top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

 

 

Maumivu ya kifua kutokana na magonjwa ya moyo.

 

Kuna matatizo mbalimbali ya moyo yanayoweza kusababisha maumivu ya kifua , ambayo  ni shambulio la ghafla la moyo(mshiko wa moyo), kufa kwa chembe hai za moyo na kuziba kwa mishipa inayolisha moyo.

 

Dalili

 

  • Maumivu makali ya kifua huwa ya kufululiza bila kuacha kwa muda wa dakika 30  au zaidi, maumivu yanaweza kuwa ya kubana,kugandamiza au kuchoma maumivu haya husambaa kuelekea kwenye shingo, mkono na bega la kushoto

​

Dalili zingine ni hali ya

  • Kuchoka

  • Kichwa kuuma ,

  • Kukohoa,

  • Kichefuchefu na

  • Kutapika.

​

Visabbishi

 

Kuna  mambo au tabia ambazo zinaweza sababisha matatizo ya moyo, nayo ni

 

Vipimo na Ugunduzi wa tatizo

 

Tatizo linaweza gundulika kwa dalili kwa asilimia kubwa na kufanya vipimo

Vipimo hivi huwa na lengo la kutazama utendaji kazi wa moyo na tabia au ukubwa wa moyo

  • Vipimo hivyo ni kama kipimo kinachoangalia tabia ya mawimbi umeme ya moyo - ECG

  • Picha ya mionzi ya X ray ya kifua

  • Na ultrasound ya moyo-Echocardiogram.

 

Vizuizi vya tatizo:

  • Tatizo la moyo linaweza kupungua kwa kuboresha maisha yako, inashauriwa kuacha kuvuta sigara, pia fanya maozezi ya mwili, kula mlo kamili na kupunguza kula vyakula vyenye mafuta mengi ya wanyama.

 

Madhara

 

Matatizo ya moyo hasa shambulio la moyo huweza sababisha seli za moyo kufa hivyo kuleta madhara yafuatayo;

​

Soma zaidi sababu zingine zinazoweza kusababisha maumivu ya kifua kwa kubonyeza hapa

​

au

​

Bonyeza kusoma makala zingine kuhusu; maumivu ya katikati ya kifua, maumivu ya kifua kwa ujumla, kifua kubana na kuwaka moto

​

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa uchunguzi zaidi na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile inayodhuru afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa elimu na ushauri zaidi kwa kubonyeza hapa"Pata Tiba" au kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti yetu

Rejea za mada hii

​

  1. Maswali na majibu kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC

  2. ULY CLINIC. MAumivu ya kifua. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Maumivu-ya-kifua%2C-kifua-kubana%2C-kifua-kuwa-kizito. Imechukuliwa 19.06.2020

​

bottom of page