top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Maumivu ya jino

​

Maumivu ya jino au michomo kutokana na shambulio la kinga za mwili husababishwa mara nyingi  na maambukizi kinywani. Hata hivyo maumivu ya jino yanaweza kusababishwa na tatizo lisilo la moja Kwa moja kutoka kwenye jino bali ikawa ishara ya kwamba sehemu nyingine ya mwili haipo Sawa. 

​

Visababishi vikubwa vya Meno kuuma huwa pamoja na;

​

  • Kuoza Kwa meno

  • Kujing'ata

  • Kung'ata kitu kigumu

  • Kukaa kwa vitu vigumu katikati ya meno

  • Kwa watoto maumivu ya meno ni dalili ya kawaida kama sehemu ya ukuaji wao

  • Mashimo kwenye Jino

  • Kuharibiwa Kwa jino lililozibwa

  • Kuota au kung'oa Kwa jino

  • Majeraha ya Meno

  • Kutingishika Kwa jino

  • Kuvunjika Kwa jino

  • Maambukizi kwenye uwazi ndani ya fizi

​

Dalili

  • Maumivu Makali, ya kuchoma au yanayoonekana wakati wote au uking'ata au kutafuna chakula

  • Kuvimba Kwa maeneo jirani na Meno au fizi

  • Maumivu ya kichwa

  • Homa

  • Kinywa kutoa harufu mbaya

​

Endapo Una dalili zifuatazo mpigie daktari wako mara moja Kupata Tiba;

​

  • Maumivu ya jino yaliyo endelevu yaani zaidi ya siku tatu

  • Maumivu ya Jino pamoja na dalili za

    • homa, kuvimba Jino, maumivu ukiwa unatafuna chakula, kutoka harufu mbaya mdomoni au fizi kubadilika rangi

 

Nini husababisha Jino kuoza?

​

Jino kuoza husababishwa na kuharibiwa kwa jino na tindikali inayozalishwa na bakteria walio kwenye kinywa. Bakteria hawa hi walinzi wa kinywa, lakini huishi Kwa kutegemea sukari. Bakteria mara wanapotumia sukari huzalisha tindikali inayounguza Meno na kufanya yaoze na kutengeneza mashimo.

 

Dalili ya Kwanza ya Meno kuoza inaweza kuwa ni maumivu ya Meno ukila vitu vitamu, cha baridi Sana au cha moto.

​

Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya jino;

​

ULY Clinic inakushauri siku zote usichukue hatua yoyote ile inayoathiri afya yako bila kuwasiliana na daktari wako. 

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kutumia namba za simu chini ya tovuti hii kwa elimu suhauri na Tiba

​

Imeboreshwa 11.2.2020

​

Rejea za mada hii;

​​

  1. Toothache. https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/10957-toothache. Imechukuliwa 10.02.2020

  2. Toothache. kidsclinic.http://kidsclinic.pediatricweb.com/Is-Your-Child-Sick/Is-Your-Child-Sick/Toothache. Imechukuliwa 10.02.2020

  3. MOuth health. https://www.mouthhealthy.org/en/az-topics/a/abscess. Imechukuliwa 10.02.2020

  4. Cambrige clinic. https://www.cambridgedentalhub.co.uk/cambridge-toothache-clinic/. Imechukuliwa 10.02.2020

bottom of page