Imeandikwa na ULY CLINIC
​
Mhariri: Dkt Benjamin L, MD
Imeandikwa: 04.07.2019
Tatizo la mimba Kuharibika
​
Utangulizi
​
Tatizo la mimba kutoka au mimba kuharibika hutokea endapo mimba imetoka kabla ya wiki 20 za ujauzito. Asilimia 10 hadi 20 ya ujauzito zinazotokea duniani, hutoka, idadi halisi hata hivyo inawezekana kuwa kubwa kwa sababu mimba nyingi hutoka mapema zaidi kiasi kwamba mwanamke hajui kama alikuwa na ujauzito.
​
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha mimba kuharibika, inaweza kuwa upungufu wa vitu mwilini mwa mama wakati wa kubeba ujauzito na wakati mwingine sababu hii haina mashiko.
Mimba nyingi hufikirika kuharibika kwa sababu madhaifu ya kuumbika vema kwa kijusi kutokana na madhaifu katika vinasaba. Wakati mwingine, karibia asilimia 50 ya mimba zinazotoka, kisababishi huwa hakifahamiki.
​
Mimba inapoharibika usihofu, utaaswa kukaa chini na daktari wako ili kwa pamoja mtambue visababishi na mambo ambayo yamekuweka hatarini kupata tatizo hili.
​
Dalili za mimba Kuharibika
Mimba nyingi huharibika kabla ya wiki 12 za ujauzito.Dalili na ishara za mimba kuharibika zinaweza kuwa kati ya zifuatazo;
-
Kutokwa damu ukeni au matone ya damu.
-
Maumivu ya tumbo la uzazi ya kubana au maumivu ya mgongo.
-
Kutokwa na majimaji au mabonge ya tishu za mtoto
Kama umepitisha tishu za mtoto ukeni unaweza kuziweka katika kopo safi na kupeleka kwa daktari wako au hospitali kwa ajili ya vipimo na utambuzi.
Kumbuka kwamba wanawake wengi wanaopata au kuona damu au kutokwa na damu katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito , ujauzito huendelea na hatimaye kijifungua mtoto aliyekamilika.
​
Visababishi vya kuharibka mimba
Kuwa na jeni/vinasaba visivyo vya kawaida
​
Tatizo la jeni linaweza kusababisha mtoto kufanyika kwa namna isiyo ya kawaida. Matatizo ya jeni yanaweza kutokea wakati yai lililoshavushwa linagawanyika ili kufanya chembe za kijusi. Tatizo hili hutokea na si wakati wote huwa ya kurithi, mfano wa udhaifu katika jeni na utengenezaji wa mtoto ni;
-
Kutotengenezwa kwa kijusi kutoka kwenye yai
-
Kijusi kutoendelea kuumbwa/hatua za utengenezaji wa mtoto husimama hatimaye mtoto hakui, hufa / kupoteza maisha.
-
Ujauzitozabibu – hili ni tatizo la viumbe usio saratani, hutokea endapo kuna seti nyingi za jeni za baba kwenye yai lililochavushwa, tatizo hili linapotokea ukuta ambao ulitakiwa kuwa kondo la nyuma hubadilishwa na kuwa vijifuko vidogo vilivyojaa maji na kuwa na mwonekao wa zabibu, tatizo hili ni nadra kama sababu ya ujauzito kutoka.
-
Hali ya afya ya mama.
-
Kwa wamama wachache, afya ya mama inaweza kupelekea mimba kutoka kwa mfano
-
​Ugonjwa wa kisukari ulioshindwa kudhibitiwa
-
-
Mambo yasiyosababisha mimba kuharibika
​
1. Kazi za kila siku
​
kazi zifuatazo huwa hazipelekei mimba kuharibika:
-
Kujamiiana
-
Kufanya kazi
-
lakini unatakiwa usijiweke kwenye vihatalishi kama kemikali au mionzi.
-
​
Vitu hatarishi vinavyo weza kusababisha mimba kuharibika
Sababu mbalimbali zinaweza kuongeza hatari ya mimba kutoka kama.
-
Umri - wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35 wana hatari ya kutokwa mimba kuliko wanawake walio chini ya umri huo. Unapofikisha miaka 35 unakuwa kwenye hatari mara 20 zaidi ukiwa na miaka 40 hatali mara 40 zaidi miaka 45 hatari mara 80 zaidi.
-
Umri wa Baba nao unaweza kuchangia kwa kiasi kidogo kutokana na tafiti zilizofanyika
-
Historia ya ujauzito uliopita kutoka: wanawake ujauzito wa kwanza uliharibika wapo katika hatari zaidi ya wale ambao hawana historia hii
-
Magonjwa sugu-Wanawake wenye magonjwa sugu kama kisukari kisicho dhibitiwa wapo na hatari kubwa ya kutokwa na ujauzito
-
Matatizo kwenye mfumo wa uzazi na shingo ya uzazi- matatizo kwenye shingo ya uzazi kama udhaifu kwenye chembe za shingo ya kizazi na matatizo ya kuta za uzazi huongeza hatari ya ujauzito kutoka .
-
Uzito; kuwa na uzito kidogo au uzito mkubwa sana huambatana na mimba kutoka.
-
Vipimo; vipimo wakati wa ujauzito kama kile cha kuchukulia maji kwenye chupa ya uzazi huongeza hatari ya mimba kutoka.
​
Madhara ya mimba kuharibika
Baadhi ya wanawake ambao mimba zao zimetoka wanaweza kupata maambukizi kwenye uzazi, dalili na ishara huweza kuwa;
-
Homa
-
Kutetemeka
-
Maumivu ya tumbo la uzazi
-
Kutokwa na uchafu unaonuka vibaya ukeni
-
Mshituko wa moyo
​
VIpimo
Dakitari wako atafanya vipimo mbalimbali vya kutambua kisababishi kama vile:
-
Vipimo vya uchunguzi wa mwili ya maeneo shingo ya kizazi kuangalia kama imeanza kufunguka
-
Picha ya mionzi sauti – (ultrasound) – Kipimo hiki kitamsaidia dakitari wako kuangalia mapigo ya moyo ya kijusi na kama mtoto ana kuwa vyema.
-
Kipimo cha damu – Kama ujauzito umetoka unaweza kupimwa vichocheo vinavyohusika na suala la ujauzito, kipimo cha kuonyesha kama una ujauzito (HCG). Vipimo hivi ni vya umuhimu ili kuonyesha kama ujauzito umetoka kabisa.
-
Kipimo cha chembechembe(tishu) za ujauzito– Endapo umepitisha tishu za kijusi wakati ujauzito unatoka, chembe hizo zitapimwa maabra ili kuangalia kama zinahusiana na ujauzito au tatizo linguine.
Aina za mimba kuharibika
Baada ya vipimo hapo juu, dakitari anaweza kukuambia tatizo lako ni nini kama vile;
-
Kuharibika kwa viashiria vya kikemia- Kwa wanawake ambao mimba imechavushwa kwa njia za saidizi za kitekinolojia, kabla ya wiki ya 6, kiwango cha homoni ya ujauzito HCG kupungua. Wakati huu kwenye Ultrsound mimba huwa bado haionekani.
-
Mimba iliyotoka bila dalili- Ikiwa mimba imeharibika pasipo kuwa na dalili yoyote ikiwa pamoja na kutokwa na tishue za mimba.
-
Mimba inayotishia kutoka - Ikiwa unatokwa na damu lakini shingo ya uzazi haijatanuka bado. Ujauzito huu unaweza kuendelea vizuli bila tatizo lolote.
-
Mimba iisiyozuilika kutoka – Ikiwa unatokwa na damu, tumbo la uzazi linabana na kusinyaa na shingo ya uzazi imefunguka basi mimba hii nilazima itoke.
-
Mimba iliyotoka nusu - Endapo umepitisha tishu ukeni zinazoashiria uwepo wa kijusi tumboni lakini chembe zingine zime baki.
-
Mimba imetoka nusu – Endapo chembechembe za mtoto zimebaki kwenye kuta za uzazi humaanisha mimba imetoka nusu .
-
Mimba imeharibika - Endapo londo la nyuma na chembe za mtoto zimabaki ndani ya mfuko wa uzazi lakini mtoto hayupo hai.
-
Mimba iliyokamilika kutoka - Endapo kondo la nyuma na chembe za mtoto zimetoka zote. Hutokea mara nyingi kabla ya wiki 12 na ujauzito.
-
Mimba inayojirudia kuharibika- Kuwa na hali ya kuharibika mfululizo kwa ujauzito mara 2 au zaidi, baadhi ya wataalamu husema kupoteza mimba 3 au zaidi mfululizo.
-
Maambukizi ya mimba iliyotoka– Endapo maambukizi yametokea katika mfuko wa uzazi. Tatizo hili linaweza kuambatana na maambukizi mabaya na kuhitaji matibabu ya haraka.
​
Matibabu
​
Matibabu hutegemea aina ya mimba kutoka ambapo hufahamika baada ya kufanyiwa vipimo. Matibabu hayo huhusisha.
Mimba iliyotishia kutoka
-
kama ukiwa na tatizo hili daktari atakushaulri upumzike mpaka damu na maumivu yatakapoisha.
-
Unaweza kuambiwa uepuke mazoezi na kujamiana pia, ingawa hatua hizi hazija hakikiwa kupunguza hatari ya mimba kutoka zinawea kukusaidia kupata faraja.
-
Ni wazo jema pia kuacha kusafiri sana kwenda maeneo ambapo ni vigumu kupata msaada wa kiafya endapo utapata matatizo
​​
Matibau ya Mimba iliyokamilika kutoka
-
Kwa kutumia kipimo cha ultrasound hivi sasa ni rahisi kujua kwamba mtoto amefia tumboni au hakutengenezwa kabisa. Kipimo hiko kitaonyesha hali ya mimba na uamuzi wa nini cha kufanya kuamriwa na daktari kutokana na vipimo.
​Matibabu unayotarajia kupatiwa kwa mimba zilizoharibika
-
Kama huna ishara na dalili za maambukizi unaweza kuchagua ujauzito utoke wenyewe bila kuanzishiwa uchungu. Kwa njia ya kusubiri mimba inaweza kutoka wiki kadhaa baada ya mwili kugundua kwamba ujauzito haupo hai. Mara nyingine inaweza kuchukuwa wiki tatu na hili linaweza kumdhuru mama kihisia na kisaikolojia na hiyo kama uchungu hauta anza wenyewe basi madawa yatatumika kuamisha uchungu au kutumia njia ya upasuaji.
​​
-
Dawa- kama tatizo lako limeshajulikana umepoteza ujauzito unaweza kuchagua njia hii ya dawa ili kuharakisha ujauzito wote kutoka [ kondo la nyuma na chembe za mtoto] dawa unaweza kunywa na nyingine kuwekewa ukeni maeneo ya shingo ya uzazi asilimia 70 hadi 90 ya wanawake matibabu haya hufanya kazi ndani ya masaa 24.
Matibabu ya nyumbani na kubadili mfumo wa maisha
Tiba ya mwili; Unaweza kuchukuwa masaa machache au siku kadhaa kupona kabisa , onana na daktari endapo unaona damu inatoka sana au maumivu makali ya tumbo.
Siku zako za mzunguko wa hedhi zinaweza kurudi ndani ya wiki 4 hadi 6 . unaweza kuanza kutumia uzazi wa mpango baada ya mimba kutoka zuia kujamiiana na kuweka vitu kama pedi za kuchomeka ukeni kwa wiki baada ya ujauzito kutoka.
Lini upate Ujauzito mwingine baada ya mimba kuharibika
Inawezekana kupata mimba nyingine mzunguko wa hedhi utakaporudi baada ya mimba kutoka lakini kama wewe na mpenzi wako mmeamua kutaka ujauzito mwingine hakikisheni kwamba mama yupo tayari kimwili na kisaikoloji. Unawez akupata ujauzito wakati wowote mnapokuwa tayari.
​
Kumbuka kwamba mimba kuharibika maranyingi hutokea mara moja tu. Wanawake wengi wanaopoteza ujauzito watakapopata ujauzito mwingine huweza kuendele na kuzaaa mtoto kama mwanamke ambaye hajawahi kupoteza ujauzito. Kati ya asilimia 5 ya wanawake wliopoteza ujauzito miwili mfululizo, asilimia 1 tu hupoteza kwa mara ya tatu mfululizo.
Kama ujauzito au mimba zikiwa zinatoka mara kwa mara na zaidi ya mara tatu, ongea na dakitari wako ili afanye vipimo kugundua hasa ni nini kinachosababisha tatizo hilo, yanaweza kuwa matatizo ya mfuko wa kizazi, magonjwa ya ugandishaji damu, au madhaifu katika jeni zako za uzazi. Dakitari anaweza kukushauri kufanya vipimo hivi wakati umepoteza mimba ya pili mfululizo.
​
Kama sababu isipo fahamika, usikate tama maana asilimia 60 hadi 70 ya wanawake wanaopata tatizo hili, visababishi vinavyoambatana na kuharibika kwa mimba zao huwa havifahamiki kwa vipimo, hata hivyo huweza kupata ujauzito na kuzaa mtoto mwenye afya njema katika maisha yake
Kukabiliana na matokeo
Mara baada ya mimba kuharibika mara moja au mbili, unaweza kupata shida ya saikolojia na kimwili pia. Kupona kisaikolojia huchukua muda mrefu kwa wanawake wengi kuliko kupona maumivu ya mwili. Unapofikia hatua hii, unatakiwa ujitie moyo shupavu na uwe na imani mambo yatakaa vyema. Unaweeza kufikia kipindi cha kujihukumu mwenyewe kuhusu yaliyotokea, na kupata hasira na kuhisi ni mtu wa kudharauliwa.
​
Upatapo dalili hizi, jipe muda wa kuomboleza kwa mimba iliyoharibika na tafuta msaada kutoka kwa wapendwa, na daktari wako, epuka kukaa mwenyewe na kuwaza sana kuhusu jambo lililotokea kwani linakuweka hatarini kupata magonjwa ya kiakili.
​
Unaweza usisahau matumaini yako na ndoto kuhusu ujauzito uliopotea, lakini kukubali kuhusu lililotokea litakusaidia kupunguza maumivu moyoni na hisia. Ongea na dakitari wako endapo unajihisi huzuni sana au msongo wa mawazo unazidi
Mambo ya kufanya ili kuzuia mimba kutoka
Mara nyingi hakuna unachoweza kufanya ili kuzuia mimba kutoka. Cha msingi unatakiwa kutunza ujauzio wako vyema kwa kufuata ushauri wa kiafya unaopew ana mtaalamu wa Afya. Tafuta au hudhuria huduma za kiafya kama kliniki ya ujauzito kisha zuia vihatarishi vinavyofahamika kusabaisha madhara katika ujauzito wako kama vile uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe na kahawa kwa wingi. Kama una magonjwa sugu, mfano mgonjwa wa kisukari, na shinikizo la juu la damu, hakikisha unashirikiana na dakitari wako na kufata taratibu za matibatu wakati wote wa matibabu kujiondoa hatarini na matatizo yatokanayo na gonjwa hili katika ujauzito
​​​
Kusoma kuhusu kutoa mimba na madhara yake bonyeza hapa
​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyoteyanayodhuru afya yako.
​
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 08.10.2024
​
Rejea za mada hii;
​
-
Tulandi T, et al. Definition and etiology of recurrent pregnancy loss. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Tulandi T, et al. Evaluation of couples with recurrent pregnancy loss. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Septic abortion. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/abnormalities-of-pregnancy/septic-abortion. Imechukuliwa 04.07.2020
-
What is recurrent pregnancy loss (RPL)? American Society for Reproductive Medicine. https://www.asrm.org/uploadedFiles/ASRM_Content/Resources/Patient_Resources/Fact_Sheets_and_Info_Booklets/recurrent_preg_loss.pdf. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Para A, et al. Exercise and pregnancy loss. American Family Physician. 2015;91:437. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Moscrop A. Can sex during pregnancy cause a miscarriage? A concise history of not knowing. British Journal of General Practice. 2012;62:e308. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3310038/. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Risk factors for miscarriage from a prevention perspective: A nationwide follow-up study. BJOG: An international journal of obstetrics and gynaecology. 2014;121:1375. https://www.clinicalkey.com/#!/content/medline/2-s2.0-24548778. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Tulandi T, et al. Spontaneous abortion: Risk factors, etiology, clinical manifestations, and diagnostic evaluation. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Spontaneous miscarriage. In: Ferri's Clinical Advisor 2016. Philadelphia, Pa.: Mosby Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Recurrent pregnancy loss. In: Creasy and Resnik's Maternal-Fetal Medicine: Principles and Practice. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2014. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Ectopic pregnancy and miscarriage. National Institute for Health and Care Excellence (NICE). https://www.clinicalkey.com/#!/content/nice_guidelines/65-s2.0-QS69. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Marx JA, et al., eds. Acute complications of pregnancy. In: Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 8th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2014. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.07.2020
-
Quenby S, Gallos ID, Dhillon-Smith RK, Podesek M, Stephenson MD, Fisher J, Brosens JJ, Brewin J, Ramhorst R, Lucas ES, McCoy RC, Anderson R, Daher S, Regan L, Al-Memar M, Bourne T, MacIntyre DA, Rai R, Christiansen OB, Sugiura-Ogasawara M, Odendaal J, Devall AJ, Bennett PR, Petrou S, Coomarasamy A. Miscarriage matters: the epidemiological, physical, psychological, and economic costs of early pregnancy loss. Lancet. 2021 May 01;397(10285):1658-1667. [PubMed]
-
Schliep KC, Mitchell EM, Mumford SL, Radin RG, Zarek SM, Sjaarda L, Schisterman EF. Trying to Conceive After an Early Pregnancy Loss: An Assessment on How Long Couples Should Wait. Obstet Gynecol. 2016 Feb;127(2):204-12. [PMC free article] [PubMed]
-
Sundermann AC, Hartmann KE, Jones SH, Torstenson ES, Velez Edwards DR. Interpregnancy Interval After Pregnancy Loss and Risk of Repeat Miscarriage. Obstet Gynecol. 2017 Dec;130(6):1312-1318. [PMC free article] [PubMed]
-
Stirrat GM. Recurrent miscarriage. Lancet. 1990 Sep 15;336(8716):673-5. [PubMed]
-
Pillarisetty LS, Mahdy H. StatPearls [Internet]. StatPearls Publishing; Treasure Island (FL): Aug 28, 2023. Recurrent Pregnancy Loss. [PubMed]
-
Birch JD, Gulati D, Mandalia S. Cervical shock: a complication of incomplete abortion. BMJ Case Rep. 2017 Jul 14;2017 [PMC free article] [PubMed]
​
​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​