top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

3 Juni 2020, 13:42:16

Kuimarisha sakafu ya nyonga
Kuimarisha sakafu ya nyonga
Kuimarisha sakafu ya nyonga
Kuimarisha sakafu ya nyonga

Kuimarisha sakafu ya nyonga

Nyonga ni nini?


Nyonga ni sehemu ya mwili inayopatikana maeneo ya chini ya chini kidogo ya kiuno kwa juu na upande wa chini ni eneo ambalo limeshikanishwa na sakafu inayobena njia ya haja kubwa, uke/uume.


Mifupa ya nyonga


Nyonga imeundwa na mifupa miwili mikuu inayoitwa pelvis (angalia picha namba moja). Mifupa hii imefunikwa kwa misuli chini na pembeni kama ilivyo kwenye picha namba 2.


Ukuta wa chini uliofanywa na misuli hushika vilivyomo ndani ya nyonga ikiwa pamoja na via vya uzazi, mfuko wa uzazi, uke , mfumo wa mkojo na njia ya haja kubwa pia imejishikiza katika misuli ya nyonga. Misuli ya sakafu ya nyonga yenyewe kama inavyoonekana katika picha namba mbili inaonekana imeshika uke, njia ya haja kubwa, njia ya mkono, na mfuko wa uzazi. Hata hivyo kuna ogani nyingi ambazo zimeshikwa na ukuta wa sakafu ya nyonga.


Athari za ujauzito kwenye misuli ya sakafu ya nyonga


Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa wa mtoto hufanya misuli ya sakafu ya nyonga ilegee na hivyo ni vema kufanya mazoezi ili kuiimarisha na kukufanya ujifungue kirahisi zaidi na ubaki kuwa na misuli imara. Kufanya mazoezi haya hutumiwa sana kwa ajili ya kuimarisha uke, kuzuia mkojo kutoka bila ruhusa baada ya kujifungua na kufanya uke ujirudie kwenye hali ya zamani baada ya kujifungua.


Mjamzito afanye nini ili kuimarisha misuli ya sakafu ya nyonga?


Ili kimarisha misuli ya nyonga unaweza kufanya mazoezi mbalimbali


Zoezi la kwanza kaa kama kwenye picha namba nne;

Tulia na kisha waza kuhusu kubana mkojo kutoka,

Bana pia kama unazuia haja kubwa kutoka

Rudia zoezi hili mara nyingi uwezavyo kwa kubadilisha aina ya zoezi la kuzuia mkojo au kuzuia haja kubwa kutoka


Unaweza kufanya zoezi hili pia vizuri kwa kuzuia mkojo kutoka wakati unakojoa, unaweza kuzuia mara kazaa pale unapokuwa unaenda haja ndogo. Zuia na kuachia mkojo mara nyingi uwezavyo unapokuwa unakojoa.


Ni muhimu kuwa makini na zoezi hili kwa sababu mtoto huwa amekaa kwenye sakafu ya nyonga. Utatakiwa kulegeza nyonga yako ili kufanya mtoto atoke kirahisi wakati wa kujifungua. Kulegeza nyonga yako wakati wa kujifungu akutakuzuia kupata michaniko ya kwenye sakafu ya nyonga wakati wa kujifungua.

Je unaweza kufanya mazoezi mengine na zoezi la kuimarisha sakafu ya nyonga?


Ndio, kwa ufanisi zaidi fanya zoezi hili pia kwa kufanya mazoezi mengine kama kwenye picha namba 3, na picha namba tatu. Pia unaweza kusoma zaidi kuhusu mazoezi ya kuimarisha misuli ya sakafu ya nyonga kwa kusoma mazoezi ya Kegeli yaliyo kwenye tovuti hii.

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

  1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

  2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

  3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

  4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

  5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

  6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

  7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

  8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

  9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page