Mwandishi:
ULY CLINIC
2 Juni 2020, 11:39:26
Upumuaji mzuri wakati wa ujauzito
Ukiwa kwenye hali ya kawaida, mjongeo wa kifua na upumuaji hufanyika kawaida kulinga na mahitaji ya mwili wako na unavyopenda. Wakati wa ujauzito, mtoto tumboni hukua na huchukua nafasi ya kutosha kiasi cha kupunguza nafasi kwa ajili ya kupumua vema. Hii ndo maana unaweza kuhisi kuishiwa pumzi wakati huu wa ujauzito.
Namna ya kutambua aina ya upumuaji wako kwenye ujauzito?
Endapo unataka kujua namna unavyopumua fanya yafuatayo;
Kaa pozi zuri lenye uhuru(Unaweza kukaa au kulala)
Weka mikono yako miwili eneo la chini ya mbavu/kifua
Vuta pumzi kupitia pua kiasi cha kusukuma mikono yako uliyoweka chini ya kifua kwa jinsi unavyoweza. Toa pumzi kupitia mdomo. Rudia zoezi hili mara tatu kwa siku.
Rudia zoezi hilo hapo juu wakati umeweka mikono kwenye tumbo
Madhara ya kuvuta pumzi vibaya wakati wa kujifungua
Ulipokuwa unavuta pumzi kwenye zoezi la hapo juu, kifua kilikuwa kinapanuka taratibu. Mijongeo ya kifua na tumbo ni muhimu sana wakati wa upumuaji wa kawaida. Kuvuta pumzi kunaweza kuwa hatari kwa mama na mtoto tumboni.
Hatari inatokea endapo
Unapopumua haraka haraka haswa wakati uchungu upo kileleni
Unaposimamisha pumzi
Kupumua haraka haraka na si kwa kina. Hii husababisha hewa kidogo kuingia kwenye mapafu na hupelekea haipoventilesheni
Kupumua taratibu na kwa kina huweza kusababisha haipaventilesheni na kupelekea kuhisi ganzi ya vitu kuchomachoma vidoleni.
Upumuaji wakati wa ujauzito na kujifungua
Wakati wa ujauzito na kujifungua, unahitajika kutilia umaanani kupumua kawaida. Wakati wa leba(uchungu) kila uchungu unavyotokea unatakiwa kuongeza upumuaji na kuvuta hewa kwa kina na kwa urahisi iwezekanavyo. Pumua kawaida bila kutumia nguvu za ziada.
Namna ya kupumua vema wakati wa kujifungua
Tumia pozi kama linaloonekana kwenye picha kisha pumua taratibu wakati unataka kuanza kufanya mazoezi yoyote yale.
Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.
ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021
American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020
National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020
National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020
https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020
Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020
Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020
Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020
NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020
Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020