Mwandishi:
ULY CLINIC
1 Mei 2020 14:52:34
Pozi sahihi wakati wa ujauzito 1
Moja ya kitu muhimu katika afya ya ujauzito ni kukaa pozi sahihi. Kukaa pozi sahihi husaidia kupunguza maumivu ya shingo na nyuma ya mgongo na kuondoa uchovu wa kupitiliza. Hata hivyo wakati wa ujauzito mabadiliko ya kifiziolojia mwilini hutokea na huchangia mwili wa mama usikae katika mpangilio mzuri.
Maelezo katika sehemu hii yatakusaidia kukaa katika pozi la kiafya kipindi chote cha ujauzito, wakati wa kukaa, kulala na kusimama. Ukiwa na pozi sahihi, mwanao tumboni anakuwa kwenye pozi la utulivu na kujihisi vizuri pia husaidia kichwa cha mtoto kiingie vema kwenye tundu la uzazi na ujifungue kwa wepesi. Hii hupelekea mama kufurahia kipindi cha ujauzito na kupata matokeo mazuri ya mimba.
Madhara ya ujauzito kwenye mhimiri wa mwili
Pozi la mhimiri wa mwili hubadilika kutokana na ujauzito, hii ni jambo la asilia na ni kwa sababu misuli ya tumbo hutanuka jinsi mtoto anavyokuwa. Misuli ya tumbo kipindi hiki hushindwa kusinyaa vema ili kuleta mpangilio mzuri wa mgongo. Ili kupinga upinde mkubwa unaotokea nyuma ya mgongo katika kipindi hiki, ni vema ukatembea ukiwa umenyooka ili kwamba masikio, mabega, mgongo na nyonya viwe kwenye mpangilio asilia.
Namna ya kuhimarisha muhimili wa mwili
Ili kuweza kuhimirisha muhimiri wa mwili wako wakati umesimama, vitu vifuatavyo vinaweza kuwa muhimu
Hakikisha nyonga yako imekaa pozi sahihi muda wote, hii itasaidia kupinguza upinde wa mgongo wa chini
Kaza misuli ya tumbo na makalio ili ifanye kazi asilia ya kuimarisha mgongo
Ingiza ndani kidevu chako, yaani kielekee karibu na kifua na masikio yako yawe kwenye msitari mnyoofu na mabega
Zuia kuvaa viatu vyenye visigino virefu, viatu hivi husababisha uzito wako uelekee zaidi mbele ya mwili. Vaa viatu vyenye visigino vifupi na vinavyokupa uhuru
Unapofanya kazi yoyote wakati umesimama kwa kipindi kirefu kama vile kupiga pasi, kuosha vyombo, hakikisha umeweka mguu mmoja juu ya stool au jiwe au kiti kifupi, au kaa kwenye stuli ndefu, hii itazuia mgongo wako kupindia mbele.
Usikunje nne kama kwenye picha namba 3 unapokuwa umekaa kwenye kiti au kukunja miguu yako, hii itasaidia damu kupita vema
Ukiwa umekaa kaa kama inavyoonekana kwenye picha namba 4 kwa kuweka miguu chini ya stuli fupi
Mambo ya kutofanya ili kutoharibu muhimili wa mwili wako
Zuia kuupa upinde mgongo wako na pozi lolote lile la kujikuunjia mbele. Simama wima na legeza mabega yako, fanya hivi kwa namna yoyote ile na unapotembea tembea ukiwa unapishanisha mikono yako mmoja baada ya mwingine.
Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.
ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021
American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020
National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020
National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020
https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020
Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020
Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020
Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020
NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020
Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020