Mwandishi:
ULY CLINIC
3 Juni 2020, 12:54:05
Kuandaa nyonga kabla ya kujifungua
Wakati wa kujifungua unapokaribia, mtoto atashuka chini ya tumbo kuelekea kwenye shimo la nyonga katika pozi la kichwa chini matako juu. Jukumu lako kubwa ni kujiweka fiti kimwili ili kumwezesha mtoto apite kirahisi kwenye nyonga na tundu la uzazi.
Baadhi ya tamaduni huwafundisha wanawake mabinti toka wakiwa wadogo kukaa kwa kukunja miguu kama inavyoonekana kwenye picha namba moja. Aina hii ya kukaa inafanya misuli na ligamenti za nyonga kuwa fupi, hivyo kuna mahitaji ya kuiongeza urefu kwa mazoezi. Kama unaona aibu kukaa huku miguu imeachana, utanza kujhisi vema tu kukaa hivyo baada ya kuanza mazoezi haya.
Faida za kuandaa nyonga kabla ya kujifungua ni zipi?
Mazoezi yaliyoandikwa hapa chini yatakusaidia kuandaa vema njia ya mtoto kupita na hivyo kukusababishia ujifungue kirahisi kwa njia ya kawaida. Hakikisha unafanya mazoezi haya mara kwa mara.
Zoezi la kwanza la kuimarisha sakafu ya nyonga
Tazama picha namba 3
Fanya mazoezi haya na hakikisha unafanya katika pozi ambalo halikupi maumivu.
Fanya zoezi taraibu na usijilazimishe, unaposhika magoti juu kama kwenye picha namba 3 kulia, hakikisha huliachii kwa muda wa wa kuhesabu 1,2,3,4,5 labla ya kuachia taratibu chini.
Ili kulegeza misuli ya kinena, nyonga na misuli ya ndani ya kati ya mapaja kaa pozi kama kwenye picha namba 2 huku umeshika kiwiko cha mguu huku ukisogeza nyonga karibu na makanyagio.
Zoezi la pili la kuimarisha sakafu ya nyonga kwa ajili ya kijifungua salama
Kufanya zoezi katika picha namba 4 b;
Kaa pozi kwenye mkeka wa kufanyia mazoezi
Hakikisha hauumii kwenye makalio
Panua miguu yako kama kwenye picha inavyoonekana
Rudia kwa kutanua na kukutanisha miguu kama kwenye picha namba 4a
Rudia mara nyingi unavyoweza na unavyotaka
Zoezi namba tatu la kuimarisha sakafu ya nyonga kabla ya kujifungua
Kufanya zoezi namba 4a
Hakikisha upo sehemu salama
Unaweza kushika kitu mbele yako ili kuzuia kuanguka inaweza kuwa bomba lililojishika aridhini au chuma lilichojishikiza kwenye kitu au kwa kushikana mikono na mwenzako huku mkichuchumaa pamoja
Chuchumaa kutoka kwenye pozi la kusimama
Hakikisha unafanya mazoezi haya bila kujilazimisha endapo umechoka
Unapopata maumivu yoyote yale inamaanisha unafanya mazoezi haya isivyopaswa na unaweza kuwa unaharibu afya yako.
Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.
ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021
American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020
National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020
National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020
https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020
Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020
Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020
Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020
NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020
Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020