Imeandikwana daktari wa ULY CLINIC
​
Mkanda wa jeshi
Mkanda wa jeshi ni aina ya maambukizi yanayosababisha harara na vipele kwenye ngozi vyenye maumivu. Tatizo hili huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili na huonekana kama mkanda wenye vipele maji( vipele vyenye maji ndani) upande wa kulia au kushoto kwenye mwili wa binadamu.
​
Mkanda wa jeshi kwa jina jingine hufahamika kama Shingless na husababishwa na kirusi anayeitwa varicella zosta, kirusi ambaye anasababisha pia ugonjwa wa Tetekuwanga. Mara baada ya mtu kupata maambukizi ya kirusi huyu kwa mara ya kwanza na kupona, kirusi hujificha na kulala kama wamekufa kwenye ubongo na uti wa mgongo ambapo kuna kwenye mishipa ya fahamu.
Baadaye kirusi huweza kuamka na kuleta dalili ya mkanda wa jeshi unaopita kwenye mstari mshipa wa fahamu ulipopita.
Ugonjwa huu si wa kutishia amani yako, ila tu unasababisha maumivu na maumivu yanaweza kuwa makali kwa wakati mwingine. Kupewa chanjo dhidi ya kirusi huyu kunaweza kuzuia kupata ugonjwa huu, matibabu pia hufupisha tatizo la mkanda wa jeshi na kuzuia madhara yake yasitokee.
​
Dalili za mkanda wa jeshi, Visababishi, Vihatarishi, Madhara, Matibabu/pata tiba na chanjo