Moyo kufeli kufanya kazi (Heart failure and congestive heartfailure)
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
​
Moyo kushindwa kufanya kazi hudhuru karibia watu milion 6 huko amerika na watu 670,000 wanapata ugonjwa huu kila mwaka. Katika nchi zinazoendelea (mataifa mengi ya afrika) ugonjwa huu unazuka pia kwa kasi kubwa kwa sababu ya kubadilisha mfumo wa maisha na kupungua kwa kiwango kujishughulisha au mazoezi
Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure) haimaanishi moyo umesimama kufanya kazi yake ya kusukuma damu ila ina maana kwamba moyo unasukuma damu chini ya kiwango kinachohitajika kusukumwa kwa kila dakika. Kushindwa kufanya kazi kwa moyo husababisha damu kutembea kwa kiwango kidogo kwenye mishipa na kuongezeka kwa shinikizo la damu ndani ya moyo, matokeo yake ni kukosekana kwa hewa safi ya oksigeni na virutubisho sehemu mbalimbali za mwili ambavyo hupelekwa na damu. Kuongezeka kwa shinikizo ndani ya moyo husababisha moyo kutanuka, na ili kusukuma damu iliyojirundika nje ya moyo, moyo huhitaji kutumia nguvu nyingi sana, matokeo ya mda mrefu ya hali ni moyo kupata udhaifu na kushindwa kufanya kazi kabisa (moyo kufeli).
​
Kukosekana kwa oksijeni na virutubisho huamsha figo izalishe vichochezi vinavyo sababisha kutunza maji na chumvi mwilini, hii huletwa na kuwa kwa kiwango kidogo cha damu inayoingiwa kwenye figo hivyo maji huendelea kuzidi na moyo hushindwa kuya sukuma maji kwenda sehemu zingine za mwili kama damu. Matokeo ya haya yote ni kutuama kwa maji kwenye maeneo mbalimbali ya mwili kama mikononi, miguuni, kiwiko cha mkono, mapafu, na organi mbalimbali mwilini na kujaa kwa maji huitwa congestive heart failure
​
Dalili za mgonjwa wa moyo ulioshindwa kufanya kazi
Mtu anaweza asipate dalili yoyote, au dalili zinaweza kuwa sio kali sana au mtu anaweza kuwa na dalili mbaya. Kama dalili zitatokea zinaweza kuwa kati ya zifuatazo;
-
Maji kujaa kwenye mapafu
-
Maji kujaa kwenye mapafu kunaweza kusaabisha mtu kukosa pumzi ya kutosha anapokuwa anafanya mazoezi, wakati mwingine akiwa amepumzika na akiwa amelala chali kitandani. Wagonjwa hawa pia huweza kupata kikohozi kikavu na miruzi kwenye mapafu
-
-
Kutuwama kwa maji na chumvi mwilini.
-
Damu ikiwa kidogo inayoingia katika mishipa ya figo kutokana na moyo kushindwa kufanya kazi, Figo hutoa vichochezi vinavyo sababisha kutuwama kwa maji na chumvi ndani ya mwili. Maji yanapo ongezeka mwilini hujikusanya kwenye vifundo vya miguu, miguu, tumbo, hatimaye mtu huongezeka uzito. Dalili zinazoweza kutokea huwa pamoja na kukojoa sana wakati wa usiku, kukosa hamu ya kula au tumbo kujaa gesi na kichefuchefu
-
-
Kizunguzungu, kuchoka na uchovu
-
Haya yote hutokana na kiwango kidogo cha damu kinachoingia kwenye organi mbalimbali mwilini, kukiwa na kiwango kidogo cha damu kinachoingia kwenye ubongo basi mtu anaweza kupata kizunguzungu na kuchanganayikiwa pia.
-
-
Mapigo ya moyo kupiga kusiko kawaida
-
Moyo husukuma kwa haraka ili kuhakikisha damu inaenda sehemu za mwili na matokeo yake ni husababisha mapigo ya moyo kubadilika kwa kwenda kasi na mapigo yasiyo na utaratibu wa kawaida
-
Nini husababisha moyo kushindwa kufanya kazi-Heart failure?
Moyo kufeli kufanya kazi husababishwa na mambo mengi ambayo yanaharibu misuli ya moyo kama vile
-
Magonjwa ya mishipa inayolisha moyo-coronary heart disease
-
Magonjwa haya ya mishipa inayolisha moyo yaani kuipatia gesi ya oksigeni na virutubisho, hutokea kutokana na kuziba au tundu kuwa dogo kutokana na kuganda au migando na mafuta husababisha upungufu wa virutubisho na gesi ya oksigeni na hivyo sehemu ya misuli ya moyo huaribika na kufa
-
-
Shambulio la moyo la ghafla
-
Kushambuliwa kwa moyo kuna sababishwa na tatizo la kuziba ghafla kwa mishipa ya moyo kutokana na damu iliyoganda au mafuta yanaotembea kwenye mishipa ya damu inayolisha moyo na hivo hewa ya oksigen na virutubisho vinashindwa kufika maeneo fulani ya moyo na kuleta kufa kwa chembe sehemu hizo zilizokosa damu matokeo yake kushindwa kufanya kazi kwa sehemu iliyoharibika.
-
-
Moyo kufanya kazi zaidi ya kiwango
-
Hali zinazosababisha moyo kufanya kazi zaidi ya kiwango ni kama shinikizo la juu la damu, Magonjwa ya milango ya moyo, magonjwa ya tezi shingo(thyroid), magonjwa ya figo, kisukari, magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, haya yote kama mtu anayo anaweza kupata tatizo la moyo kufeli. Hata hivyo moyo kushindwa kufanya kazi kunaweza kutokea kama magonjwa sugu yakitokea kwa pamoja
-
​
Toleo la 2
Imeboreshwa8/12/2018