top of page

Mazoezi ya kujiandaa mwili dhidi ya  leba na kujifungua salama

Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo

Mazoezi ya kuimarisha misuli ya Tumbo

Kabla hujaanza kufaya mazoezi haya, ni vema ukaelewa kwanza taarifa zifuatazo kuhusu kuitenganisha misuli ya tumbo. Wakati wa ujauzito, mstari mweusi unaoitwa linea alba hujitokeza katikati ya mwili nje ya tumbo. Hii ni kwa sababu ya mabadiliko ya homoni kwa mama mjamzito yanayoletwa na ujauzito. Msatri huu huligawa tumbo kwenye sehemu mbili iznazofanana.

Kuandaa nyonga kabla ya kujifungua

Kuandaa nyonga kabla ya kujifungua

Wakati wa kujifungua unapokaribia, mtoto atashuka chini ya tumbo kuelekea kwenye shimo la nyonga katika pozi la kichwa chini matako juu. Jukumu lako kubwa ni kujiweka fiti kimwili ili kumwezesha mtoto apite kirahisi kwenye nyonga na tundu la uzazi.

Kuimarisha sakafu ya nyonga

Kuimarisha sakafu ya nyonga

Nyonga ni sehemu ya mwili inayopatikana maeneo ya kiuno, sehemu hii imeundwa na mifupa miwili mikuu inayoitwa pelvis(angalia picha namba moja). Mifupa hii imefunikwa kwa misuli chini na pembeni kama ilivyo kwenye picha namba 2.

Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi

Kumwongoza mtoto kwenye pozi sahihi ili ujifungue kirahisi

Maelezo yaliyoandikwa hapa yatakusaidia kumwongoza mtoto wako aliye tumboni kwenye njia ya uzazi ili uweze kujifungua kirahisi kabla ya uchungu kuanza.

Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua

Mapozi ya kukaa wakati wa uchungu na kujifungua

Katika kipindi uchungu unaanza hadi kipindi unajifungua, masaa kadhaa yatapita. Kwa mama ambaye anaujauzito wa kwanza inaweza kuchukua muda wa masaa 11 toka uchungu umeanza mpaka kujifungua endapo uzazi ni wa kawaida.

bottom of page