Imeandikwa na daktari wa ULY clinic
​
Namna ya kujieleza kuhusu maumivu ya kichwa
​
Umekuwa ukisumbuliwa na maumivu ya kichwa? Maumivu ya kichwa yanaweza kusababishwa na hali au magonjwa mbalimbali kama yanavyofahamika katika mada zilizoandikwa kwenye website hii(bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu maumivu ya kichwa). Kwa sababu hii mtu anapokuwa anachukuliwa historia ya maumivu ya kichwa kuna mambo muhimu yanatakiwa kuulizwa au kuelezewa vema ili kujua kisababishi halisi. Si kwamba unasoma maelezo haya ili uwe daktari wa wengine bali unasoma ili uweze kumpa maelezo mazuri daktari kujua chanzo, sababu na kisababishi cha maumivu yako ya kichwa
​
Kwenye historia ambayo utakuwa unampa daktari unabidi ufuate maelekezo haya yafuatayo;
​
Maumivu yana siku ngapi?
​
-
(idadi ya siku za maumivu ya kichwa hutumika kuelezea sababu za maumivu, maumivu ya muda mfupi makali humaanisha kunashida inayoendelea kwa haraka ndnai ya kichwa mfano mgandamizo ndani au nje ya kichwa au kuvilia kwa damu ndani ya kichwa n.k)
​
Maumivu yapo sehemu gani ya kichwa (mbele ya kichwa au paji la uso, kisogoni, pembeni ya kichwa upande wa kushoto au kulia)?
​
Maumivu yalianzaje?
​
-
Maumivu yanaweza kuanza kwa namana tofauti na kuendelea kubadilika kwa makali au kupungua jinsi muda unavyoenda
-
Mfano maumivu yanaanza taratibu na kuongeze makali jinsi siku zinavyoenda
​
Sifa au Aina gani ya maumivu?
​
Maumivu yanaweza kuwa
​
-
Maumivu kama yale ya kugonga na nyundo
-
Maumivu ya kupwita pwita(kutokana na kudunda kwa mishipa ya damu)
-
Maumivu ya kuungua kama moto
​
Maumivu yanahamia sehemu yoyote ile ya mwili?
​
Maumivu yanaweza kuanza sehemu moja ya mwili kisha kuhamia sehemu nyingine ya mwili, mfano
-
Maumivu yanayoanzia upande mmoja wa kichwa kisha kusambaa kichwa chote
-
Maumivu yaliyo sehemu zote za kichwa(yasiyo sehemu maalumu)
​
Mara ngapi hutokea?
​
Maumivu ya kichwa yakitokea mara nyingi huweza kudhuru ubora wa maisha ya mtu, hii ni kwa sababu mtu huyu atakuwa anaumwa mara kwa mara.
​
Maumivu yanaweza kuwa yanatokea mara kadhaa katika siku au katika wiki
​
Mfano maumivu ya kipanda uso (migraine) hutokea miezi maalumu katika kila mwaka, mfano kila mwezi wa sita wa mwaka au mwezi wa 2 wa mwaka. Maumivu yanapotokea hudumu kwa muda wa dakika kadhaa na kuondoka( mfano nusu saa kisha kuondoka)
​
Viamsha maumivu
​
Viamsha maumivu ni mambo au vitu vinavyofanya maumivu kuwa makali zaidi au kuanza kwa maumivu. Mambo mbalimbali yanayoweza kuanzisha maumivu ya kichwa huwa pamoja na;
​
-
Mwanga wa jua
-
Kusoma kurasa nyeupe
-
Kelele za masauti
-
Mawazo au msongo wa mawazo
-
Kutopumzika au kulala vizuri
-
Kupigwa kichwani
-
Kazi/shughuli za kutingisha kichwa na ubongokusiko kawaida
​
Vituliza maumivu
​
Ni vitu au mambo mtu yanayopunguza maumivu, huweza kuwa;
​
-
Kukaa sehemu tulivu
-
Kukaa sehemu yenye giza
-
Kuacha kusoma au kutumia miwani
-
Kunywa dawa aina fulani
Vitu/mambo ambatwa
​
Maumivu ya kichwa yanaweza kuambatana na mambo mbalimbali, mambo haya yanaweza kumaanisha hali ya hatari na inayotisia maisha au kuwa ishara nzuri ya kuchukua ili kuzuia madhara. Mfano
​
-
Kuzimia/kupoteza fahamu
-
Kizunguzungu
-
Makelele masikioni
-
Kuongezeka kwa shinikizo la damu
-
Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
-
Kupanda kwa joto la mwili au homa
-
Maumivu ya shingo au mgongo
Namna ya kujielezea kuhusu maumivu ya tumbo
​
Sehemu yalipo(tumbo la chini au tumbo la juu)
​
Yana siku ngapi
​
Yanahamia sehemu yoyote ya tumbo au mwili
Yanaambatana na dalili zozote zile?
-
Mf Kuharisha, kutopata haja kubwa au haja kubwa kuwa ngumu, damu kwenye haja kubwa,
-
yana
​
​
Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu mada ya maumivu ya kichwa na visababishi vyake
​
ULY clinic inakushauri siku zote ufanye mawasiliano na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili zilizosemwa kwenye makala hii.
​
​
Imeboreshwa, 26.06.2020
​
​
Rejea za mada hii
​
-
Flu symptoms & severity. Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/flu/about/disease/symptoms.htm. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Cutrer FM, et al. Cough, exercise, and sex headaches. Neurologic Clinics. 2014:32:433.
-
Bajwa ZH, et al. Evaluation of headache in adults. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Evans RW, et al. Postconcussion syndrome. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Green MW. Secondary headaches. In: Continuum Lifelong Learning Neurology. 2012;18:783.
-
Simon RA. Allergic and asthmatic reactions to food additives. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.06.2020
-
NINDS stroke information page. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. http://www.ninds.nih.gov/disorders/stroke/stroke.htm. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Cutrer FM. Primary cough headache. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Garza I, et al. Overview of chronic daily headache. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 26.05.2020
-
Friedman BW, et al. Headache emergencies: Diagnosis and management. Neurological Clinics. 2012;30:43.
-
Headache hygiene tips. American Headache Society Committee for Headache Education. http://www.achenet.org/resources/trigger_avoidance_information /. Imechukuliwa 26.06.2020
-
External compression headache. International Headache Society. http://ihs-classification.org/en/02_klassifikation/04_teil3/13.10.00_facialpain.html. Imechukuliwa 26.06.2020
-
The elusive hangover cure. British Columbia Drug and Poison Information Centre. http://dpic.org/article/professional/elusive-hangover-cure. Imechukuliwa 26.06.2020
-
Headache: Hope through research. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. http://www.ninds.nih.gov/disorders/headache/detail_headache.htm#142883138. Imechukuliwa 26.06.2020
-
When to see a physician for your headache. National Headache Foundation. http://www.headaches.org/when-to-see-a-physician-for-your-headache/. Imechukuliwa 26.06.2020