top of page

Nini cha kufanya baada ya kutoa mimba ama baada ya mimba kutoka

​

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

​

Utangulizi

Mimba kutoka ni kitendo ambacho huambatana na kutokwa damu kwa kiasi kikubwa, na jambo hili ni la kweli endapo mimba ilipangwa kutolewa yaani induced abortion. Kwa sababu hiyo mtu anaweza kupoteza kiwango kikubwa cha damu katika mwili wake na kusababisha kupata dalili mbalimbali zikiwa ni pamoja na

  • Kuhisi kizunguzungu

  • Mapigo ya moyo kwenda haraka

  • Kujaa maji kwenye miguu ama mapafu

  • Mwili  kuwa mchovu

  • Kuchoka haraka unapofanya kazi

  • Wakati mwingine hata kushuka kwa shinikizo la damu

 

Mtu kwa kawaida mtu ana lita 4.5 hadi 5 za damu, inayozunguka katika mishipa ya damu, na endapo mtu amevuja damu ya kutosha basi kiwango cha damu kwenye  mishipa ya damu hupungua sana, na hili hupelekea kushuka kwa shinikizo la damu hatimaye damu hushindwa kusafili na kufika katika maeneo muhimu. Endapo mtu huyu atasimama basi kiwango cha damu kinachoenda kwenye ubongo hupungua na mtu atapata dalili kama vile;

  • Kizunguzungu

  • Kutoona ama kuhisi giza kuu

  • Kuanguka chini

​

Mambo haya hutokea makusudi, mtu anapoanguka na kulala chini basi moyo hupata urahisi wa kusukuma kiwango kidogo cha damu kupeleka kwenye ubongo na kusaidia ufanye kazi, hivyo mtu anayepoteza damu hakikisha amelala kichwa chini zaidi na miguu juu yaani sehemu ya miguu iwe juu zaidi kuliko kichwa.

​

Mambo gani sasa ya kufanya unapotokwa na damu nyingi baada ya kutoa mimba ama mimba kutoka yenyewe

​

Unapokuwa maeneo ya hospitali ni dhahiri kwamba utapimwa kiwango cha damu katika mwili ama HB grouping, kiwango hicho kitamsaidia mtaalamu wa afya kujua matibabu gani akupe, ingawa unaweza kuwa na kiwango cha chini cha damu wakati mwingine huwezi kuongezewa damu labda uwe na dalili kama zilizotajwa hapo juu

​

Kiwango cha wingi wa damu kimegawanywa katika makundi matatu

  • Upungufu wa damu wa kawaida ambapo damu yako inakuwa chini ya 12g/dl lakini juu ya 9g/dl

  • Upungufu wa damu wa wastani (7-9) g/dl

  • Upungufu wa damu mkali (4-7) g/dl

  • Upungufu wa damu mkali sana chini ya 4g/dl

​

Katika viwango vyote hapo juu mtu anapokuwa na upungufu wa damu kati ya 11-9g/dl na 7-9 basi unaweza kushauriwa kuhusu kutumia chakula cha kinachosaidia kuongeza damu ama basi anapewa vidonge/dawa ya kuongeza damu na utahitajika kutumia kwa muda usiopungua miezi mitatu

Kiwango cha 4-7 na pungufu ya hapo basi daktari wako atashauriwa uongezewe damu papo hapo.

​

Ni vyakula gani vinavyosaidia kuongeza damu?

Mboga mboga za majani kama mchicha kwa wingi pamoja na kutumia dawa za kuongeza damu. Kwa ushauri zaidi wasiliana na daktari wako au kupitia namba za simu zilizo kwenye tovuti hii

​

Toleo 3

Imeboreshwa 10/2/2019, 23.02.2020

bottom of page