top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Maumivu katika ya kifua

 

Maumivu katikati ya kifua mara nyingi hutokana na magonjwa ya ogani mbalimbali zilizo ndani ya kifua ya kifua na mara chache sababu zinaweza kuwa nje ya kifua au sehemu ya mbali na  kifua. Mara nyingi husababishwa na magonjwa ya moyo, mapafu na ukuta wa dayaframu. Baadhi ya sababu zinahitaji matibabu ya haraka zaidi kwani mtu anaweza poteza uhai endapo hata pata msaada.

 

Endapo unapata maumivu yafuatayo unahitaji kupata msaada wa haraka.

 

  • Maumivu ya kifua yanayokuwa makali zaidi na kuhisi kama kifua kinachanika kwenye maeneo ya titi

  • Maumivu ya kifua yanayosambaa kwenye taya, mkono wa kushoto au mgongoni

  • Maumivu yanayoambatana na Kupoteza fahamu, mapigo ya moyo kwenda kasi na kupummua harakaharaka

 

Visababishi

 

Visababishi vya maumivu katikati ya kifua

 

Huwa pamoja na;

 

  • Homa ya mapafu(nimonia)

  • Homa ya kifuko cha kongosho

  • Infaksheni ya mayokadiamu

  • Kolesistaitizi

  • Kubana kwa misuli ya kifua

  • Majeraha kwenye mbavu

  • Vidonda vya tumbo

  • Kucheua tindikali

  • Pumu ya kifua

  • Kostokondraitizi

  • Kusinyaa kwa mapafu

  • Magonjwa ya mijongeo ya misuli ya esofagasi

  • Kuchanika kwa mrija wa esofagasi

  • Henia ya hiatasi

  • Magonjwa ya mishipa ya moyo

  • Kuchanika kwa mshipa wa aotiki

  • Pankreataitizi

  • Shinikizo la damu katika mapafu

  • Anjaina

  • Mayokadaitizi

  • Mshituko wa moyo

  • Nimonia

  • Embolizimu ya palmonari

  • Perikadaitizi

  • Mshiko wa kupaniki

  • Magonjwa ya milango ya moyo

  • Kifua kikuu

  • Kuchanika kwa mshipa wa damu wa aota

 

 

Kumbuka kila kisababishi huja na dalili zake.kusoma zaidi bonyeza kwenye makala moja moja au tafuta kwenye kisanduku hapo juu kilichoandikwa “Tafuta chochote hapa”

​

​

Dalili

​

Dalili zinazoambatana na maumivu ya kifua huwa pamoja na;

​

  • Kifua kubana

  • Kifua kuwaka moto

  • Hisia za kuchanika kwa kifua

  • Kuzimia/kupoteza fahamu

  • Maumivu ya kifua yanayotokea wakati una njaa au unapokuwa unakula chakula

  • Kizunguzungu

  • Kuishiwa pumzi

  • Homa

  • Kutokwa na  jasho jingi

​

Matibabu

​

Matibabu ya maumivu ya kifua hutegemea kisababishi.Ongea na daktari wako ili kujua kisababishi kisha uanze matibabu.

​

​

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu zaidi na Tiba kwakubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.

​

Bonyeza kusoma makala zingine kuhusu; maumivu ya kifua yanayosababishwa na moyo, maumivu ya kifua kwa ujumla, kifua kubana na kuwaka moto

​

Imeboreshwa mara ya mwisho, 05.08.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. Chest pain. https://www.medicalnewstoday.com/articles/321650. Imechukuliwa 05.08.2020

  2. Mayo clinic. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/chest-pain/symptoms-causes/syc-20370838.  Imechukuliwa 05.08.2020

  3. http://www.heart.org/HEARTORG/Conditions/HighBloodPressure/AboutHighBloodPressure/What-is-Pulmonary-Hypertension_UCM_301792_Article.jsp#.WbEo3WeGNaQ. Imechukuliwa 05.08.2020

  4. Hollander JE, et al. Evaluation of the adult with chest pain in the emergency department. https://uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 05.08.2020

  5. Heart attack. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/heartattack/treatment. Imechukuliwa 05.08.2020

  6. Light RW. Primary spontaneous pneumothorax in adults. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 05.08.2020

​

bottom of page