top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

 

Kinywa kutoa harufu mbaya

​

​

Utangulizi

​

Kinywa kutoa harufu mbaya huweza kuwa kero kwako  binafsi au kwa watu wanaokuzunguka.

​

Yapo matibabu aina mbalimbali dhidi ya kinywa kutoa harufu mbaya, ikiwepo pamoja na pipi, bigijii na dawa za kusafisha meno

​

Dawa hizi huweza kuwa zinafanya kazi au kutomsaidia mtu. Jambo la msingi ni kufahamu nini kisababishi na kuanza matibau ya

 

​

Dalili

​

Harufu ya kinywa hutofautiana kutokana na nini kilichosababisha, baadhi ya watu hupata hofu sana kuhusu harufu ya kinywa ingawa wana harufi kidogo inayotoka, na kuna wengine wanavinywa vinavyotoa harufu mbaya bila wao kujitambua. Siku zote muulize jirani yako endapo kinywa chako kinatoa harufu au la.

 

Visababishi

​

Kuna visababishi mbalimbali vinavyoweza kupelekea kinywa kutoa harufu mbaya, mara niyngi huwa chakula, Tania na hali ya kiafya ya mtu

​

Chakula

​

Vyakula jamii ya vitunguu, tangawizi, na viungo vingi vinavyotumika kwenye chakula endapo vitameng'enywa na bakteria katika kinywa huleta harufu mbaya ya kinywa. Vyakula jamii ya nyama pia endapo vitaliwa na kubaki katika kinywa huoza na kusababisha harufu mbaya kutoka kinywani

 

Kutofanya usafi wa kinywa

​

Kama husafishi kinywa kwa dawa ya mswaki na kuchukuchua mdomo mara haswa baada ya kula  wakati wa jioni, utapata harufu mbaya mdomoni kutokana na vyakula hivyo vinavyobaki kinywani kuozeshwa na bateria pamoja na vimeng'enya. Vyakula mara nyingi vikibaki kinywani hutengeneza ukuta kuzunguka meno na ulimi na kuta hizi ni chakula kizuri kwa bakteria waliopo mdodomoni. Bakteria wanapokula kuta hii husababisha kuzalisha kwa tindikali na harufu mbaya mdomoni

 

Midomo kukauka

​

Mate husaidia kuosha mdomo dhidi ya mabaki ya chakua na harufu, endapo mtu ana midomo iliyokauka, kwa kukosa unyevu wake atapata harufu mbaya kinywani. Midomo kukauka hutokea sana wakati wa usiku kama asili ya maumbile ya binadamu na hivyo mtu kuamka na harufu mbaya kinywani wakati wa asubuhi. Tatizo la harufu mbaya kinywaji huzidi endapo mtu amelala kinywa kikiwa wazi.

​

Baadhi ya dawa

​

Dawa zinazokausha mate husababisha kinywa kutoa harufu kama yalivyo maelezo  ya hapo juu. Baadhi ya dawa pia huwa na kemikali ambazo zikivunywa kinywani au tumboni husababisha mtu kuwa na harufu mbaya kinywani.

​

Maambukizi ya kinywa

​

Mtu akiwa na maambukizi kinywani huweza kutoa harufu mbaya. Maambukizi haya yanaweza kuwa kwenye vidonda vinavyotokana na upasuaji, kutolea jino, kuoza kwa meno au magonjwa mengine ya kinywa na meno, magonjwa ya kinywa, koo na pua kama tonsil n,k

​

Saratani, magonjwa ya kimetaboliki na tatizo la kiungulia huweza kusabaisha kinywa kutoa harufu kali, watoto wadogo wanaweza kutoa harufu kali kinywani kutokana na vipande vya chakula kubaki kinywani.

​

Mara nyingi mtu anaweza kuimarisha afya ya kinywa chake kwa kuzingatia usafi wa kinywa.

​

​

Matibabu

​

Matibabu ya kinywa kutoa harufu mbaya hutegemea kisababishi, endapo una magonjwa ya fizi ni vema ukapata matibabu ya maambukizi hayo upamoja na kufanya usafi wa kinywa chako. Shirikiana na daktari wako kwa ufanisi zaidi kwa kufanya mambo yafuatayo

​

Safisha kinywa kwa kutumia dawa ya meno na mswaki, kisha susukutua na maji safi na kutema. Endapo meno yako yana ukuta wa uchafu, utapewa dawa ya meno yenye uwezo wa kutoa ukuta huo wa bakteria unaosabisha kinywa chako kutoa harufu mbaya.

​

Pata matibabu ya magonjwa ya kinywa- endapo kinywa chako kina maambukizi, utapatiwa dawa za kutibu maambukizi hayo. Kuna wakati utahitaji kusafishwa meno na daktari wako ili kuondoa bakteria kwenye vijishimo vilivyo kwenye mashina ya meno.

​

Safisha meno yako kila siku hata baada ya kula chakula, endapo unaenda kazini, nenda na mswaki wako kwa ajili ya kuutmia baada ya kula chakula. Tumia dawa za meno zenye fluoride kusafishia kinywa chako angalau mara mbili kwa siku.

​

Badilisha mswaki wako mara kwa mara unapokuwa umechakaa au kuchanuka chanuka, chagua mswaki laini usioumiza kinywa chako.

​

Rekebisha mlo wako kwa kuepuka kula vyakula vyenye vitunguu swaumu au vitunguu maji na vyenye sukari kwa wingi ambavyo husababisha kinywa kutoa harudu mbaya.

​

Chukutua kinywa chako kwa maji safi ya uvuguvugu angalau mara tatu  kwa siku, hii husaidia kuondoa mabaki ya chakula kinywani mwako, hii inasaidia sana kupunguza harufu mbaya ya kinywa

​

Hakikisha unasafisha ulimi wako wakati unapiga mswaki, ulimi unapaswa kuwa safi, hii ni  kwa sababu uchafu unaobaki kwenye ulimi huozeshwa na bakteria wa kinywani na kuleta harufu mbaya ya kinywa. Tumia  kikwangua ulimi maalumu kabisa kutoa ukuta wa juu ya ulimi(mabaki ya chakula)

​

Safisha vidani vyako  au meno ya bandia unayovaa kinywani angalau mara moja kwa siku ili kuondoa kuta za bakteria katika vidani hivyo vya kuvaa kinywani

​

Hakikisha kinywa chako hakiwi kikavu, kunywa maji safi ya kutosha na siyo kahawa, pombe au vinywaji vingine laini, epuka kuvuta sigara ili kuepuka kinywa kuwa kikavu na kutoa harufu mbaya. Unaweza kutafuna pia bablishi au kulamba pipi ambazo zitakuongezea uzalishaji wa mate na kufanya kinywa chako kisiwe kikavu na kutoa harufu mbaya.

​

​

Onana na daktari wako kwa uchunguzi wa kinywa endapo tatizo lako linaendelea licha ya kufanya mambo haya

​

Soma kuhusu meno kutoboka hapa

​

Soma zaidi kuhusu makala nyingine  ya kinywa kutoa harufu mbaya kwa kubonyeza hapa

​

ULY clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako endapo umepata dtatizo hili kwa ushauri na tiba

​

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia kitufe cha "Pata Tiba" au namba za simu  zilizo chini ya tovuti hii.  

​

Imeboreshwa, 30/11/2020

​

​

Rejea za mada hii;

​

  1. What is halitosis? Academy of General Dentistry. http://www.knowyourteeth.com/infobites/abc/article/?abc=H&iid=306&aid=1254. Imechukuliwa 26.11.2020

  2. Dry mouth. National Institute of Dental and Craniofacial Research. http://www.nidcr.nih.gov/oralhealth/topics/drymouth/drymouth.htm. Imechukuliwa 26.11.2020

  3. Should I floss? Academy of General Dentistry. http://www.knowyourteeth.com/infobites/abc/article/?abc=f&iid=302&aid=1244. Imechukuliwa 26.11.2020

  4. Diagnosing and treating bad breath. Dental Abstracts. 2014;59:203.

  5. Tongue scrapers only slightly reduce bad breath. Academy of General Dentistry. http://www.knowyourteeth.com/infobites/abc/article/?abc=t&iid=306&aid=3192. Imechukuliwa 26.11.2020

  6. Bad breath (halitosis). (2016, March 9). http://www.nhs.uk/conditions/Bad-breath/Pages/Introduction.aspx. Imechukuliwa 26.11.2020

  7. Bronchiectasis. (2015, June 15). http://www.nhs.uk/conditions/bronchiectasis/Pages/Introduction.aspx. Imechukuliwa 26.11.2020

  8. Diabetic ketoacidosis. (2017, April 24). https://www.nhs.uk/conditions/diabetic-ketoacidosis/. Imechukuliwa 26.11.2020

bottom of page