top of page

Maumivu ya tumbo

​

Imeandikwa na ULY-Clinic

​

Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo kadha wa kadha, visababishi kama gesi kujaa tumboni, ama mijongeo ya misuli ya tumbo huwa havina madhara sana. Visababishi mbali na hivyo huhitaji matibabu yafanyike kwa haraka.

 

Mara nyingi, sehemu maumivu yalipo yanaweza kuelezea kisababishi cha maumivu hayo. Wakati mwingine, maumivu ya tumbo yanaweza kutokea katika namna ya kutoeleweka na kutofahamika sababu inayosabisha maumivu hayo. Hata hivyo ni jambo la msingi kujua sababu ya maumivu ya tumbo kutokana na mahali maumivu hayo yalipo katika tumbo lako.

​​

Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na mijongeo ya misuli ya tumbo huwa ya muda mfupi na huwa si ya hatari sana.

​

Maumivu makali ya tumbo humaanisha kuna hali au ugonjwa wa kutiliwa umaanani sana, maumivu hayo yakianza ghafla na bila kutarajiwa hutakiwa kutibiwa kwa dharura haswa endapo maumivu hayo yamejikita sehemu moja ya tumbo au matumbo.

 

Endapo unapata maumivu hayo makali, piga namba za simu kwa matibabu ya harakakutoka kwa daktari au mamlaka zilizo karibu na wewe au wasiliana na daktari wako kwa ushauri wa haraka wakati unafanya mpango wa kufika hospitali

 

Sifa za maumivu ya tumbo

​

Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa yenye sifa kadhaa kama vile;

​

  • Maumivu ya kuungua na moto

  • Kunyonga

  • Kukata

  • Kung’ata

  • Maumivu makali sana

  • Maumivu ya kuchoma na kitu

  • Maumivu sugu

  • Maumivu yanayoongezeka jinsi muda unavyokwenda

  • Maumivu ya kuja na kuondoka

 

Licha ya kuwa na sifa tofauti maumivu ya tumbo yanaweza pia kuwa sehemu mbalimbali za mwili, maumivu katika sehemu hizi mbalimbali huashiria kuna shida katika sehemu hiyo. Maeneo ambayo maumivu ya tumbo yanaweza kutokea ni;

​

  • Maumivu yanayoanzia tumboni na kuhamia sehemu nyingine za mwili

  • Maumivu ya chini ya kitovu

  • Maumivu ya katikati ya tumbo

  • Maumivu upande mmoja wa tumbo

  • Maumivu juu ya kitovu

​

Licha ya kuwa katika sehemu fulani ya mwili, maumivu ya tumbo pia yanaweza kuamshwa na;

​

  • Kukohoa au kutembea

  • Kunywa pombe

  • Kula vyakula aina Fulani

  • Msongo wa mawazo

  • Hedhi

​

Kwa baadhi ya watu maumivu ya tumbo huweza kufisha au kuamsha na vitu au mambo kadhaa ambayo ni vema kufahamu ili uweze kumwambia daktari wako na kumsaidia kujua shida ni nini, vitu hivyo ni;

​

  • Kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali kama omeprazole, lansoprazole

  • Kuacha kula vyakula aina fulani

  • Kubadili pozi la mwili

  • Kula vyakula aina fulani

  • Kula mboga za majani kwa wingi

 

Kuna hali au mambo mbalimbali yanayoweza kuambatana na maumivu ya tumbo, ni muhimu pia kuyafahamu na kumwambia daktari wako, daktari wako pia atakuuliza pia mambo hayo ili kukua tatizo lako haswa ni nini, mambo hayo ni;

​

  • Kuvimba kwa tumbo

  • Kupata choo cheusi au chenye damu

  • Haja ngumu

  • Kuharisha

  • Homa

  • Kushindwa kutoa haja kubwa licha ya kuwa na hamu ya kujisaidia

  • Kupata Choo kilaini chenye majimaji

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Kijambo chenye arufu  mbaya

  • Kuhisi mdundo wa mishipa ya damu karibia na kitovu

  • Harara kwenye ngozi

  • Matumbo kupiga kelele

  • Kupoteza uzito bila sababu

  • Uhiaji wa kwenda haja kubwa mara moja

 

Visababishi

 

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo kama ilivyoelezewa kutokana na sifa za maumivu hayo ya tumbo na sehemu/mahali yalipo au ni nini kichachoyafanya yapoe au kuwa makali Zaidi.

​

Baadhi ya visababishi vimeorodheshwa hapa chini, kumbuka mada hii itaendelea kuongezwa visababishi vingine ambavyo havijaorodheshwa hapa.

 

Maumivu ya ghafla ya kunyonga yanayoambatana na kuharisha

 

Endapo maumivu yameanza hivi karibuni na yanaambatana na kuharisha, kisababishi kinaweza kuwa maambukizi kwenye mfumo wa tumbo kwa jina tiba gastroenteritis. Maambukizi haya yanaweza kuwa ya bakteria au virusi kwenye matumbo au tumbo, kumbuka maumivu haya yatapona bila matibabu ndani ya siku chache

 

Ugonjwa wa gastroenteritis unaweza kusababishwa na kula chakula chenye sumu au kula chakula kilichochanganyika na kinyesi cha mtu mwenye tatizo hilo. Chakula hiki kinaweza kuwa kimeandaliwa na mtu mwenye tatizo hili au kutumia maji yaliyochanganyika na kinyesi cha mtu mwenye tatizo.

​

Kama unapata maumivu mara kwa mara na kuharisha, unawez akuwa na tatizo la muda mrefu la sindromu ya Iritabo baweli

 

Maumivu makali na ya ghafla

 

Kumbuka endapo una maumivu aina hii wasiliana na daktari wako kwa huduma ya kwanza haraka iwezekanavyo.

​​

Kama una maumivu makali sana na ya ghafla, ni dhahiri unaweza kuwa kuna sababu ya hatari inayohitaji matibabu ya haraka. Maumivu hayo yanaweza kusababishwa na;

​

  • Appendicitis– hili ni tatizo la kuvimba kwa kidole tumbo kutokana na maambukizi. Husababisha maumivu chini ya kitovu upande wa kulia. Endapo shida ipo kwenye kidole tumbo inamaanisha kinatakiwa kutolewa kwa upasuaji.

  • Kutoboka kwa tumbo- kama kuna kidonda ndani ya tumbo au ulikuwa na vidonda vya tumbo, vinaweza kutoboka na kusababisha damu kuvilia ndani ya utumbo. Hii inaweza kuleta maumivu makali sana ya tumbo yasiyoweza kupoa kirahisi na huweza kuambatana na kuvimba kwa tumbo na kutokwa jasho jingi au kuzimia, kutokwa na kinyesi cheusi kabla dalili hii kutokea.

  • Acute cholecystitis- hii husababishwa na michomo kwenye kifuko cha nyongo inaotokana na kufanyika kwa mawe ndani ya kifuko hiko. Utatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kifuko hiki

  • Mawe kwenye figo- kufanyika kwa mawe ndani ya figo au katika mirija ya figo huweza kuziba njia ya mkojo, utatakiwa kufika hospitali mara moja ili njia hizo zizibuliwe kuepuka uharibifu wa mirija ya mkojo na figo

  • Daiverticulitis- hutokana na michomo kwenye vifuko vilivyo kwenye utumbo mpana, michomo hii hutokea kwa sababu ya maambukizi kwenye vifuko hivi. Utahitaji kupatiwa tiba dawa.

  • Maumivu ya tumbo baadhi ya nyakati yanaweza kusababishwa na sababu ambazo zinatibika kama vile maambukizi au sababu ambazo zinaisha zenyewe kama kujongea kwa misuli

 

Maumivu ya tumbo ya muda mrefu au ya kujirudia

 

Maumivu ya tumbo ya muda mrefu na ya kujirudia mara nyingi huwa si ya hatari sana, onana na daktari ili kujua kisababishi ni nini na kupata tiba.

 

Baadhi ya visababishi ni

 

  • Sindromu ya inflamatory bawel- ugonjwa huu huambatana kunyonga kwa tumbo, kuharisha au haja ngumu. Maumivu yanapoa baad aya kujisaidia

  • Ugojnwa wa inflamatori baweli huhusisha magonjwa mawili ambayo ni ugonjwa wa Crohn's na  asaletivu kolaitizi, hata hivyo ugonjwa wa endometriosisi pia huweza kusababisha aina hii ya maumivu

  • Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo(UTI)- maumivu haya huwez akujirudia rudia kw abaadhi ya watu, utapata dalili zifuatazo pia, kuungua wakati w akukojoa, kuwa au kutokuwa na homa, kichefuchefu, kutapika.

  • Haja ngumu- huweza kutokea na kusababisha maumivu ya tumbo, huambatana na mabadiliko ya hedhi pia

 

Matatizo mengine ya tumbo

  • Vidonda vya tumbo

  • Kiungulia

  • Kucheua tindikali na

  • Ugonjwa wa gastraitizi

 

Maumivu ya tumbo kwa watoto yanaweza kusababishwa na;

 

  • Haja ngumu

  • UTI

  • Kiungulia na Kucheua tindikali

  • Kipand auso cha tumbo

​

Soma zaidi kuhusu  maumivu ya tumbo kwa mwanamke, bonyeza hapa

​

ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya.
​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri kupitia namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa, 26.06.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. American College of Emergency Physicians. https://www.acep.org. Imechukuliwa 26.06.2020

  2. U.S. Food and Drug Administration. http://www.fda.gov. Imechukuliwa 26.06.2020

  3. American Academy of Orthopaedic Surgeons. https://orthoinfo.aaos.org. Imechukuliwa 26.06.2020

  4. Walls RM, et al., eds. Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 9th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  5. UpToDate. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 26.06.2020

  6. Feldman M, et al. Sleisenger and Fordtran's Gastrointestinal and Liver Disease: Pathophysiology, Diagnosis, Management. 10th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  7. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional. Imechukuliwa 26.06.2020

  8. Kliegman RM, et al. Nelson Textbook of Pediatrics. 20th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  9. Zitelli BJ, et al., eds. Zitelli and Davis' Atlas of Pediatric Physical Diagnosis. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  10. Ferri FF. Ferri's Clinical Advisor 2018. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  11. Petty RE, et al., eds. Textbook of Pediatric Rheumatology. 7th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  12. Elsevier Point of Care. https://www.clinicalkey.com.  Imechukuliwa 26.06.2020

  13. Kasper DL, et al., eds. Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  14. Wein AJ, et al., eds. Campbell-Walsh Urology. 11th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 26.06.2020

  15. Stomach ache and abdmonial pain. NHS. https://www.nhsinform.scot/illnesses-and-conditions/stomach-liver-and-gastrointestinal-tract/stomach-ache-and-abdominal-pain. Imechukuliwa 26.06.2020

maumivu-ya-tumbo-ulyclinic
bottom of page