top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

4 Juni 2020, 07:59:12

Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi
Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi
Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi
Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi

Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi

Maelezo yaliyoandikwa hapa yatakusaidia kumwongoza mtoto wako tumboni kwenye njia ya uzazi ili uweze kujifungua kirahisi kabla ya uchungu kuanza.


Maelezo haya yanamfaa mjamzito yupi?


Maelezo haya ni kwa ajili tu ya mama mjamzito ambaye mwanae tumboni ametanguliza kichwa kwenye tundu la uzazi badala na si matako, wala mapacha. Kuanzia muda wa miezi minane na wiki mbili kuendelea, kufahamu pozi sahihi nakufanya mabadiliko kutamsaidia mtoto wako tumboni kulala vema na kutoka kirahisi kupitia tundu la uzazi kama inavyoonekana kwenye picha namba 1. Mtoto ambaye amelala vibaya kama vile kwenye picha namba 2 anaweza kugeuka na kulala vema kama inavyotakiwa kwenye picha namba moja haswa wakati wa mwisho wa ujauzito au wakati wa mwanzo wa uchungu.


Kuna faida zozote za kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi wakati wa kujifungua?


Ndio kuna faida chanya kama ukiweza kuzingatia mashariti ili uweze kujifungua kiurahisi na kumfanya mtoto asipate shida na matatizo yanayotokea kutokana na kujifungua kwa shida kama vile mtindio wa ubongo, kuchoka sana au kuchelewa kulia na mengine.


Ufanye nini ili kumwongoza mtoto kwenye njia wakati wa kujifungua?


Ili kuweza kufanikisha hayo yote ni vema kufanya mambo yafuatayo;


  • Tumia pozi kama zinavyoonekana kwenye picha namba 3 d,e na g

  • Ukiwa umelala maranyingi tumia pozi la picha namba 3g, lalia upande wa kushoto mara nyingi zaidi na weka mto katika ya mapaja na mwingine kichwani

  • Tumia mto kuweka ukutani endapo hakuna mtu wa kumwegemia kwa nyuma kama inavyoonekana kwenye picha namba 3f


Maelezo ya ziada napata wapi?


Endelea kufuatilia mwendelezo wa makala hii hapa hapa au kwa kuongea na daktari wa wamama wa ULY CLINIC

Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.

ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Oktoba 2021

  1. American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020

  2. National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020

  3. National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020

  4. https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020

  5. Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020

  6. Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020

  7. Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020

  8. NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020

  9. Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020

bottom of page