top of page

Maumivu ya seli mundu- sickle cell

​

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

​

Utangulizi

​

Sickle cell ni mojawapo kati ya magonjwa mengi yanayofahamika Duniani, ugonjwa huu hurithiwa kati ya kizazi na kizazi. Maumivu kwa waathirika wa ugonjwa hutokea sana na wanahitaji matibabu, maumivu wanayopata ni makali kama ya kutafuna, kumungunya au ya kufukuta.  Maeneo yenye maumivu haya huwa mekundu, yanauma yakishikwa na ya moto.

 

Maumivu ya tatizo la seli mundu huwa hayajulikani mara nyingi ni lini yatatokea au kitu gani huyaamsha ila kuna baadhi ya vitu vimeonekana kusababisha maumivu, kuepuka kuamsha maumivu unatakiwa ujizuie na vitu vifuatavyo kama inawezekana;

 

  • Kuogelea kwenye maji ya baridi

  • Kutembea nnje kipindi cha baridi

  • Kupata joto sana kama kukaa maeneo yenye joto

  • Kupungukiwa maji mwilini kwa kutokunywa maji ya kutosha

  • Mafua na maambukizi ya magonjwa

  • Kunywa pombe au kuvuta sigara

  • Hedhi

  • Misongo ya mawazo

  • Kukaa karibu na mtu anayevuta sigara

 

Ni nini hatari ya uvutaji wa sigara katika kuamsha maumivu ya sickle cell?

 

Utafiti unaonyesha kwamba watoto wanaokaa karibu na watu au wazazi wanaovuta sigara, yaani kuvuta moshi wa sigara kutoka kwa mtu anayevuta sigara hupata maumivu mara nyingi zaidi (mara mbili zaidi) kuliko wale ambao hawapo karibu na moshi wa sigara. Maumivu yao huwa makali sana na husababisha mtoto kupelekwa hospitali. Utafiti mmoja umeonyeha kwamba kuwepo mazingira au kuvuta moshi wa mtu anayevuta huongeza kujirudia kupata maumivu kwa watoto hawa kwa asilimia 90, hivyo ni vema kuacha kuvuta au kuwa mbali na watoto hawa unapokuwa unavuta sigara au tumbaku.

 

Dalili zifuatazo zikitokea kwa mtoto aliye chini ya miaka miwili, anamaumivu na homa basi mpeleke haraka  hospitali

 

  • Maumivu yasiyoisha kwa dawa anazotumia nyumbani

  • Maumivu makali ya tumbo au tumbbo kuvimba

  • Maumivu ya kifua

  • Kupata matatizo ya ghafla kwenye macho

  • Kichwa kuuma tofauti na kawaida

  • Kuhisi mchovu sana

  • Homa/joto zaidi ya degree celsium 38(siku zote mpime mtoto kama anaonekana ana homa)

  • Kutapika

  • Matatizo ya kifua au mapafu kama maumivu au kupumua kwa shida

  • Kushindwa kutembea au kupooza

  • Kupata ganzi ghafla

  • Kuchoka ghafla

  • Kuvimba maungio hasa gotini au mikononi

  • Kusimamisha uume ukiambatana na maumivu na bila kusinyaa

 

Toleo la 3

Imeboreshwa

January 6, 2015

1/7/2019

bottom of page