Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
7 Aprili 2025, 17:25:21

Maumivu ya pumbu
Maumivu ya korodani (pumbu) ni maumivu yanayoweza kutokea kwenye korodani moja au zote mbili, maumivu hayo chanzo chake kinaweza kuwa ni kwenye korodani, au sehemu nyingine mwilini. Maumivu ya pumbu yanaweza kusababishwa na maambukizi, majeraha, au matatizo ya kiafya kama vile uvimbe wa mshipa wa pumbu. Uchunguzi wa haraka na matibabu sahihi ni muhimu ili kuepuka madhara ya muda mrefu. Makala hii imeeleza kuhusu visababishi, dalili za tahadhari, na mambo ya kufanya unapokuwa na maumivu ya pumbu (korodani)
Visababishi vya maumivu ya pumbu
Kuna hali na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababisha maumivu ya korodani, majeraha madogo pia yanaweza kuambatana na aumivu makali kutokana na korodani kuwa na mishipa mingi ya fahamu inayoongeza hisia za maumivu. Visabaishi vinavyoweza kupelekea maumivu ya pumbu, endapo itabinywa au kijibana ni pamoja na;
1. Maambukizi kwenye korodani
Hutokana na bakteria au virusi.
Mara nyingi huambatana na kuvimba, joto kwenye pumbu, au maumivu ya tumbo la chini.
Wakati mwingine huambatana na homa au maumivu ya wakati wa kukojoa.
2. Kuvimba kwa mrija wa mbegu(Kutokana na michomokinga)
Huchanganya na maambukizi ya njia ya mkojo au magonjwa ya zinaa kama kisonono (gono) au klamidia
Maumivu huwa makali zaidi upande mmoja.
3. Kujisokota kwa pumbu
Ni hali ya dharura ambapo pumbu huzunguka na kukata mzunguko wa damu.
Huambatana na maumivu makali ghafla, pumbu kuvimba na kutoonekana sawa kwa ukubwa.
Inahitaji matibabu ya haraka sana – ndani ya masaa 6–8 ili pumbu isiharibike.
4. Majeraha kwenye pumbu
Pumbu inaweza kuumia kutokana na kujigonga, kuvaa nguo za kubana sana, au kufanya kazi nzito.
Hii mara nyingi husababisha maumivu unapogusa au kubinya.
5. Uvimbe wa mishipa ya vena
Ni kuvimba kwa mishipa ya damu kwenye pumbu
Hutoa hisia ya uzito au kuvuta kwenye pumbu, mara nyingi upande wa kushoto.
Huweza kuonekana mishipa kama nyuzi au "mfuko wa minyoo".
6. Ngiri kwenye kinena
Wakati sehemu ya utumbo inaingia kwenye mfuko wa pumbu kupitia njia dhaifu tumboni.
Maumivu yanaweza kuongezeka unapoinama au kubeba vitu vizito.
Visababishi vingine vya maumivu ya pumbu
Visababishi vingine ni pamoja na;
Dayabetiki nyuropathi(kwa wagonjwa wa kisukari)
Haidrosili(busha)
Maumivu yasiyofahamika kisababishi
Mawe kwenye figo
Ugonjwa wa mumps
Maambukizi kwenye tezi dume
Uvimbe kwenye pumbu
Spematosili
Maambukizi ya UTI
Dalili za tahadhari unapaswa kuchukulia kwa uzito
Ikiwa una mojawapo ya dalili hizi, ni muhimu uende hospitali haraka, hasa kupima ultrasound ya pumbu.
Maumivu makali ya ghafla.
Pumbu kuvimba au kuwa na joto kupita kiasi.
Kichefuchefu au kutapika pamoja na maumivu.
Pumbu kuonekana kubadilika ukubwa ghafla.
Homa au maumivu ya mkojo.
Vipimo vya maumivu ya pumbu
Vipimo hufaanyika ili kuthibitisha tatizo ambalo daktari atakuwa ameliona, wakati mwingine si lazima vipimo kufanyika kwa sababu kuna matatizo ambayo daktari atayatambua kutoka kwenye uchunguzi wa awali wa mwili na historia ya tatizo lako. Baadhi ya vipimo ambavyo unaweza fanyiwa ni;
Urinalysis na culture kwa wagonjwa wote
Kipimo cha magonjwa ya zinaa( endapo unatokwana usaha, au kuwa positive kwenye kipimo cha urinalysis au kuwa na maumivu wakati wa kukojoa)
Ultrasound ili kujiridhisha kwamba pumbu hazijajisokota kama kuna utata
Vipimo vingine vinavyotokana na visababishi alivyoona daktari
Kumbuka endapo vipimo vimekuja vya kawaida, chanzo cha maumivu kinaweza kuwa sehemu nyingine ya mwili.
Matibabu ya maumivu ya pumbu
Matibabu huelekezwakwenyekisababishi alichokitambua daktari wako, huweza kuwa matibabu ya dharura kama upasuaji kama shida ni kujisokota kwa pumbu au kupata mapumziko kitandani. Dawa za maumivu kama morphine na dawa zingine jamii ya opioid hutumika kupunguza maumivu ya ghafla na makali. Dawa za antibayotiki pia hushauriwa endapo kisababishi ni epididimaitizi au ochaitizi inayosababishwa na bakteria.
Unapaswa kufanya nini unapopata maumivu ya pumbu?
Usichelewe kumuona daktari wa mfumo wa mkojo au daktari wa upasuaji kwa uchunguzi zaidi.
Epuka kubinya au kugusa mara kwa mara, kwani kunaweza kuleta maumivu zaidi au kuathiri hali ya ndani.
Vaa nguo za ndani zinazobana vizuri lakini si kwa kukandamiza sana, kusaidia pumbu kutulia.
Usitumie dawa bila ushauri wa daktari – hasa antibiotiki au dawa za maumivu.
Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya pumbu
Maumivu ya pumbu si ya kuyabeza, unapaswa kuonana na daktari haraka, wakati unaenda kuonana na daktari unaweza kufanya mambo yafuatayo kusaidia kupunguza hali ya maumivu;
Kunywa dawa za kupunguza maumivukama vile aspirini, ibuprofen au parasetamo isipokuwa kama daktari wako amekupa maelekezo mengine. Aspirini haitakiwi kutumika kwa watoto chini ya umri wamiaka mitatu, watoto wanaopona kutoka kwenye homa ya tetekuwanga aumafua hawatakiwi kutumia dawa hii.
Tumia kitu chochote kuifanya korodani iwe juu wakati unalala chini
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Aprili 2025, 17:25:21
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Baird DC, Meyers P, Hu JS. Testicular torsion: diagnosis, evaluation, and management. Am Fam Physician. 2019;100(10):610–615.
2. Sharp VJ, Kieran K, Arlen AM. Testicular torsion: diagnosis, evaluation, and management. Curr Urol Rep. 2013;14(4):366–373. doi:10.1007/s11934-013-0345-0
3. Trojian TH, Lishnak TS, Heiman D. Epididymitis and orchitis: an overview. Am Fam Physician. 2009;79(7):583–587.
4. Woodward PJ, Schwab CM, Sesterhenn IA. From the archives of the AFIP: Extratesticular scrotal masses: radiologic-pathologic correlation. Radiographics. 2003;23(1):215–240. doi:10.1148/rg.231025097
5. Campbell-Walsh Urology. 12th ed. Wein AJ, Kavoussi LR, Partin AW, Peters CA, editors. Philadelphia: Elsevier; 2020.
6. American Urological Association (AUA). Evaluation of scrotal pain and swelling in adults. [Internet]. 2020 [cited 2025 Apr 7]. Available from: https://www.auanet.org/
7. World Health Organization. WHO Manual for the Standardized Investigation, Diagnosis and Management of the Infertile Male. Geneva: WHO; 2000.
8. Skoog SJ, Roberts KP, Goldstein M, et al. AUA guideline on evaluation and management of acute scrotum. J Urol. 2015;193(6):e294–e295.
8. Dubin L, Amelar RD. Etiologic factors in 1294 consecutive cases of male infertility. Fertil Steril. 1971;22(8):469–474.
9. Lewis AG, Bukosky J, Jordan GH. Varicocele: current concepts and treatment. Curr Urol Rep. 2014;15(5):408. doi:10.1007/s11934-014-0408-y
10. Eyre RC. Evaluation of acute scrotal pain in adults. https://www.uptodate.com/contents/acute-scrotal-pain-in-adults. Imechukuliwa 27.06.2020
11. PUBMED. Scrotal pain. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/6726967/. Imechukuliwa 27.06.2020
12. Scrotal pain. Uptodate. https://www.uptodate.com/contents/causes-of-painless-scrotal-swelling-in-children-and-adolescents. Imechukuliwa 27.06.2020
13. Scrotal pain. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/symptoms-of-genitourinary-disorders/scrotal-pain. Imechukuliwa 27.06.2020