho Madhaifu ya umezaji chakula Soma zaidi kuhusu kichomi kwenye makala zingine za kichomi ndani ya tovuti ya ULYCLINIC
-
Nini husababisha vichomi tumboni?Vichomi tumboni husababishwa na; Fuko maji kwenye ovari Gastroenteraitiz Kula sumu ya chakula Kutostahimili kwa laktosi Kuvimbiwa Maambukizi ya UTI Mawe kwenye kibofu nyongo Michomo kwenye kidole tumbo Sindromu ya iritabo bawel Ujauzito wa nje ya kizazi Vidonda vya tumbo Maambukizi ya virusi tumboni Maumivu ya hedhi Uchungu wa uongo Kusoma maelezo zaidi, ingia kwenye tovuti ya ULY CLINIC kwenye mada ya 'Vichomi tumboni'
-
Tatizo la kuziba kwa utumbo husababishwa na nini?Kujifunga kwa utumbo, hufahamika kwa lugha tiba kama 'intestinal obstruction' huweza kusababishwa na; Kufungamana kwa matumbo kutokana na makovu ya upasuaji Kujinyonga kwa utumbo Henia Saratani ya utumbo Matumizi ya dawa aina fulani Kusinyaa kwa tumbo kutokana na ugonjwa wa Crohn's au diverticulitis Kuzizwa na kinyesi kigumu
-
Homa ya njano ni nini?Homa ya manjano au homa ya njano ni ugonjwa unaosabababishwa na kirusi cha manjano. Unaweza pata maambukizi ya homa ya manjano endapo utang’atwa na mbu jike mwenye jina la anopheles aegypt na Haemogogus hasa kama unaishi Barani Afrika au umesafiri kwenda Amerika kusini. Baada ya kung’atwa na mbu mwenye kirusi, inakadiliwa kuchukua siku 3 hadi 6 kabla ya kupata dalili na baada ya dalili kutokea itachukua siku 3 hadi 4 ugonjwa kupotea.
-
Njano kwenye macho na ngozi husababishwa na nini?Visababishi vya kupata njano kwenye ngozi na macho Thalassemia Saratani ya kongosho Homa ya ini A, B na C, D na E Upungufu wa kimeng’enya cha glucose-6-phosphate dehydrogenase (G6PD) Ugonjwa wa ini kutokana na pombe Mawe kwenye kobofu nyongo Kusinyaa kwa ini Kuziba mirija ya kupitisha nyongo Ugonjwa wa seli mundu Saratani ya ini Pancriataitiz Kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu kutokana na magonjwa ya autoimmune Kuvunjwa kwa chembe nyekundu za damu kutokana na matumizi ya dawa Kuongezewa damu isiyona mwingiliano Homa ya njano Ugonjwa wa Weil’s Bofya kusoma zaidi maandishi yenye rangi ya bluu
-
Thalasimia ni nini?Thalasimia (thalassemia) ni ugonjwa wa damu wa kurithi unaosababisha uzalishaji wa kiwango kidogo kuliko kawaida cha himoglobin. Himoglobin hufanya kazi muhimu ya kubeba oksijeni kwenye damu na kupeleka kwenye seli ambapo huwa na kazi muhimuya kufanya ziweze kuishi na kutengeneza nguvu, mgonjwa mwenye upungufu wa himoglobin hupata dalili za kuchoka sana na kuishiwa pumzi ambazo ni dalili za upungufu wa damu. Soma zaidi kuhusu thalasimia kwa kubofya hapa
-
Inachukua muda gani dalili za gono kupotea baada ya matibabu?Kama una dalili za gono na ukapata matibabu sahihi, itachukua siku chache kupona na kupotea kwa dalili, hata hivyo inaweza kuchukua hadi wiki mbili endapo kulikuwa na dalili ya maumivu kwenye korodani au via vya ndani ya nyonga.
-
Inachukua muda gani kupona Kaswende baada ya kutumia dawa?Inaweza kuchukua muda wa wiki mbili hadi siku 28 kupotea kwa dalili za kaswende, hii inategemea na kaswende ina muda gani; Kaswende iliyodumu chini ya miaka miwili, hutibiwa na dawa za kuchoma kwenye kalio jamii ya penicillin kwa muda wa siku 10 hadi 14 na baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea Kaswende iliyodumu kwa muda zaidi ya miaka 2 hutibiwa kwa dawa za kuchoma kwenye kalio kila wiki kwa muda wa wiki tatu, au kunywa vidonge kwa muda wa siku 28. Baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea Kaswende ambayo ni ya hatari na imeathiri ubongo hutibiwa kwa kuchomwa sindano kila siku kwa muda wa wiki 2 au kunywa dawa za kumeza kwa muda wa siku 28. Baada ya muda huu utasemekana kuwa umepona kwani dalili zitapotea
-
Vyakula gani vina polyphenol kwa wingi?Vyakula vyenye kampaundi ya polyphenol kwa wingi ni; Matunda madogo ya rangi ya bluu (kama blueberi) Majani ya chai ya kijani Unga wa kokoa Wine nyekundu Zabibu nyekundu Mbegu za siha Mboga za majani Mafuta ya mzeituni Kahawa
-
Vyakula vyenye kampaundi ya carnosine kwa wingi ni vipi?Vyakula vyenye Amino asidi ya carnosine kwa wingi; Bata mzinga Kuku Nyama ya nguruwe Nyama ya ng’ombe
-
Vyakula vyenye kampaundi ya carnosine kwa kiasi kidogo ni vipi?Vyakula vyenye Amino asidi ya carnosine kwa kiasi kidogo ni; Mayai Maziwa Siagi ya ng’ombe
-
Kuna aina ngapi za rangi ya uchafu unaotoka ukeni?Kuna aina nyingi za rangi ya uchafu unaotoka ukeni ambazo ni; Ute mweupe kama maziwa Ute wa rangi ya maji Ute wa rangi nyekundu Ute wa rangi ya kijivu Ute wa rangi ya kijani Ute wa rangi ya bluu Ute wa rangi ya njano Kila rangi imeelezewa kisabaishi chake kwenye linki hii. Bofya hapa kwenda kwenye linki
-
Dawa ya jipu kwenye tundu la uke ni zipi?Dawa zinazotumika kutibu jipu tundu la uke au uvimbe wa batholini ni; • Trimethoprim-sulfamethoxazole • Amoxicillin-clavulanate • Clindamycin • Cefixime • Clindamycin Soma zaidi kuhusu uvimbe wa batholin/jipu kwenye mashavu ya uke na matibabu yake kwa kubofya hapa
bottom of page