Mwandishi:
ULY CLINIC
17 Mei 2020 17:50:56
Kujikunja, kunyanyua vitu na kufanya kazi ukiwa umesimama
Una hatari ya kupata msongo mgongoni wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua, hii ni kwa
sababu ya mabadiliko ya homoni wakati huu ambayo hulainishamaungio ya mwili na ligament
zinazoshikiria maungio hayo.
Ili kupunguza msongo kwenye mgongo fanya mambo yafuatayo hapo chini;
Kunyanyua na kufikia mzigo
Ili kunyanyua au kukifikia kitu, kaa mguu pande na tanguliza mguu mmoja mbele ya mwingine kisha kunja maungio ya goti
Kubeba na kuhamisha mzigo wakati wa ujauzito
Sogeza karibu kitu unachotaka kukibeba na kisha nyoosha maungio ya goti unapoinuka.
Hii inakuruhusu kutumia misuli ya mapaja tu kunyanyua hicho kitu kuliko kutumia misuli ya mgongo.
Unapohamisha kitu, kisukume badala ya kukivuta. Tumia miguu na sio mgongo au mikono.
Mambo usiyotakiwa kufanya wakati wa kunyanyua mzigo kwenye ujauzito
Kamwe usikunje kiuno chako wakati magoti yamenyooka, hata kama ni kupinda kidogo tu kuokota kitu. Mbadala wake, badili pozi kama vile unakaa au kuchuchumaa, kupiga magoti au kukunja goti wakati unataka kukifikia kitu kwa kukunja goti. Angalia picha ya namna ya kunyanyua vitu vizito.
Kunyanyua mzigo mkubwa wakati wa ujauzito
Kama mzigo unaonunua ni mkubwa, uvunje uwe kwenye sehemu mbili na ubebe kama inavyoonekana kwenye picha.
Muulize daktari wako siku zote endapo mazoezi haya yatakufaa kulingana na hali ya afya yako.
ULY clinic inakukaribisha kwa ushauri na Tiba. Wasiliana nasi kupitia namba za simu au bonyeza kitufe cha ‘Pata Tiba’ chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Oktoba 2021
American Pregnancy Association. Sleeping positions during pregnancy. Imechukuliwa 28.04.2020
National Sleep Foundation. The best position for sleep during pregnancy.Imechukuliwa 28.04.2020
National Posture Institute. Incorporating NPI’s 4 points of posture during pregnancy and postpartum. Imechukuliwa 28.04.2020
https://www.pregnancyexercise.co.nz/products/fit2birthmum/. Imechukuliwa mara ya mwisho 3.06.2020
Malposition and malpresentantio. https://www.gfmer.ch/Obstetrics_simplified/malpresentations_and_malposition.htm. Imechukuliwa 04.06.2020
Ocipitalposterior.https://www.uptodate.com/contents/occiput-posterior-position. Imechukuliwa 04.06.2020
Pushing the baby out.https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/childbirth-stages/pushing-and-delivery.aspx. Imechukuliwa 06.06.2020
NCBI. When and where to puch. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1804305/. Imechukuliwa 06.06.2020
Pushing during labor more isint better. https://www.parents.com/pregnancy/giving-birth/labor-and-delivery/pushing-during-labor-more-isnt-better/. Imechukuliwa 06.06.2020