Matamshi (noo-troe-PEE-nee-uh)
Imeandikwa namadaktari wa uly clinic
Utangulizi
Ni kuwa na kiwango cha chini kuliko cha kawaida cha chembe za neutrophil- neutrophili ni seli zilizo mwilini zinazopambana na maradhi ya maambukizi ya bacteria.
Kwa watu wazima ili aweze semekana ana kiwango cha chini cha seli za neutrophili kiwango hicho kinatakiwa kuwa chini ya 1,500 kwa kila micro lita ya damu. Kwa watoto inategemea na umri wake.
Baadhi ya watu wamezaliwa na kukua wakiwa na chembe nyeupe za neutrophil kwa kiwango cha chini sana lakini hawapo katika hatari ya kupata mambukizi. Kwa watu kama hao upungufu huo/kiwangi hiki huwa hakina tatizo. Kiwango chini ya 1,000 ama chini cell 500 kwa kila micro lita siku zote huitwa Upungufu wa neutrophili, ambapo bacteria rafiki walio kwenye kinywa ama mfumo wa chakula wanaweza kukusabababishia maambukizi makali.
​
​
Dalili
-
Kuhisi mwili umechoka
-
Kuishiwa pumzi haraka wakati unaamka, au kufanya kazi
-
mapigo ya moyo kwenda kasi ama kupiga kusiko kawaida
-
Kufifia kwa rangi ya ngozi kuwa nyeupe(kwenye macho) ama viganya,na nyayo
-
maambukizi ya mara kwa mara, ama kutopona haraka
-
Kuchubuka kwa haraka au kusikoelezeka
-
Kutokwa damu puani ama kwenye fizi
-
Kutokwa damu kwa muda mrefu ukijikata
-
Harara kwenye ngozi
-
Kizunguzungu
​
Visababishi login kwa kutumia email kusoma zaidi hapa
​
Visababishi vya upungufu wa chembe za neutrophil
Madawa ya kutibu Saratani huongoza katika kusababisha kiwango cha chini cha neutrophil, watu wanaotumia dawa hizo huwa hatarini kupata maambukizi mbalimbali yakiwemo maambukizi ya bakteria kwa sababu ya upungufu wa kinga mwilini.
Pia ni vema kujua chembe za neutrophil huzalishwa ndani ya mifupa- kitu chochote kinachozuia uzalishaji wa neutrophil husababisha upungufu wa nutrophil
Visababishi vya moja kwa moja ni hivi
​
-
​Tatizo la kuzaliwa la upungufu uzalishaji wa neutrophil(kutokana na madhaifu ya uumbaji wa mtu)
-
Tatizo la kuzaliwa la Kushindwa kuingia kwa chembe za neutrophil kwenye mzunguko wa damu(myelokathexis) baada ya kuzalishwa kwenye mifupa
-
Saratani ya chembe nyeupe za damu
-
Myelofibrosis
-
Madawa ya saratani
-
Matibabu ya mionzi
-
Upungufu usio na sababu
​
Maambukizi pia huweza kusababisha upungufu wa chembe hizi kama vile;
​
-
Virusi vya homa ya ini aina A,B,C
-
Ugonjwa wa lymplogin kusoma zaidi hapa
-
Maambukizi ya bacteria aitwaye salmonella
-
Maambukizi yoyote kwenye mfumo wa damu
-
Maambukizi ya virusi kwenye mfumo wa damu
​
Hali ambazo zinaweza kuharibu chembe nyeupe za damu ni kama vile;
​
-
Baridi yabisi (ugonjwa wa maungio makubwa ya mwili)
-
Bandama kufanya kazi kupita kiasi
-
Aplastic anemia (kutozalishwa kwa chembe za damu)
-
Aplastic anemia ni tatizo ambalo hutokea pale ambapo mifupa inashindwa/inasimama kazi ya uzalishaji wa chembe nyeupe, nyekundu, na chembe zinazogandisha damu(platelets)
-
Tatizo hili huwa ni la nadra sana na huweza kutokea katika umri wowote ule, huweza kutokea kwa ghafla ama kwa taratibu na kuleta madhara taratibu kwa jinsi uzalishaji unavyopungua. Matibabu ya kutozalishwa kwa chembe hizo hujumuisha madawa, kuongezewa damu na kupandikizwa kwenye mifupa kwa chembe zenye uwezo wa kuzalisha damu kutoka kwa mtu mwingine
-
​
Visababishi
​
-
Mionzi na dawa za sararani
-
Sumu-kama madawa ya kuua mbu, na wadudu, kemikali ya benzene kwenye mafuta ya gari, tatizo linaweza kutoweka kama utajiepusha na kemikali hizi
-
Matumizi ya madawa- madawa kama yale yanayotumika kutibu baridi yabisi na baadhi ya madawa ya antibiotics huweza kusababisha
-
Magonjwa ya kujishambulia kwa mwili-
-
Maambukizi ya virusi
-
Ujauzito huwa na uhusiano matatizo ya mwili kujishambulia wenyewe
-
Sababu zisizojulikana- wagonjwa wengi wanaweza wasitambuliwe nini kinachosababisha upungufu wa chembe za damu.
​​
Kutozalishwa kwa chembe za damu huweza kuendelea taratibu ama haraka ndani ya wiki ama miezi, na huweza kutokea kwa ghafla. Tatizo linaweza kuwa sugu pia. Kutozalishwa kwa chembe za damu huweza kuwa hatari na kuua pia.
Vihatarishi
-
Tatizo hili ni nadra sana kutokea. Vitu vifuatavyo vinaweza kusababisha tatizo la kutozalishwa kwa chembe za damu
-
Kutibiwa kwa dozi kubwa ya mionzi au dawa za saratani
-
Kukaa karibu/kutumia sumu kama benzene nk
-
Matumizi ya baadhi ya dawa za kuua wadudu
-
Matumizi ya dawa tiba kama chloramphenicol na dawa za gold zinazotumika kutibu baridi yabisi
-
Magonjwa ya chembe za damu, magonjwa ya kujishambulia kwa mwili na maambukizi kwenye damu
-
Ujauzito, kwa nadra sana
-
Imeandaliwa na madaktari wa ULY-Clinic