Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic
Njia za kujifungua
Zipo njia mbili mama anaweza kuchagua endapo anataka kujifungua mtoto, hata hivyo uchaguzi wa njia ya kujifungua unaweza kuathiriwa na sababu mbalimbali ikiwa pamoja na uchaguzi wa mama au matatizo ya kiafya kati ya mtoto au mama. Njia ya upasuaji imekuwa maarufu sana katika karne ya 21 ambapo wanawake wengi wamekuwa wakichagua njia hii kwa sababu imeonekana kuwa ni salama na haina madhara. Licha ya njia hii kuwa maarufu kutokana na sababu mbalimbali, yapo madhara ambayo mtoto na au mama anaweza kuyapata kwa kujifungua kwa njia hii.
Katika makala hii utajifunza njia mbalimbali za kujifungua na faida zake.
1. Kujifungua kwa njia ya upasuaji
Kujifungua kwa upasaji ni njia mojawapo ya kujifungua kupitia uwazi mdogo unauchnwa na mikasi chini ya kitovu chako. Njia hii imerekodiwa kutumika kwa mara ya kwanza huko Swaziland miaka 1580 ambapo Jacob Nufer alimfanyia mkewe mara baada ya kuona hatua za uchungu haziendelei. Hata hivyo njia hii iliendelea kutumika kama njia ya kuwatoa watoto tumboni kwa wamama wajawazito waliofariki kabla ya kujifungua.
Maendeleo ya sayansi na kujifunza zaidi kuhusu upasuaji kwenye maiti na ugunduzi wa dawa za kupooza mwili katika karne ya 19, ilifanya wanasayansi waanze kufikiria na kutumia njia hii kuwa sehemu ya njia ya kujifungua.
Kabla ya kufanyiwa upasuaji huu wa tumbo la chini, utachomwa sindano ya ganzi iliusisikie maumivu katika eneo la tumbo kuelekea miguuni. Kwa njia hii unaweza kusikia mwanao akilia kwa mara ya kwanza mara baada ya kutoka. Aina ya kidonda kitakachowekwa inategemea n uchaguzi wa daktari, kovu linalokatwa kuelekea chini ya kitovu au kovu la fenestro linaweza kuchaguliwa na daktari wako. Si kila mtu atashauriwa kujifungua kwa njia hii endapo ilikuwa si uchaguzi wake, hata hivyo sababu zilizoorodheshwa hapa chini zitafanya ujifungue kwa njia ya upasuaji;
Sababu gani husababisha kujifungua kwa upasuaji?
Sababu kutoka kwa mtoto- mtoto kushindwa kuvumilia uchungu mrefu, matatizo ya kiuumbaji kwa mtoto yanayozuia kujifungua kwa njia ya uke, mlalo mbaya wa mtoto (kutanguliza matako, kutanguliza uso vibaya- baadhi), mapacha wawili au zaidi, mtoto mkubwa zaidi ya gramu 4500 kwa mwanamke mwenye kisukari au zaidi ya gramu 5000 kwa mwanamke asiye na kisukari.
Sababu za mama
Mama kuwa na kifafa cha mimba) au shinikizo linaloelekea kifafacha mimba, maoteo sehemu za siri, saratani ya shingo ya uzazi, kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.
Sababu za mama na mtoto
Kusimama kwa uchungu- Hutokea endapo uchungu hauendelea kama inavyotakiwa
Kondo na kitovu- kutangulia kwa kondo, kujipandikiza kwa kodno kwenye kuta za uzazi, kujiachia kwa kondo la nyuma kabla ya muda-, kutangulia kwa kitovu mbele ya kichwa cha mtoto, kitovu kujitokeza nje ya uke.
Nyonga- matatizo ya anatomia ya nyongo ya mama, uvimbe kwenye nyonga unaozuia mtoto kutoka(uvimbe kwenye kizazi n.k) historia ya uzazi wa hsida na jeraha wakati wa kujifungua(fistula, kuchanika kwa uke) historia ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga.
Mfuko wa uzazi- kupata makvu( kwa sababu ya kutoa mtoto, kutolewa sehemu ya kuta za uzazi, kutolewa kwa uvimbe wa fibroid zilizo ndani ya ukuta wa uzazi)
Madhara ya kujifungua kwa upasuaji
Ifahamike kuwa, kujifungua kwa njia ya upasuaji huwa ni moja ya upasuaji mkubwa unaohusisha kupewa dawa za usingizi na kuchanwa kwenye tumbo ili kukifikia kizazi na kutoa mtoto. Upasuaji huu una hatari sawa na hatari zingine zinazotokea kwa watu wanaojifungua kwa upasuaji.
Baadhi yamadhara ya muda mfupi ni;
-
Kupoteza damu nyingi
-
Kukaa hospitali kwa muda mrefu(mpaka siku 4)
-
Mama kuchelewa kupona na kurejea kwenye shughuli zake za kila siku
-
Kujeruhiswa kibofu cha mkojo utumbo(kupelekea fistula)
-
Kujeruhiwa kwa mtoto, majeraha ya kukatwa usoni au kwenye kiwiliwili chake
-
Maambukizi kwenye jeraha la upasuaji na kuachia kwa nyuzi
-
Madhara ya dawa za usingizi
-
Kuchelewa kunyonyesha mtoto au kuungana na mtoto mara baada ya kujifungua
-
Matatizo ya upumuaji kwa mtoto kama pumu ya kifua
-
Kupoteza maisha(kwa nadra)
Madhara za muda mrefu ya kujifungua kwa upasuaji
-
Kupata makovu kwenye ngozi ya tumbo
-
Maumivu ya tumbo la chini kutokana na makovu kwenye tumboni
-
Kovutia kwa tumbo kutokana na mwonekano wa makovu
-
Kujifungua kwa upasuaji mimba zinazofuata
Faida za kujifungua kwa upasuaji
Faida za kujifungua kwa njia hii zipo chache, zinategemea hali ya mama na mtoto. Faida huwepo pale endapo njia ya kawaida haiwezi fanya kazi, hivyo kujifungua kwa njia hii husaidia kumtoa mtoto na kumfanya asipate madhara ya kunwa maji au kuvuta kinyesi kwenye mapafu.
Faida zingine ni
-
Kutoongezeka kwa njia ya uzazi(uke) kwa sababu mtoto hapiti kwenye tundu la uzazi
2. Kujifungua kwa njia ya uke
Kujifungua kupitia tundu la uke ni njia ya kujifungua ambayo imekuwa ikitumika toka binadamu ameanza kupata mtoto. Njia hii ni nzuri endapo hakuna kipingamizi chochote kile kwenye njia ya uzazi kama vilivyoorodheshwa katika sababu ambazo zinasababisha mama ajifungue kwa njia ya upasuaji
Faida za kujifungua kwa njia ya uke
-
Utawahi kuruhusiwa kutoka hospitali. Ndani ya masaa 24 hadi 48
-
Utapasa mgusanao na mwanao punde baada ya kujifungua na utaweza kumnyonyesha mara
-
Mtoto anapokuwa anapita ukeni atapata mgandamizo kwenye kifua hivyo kusaidia kuondoa maji yaliyo kifuani na kufanya apumue vema na kupunguza hatari ya matatizo ya upumuaji
-
Mtoto anapopita kwenye tundu la uke huambukizwa bakteria wema ambao hufanya kinga za mwili za mtoto kukua na kumlinda mwanao dhidi ya magonjwa ya mfumo wa tumbo
Madhara ya kujifungua kwa njia ya uke
-
Mtoto anaweza kupata majeraha kiasi kama kuchanika kichwani kufunjika mfumo wa kola
Endapo utachagua kujifungua kwa njia ya uke, hakikisha unafahamu kuhusu uchungu, bonyeza hapa kujifunza kuhusu uchungu
Imeboreshwa 02.03.2021
ULY Clinic inakushauri siku zote wasiliana na daktari wako kabla ya kuchuku hatua yoyote ile inayohusu afya yako.
Rejea za mada hii;
-
How didi C-section begun. https://www.birthinjuryguide.org/2018/05/how-c-sections-begin. Imechukuliwa 12.09.2020
-
Caesarian section history. https://www.news-medical.net/health/Cesarean-Section-History.aspx. Imechukuliwa 12.09.2020
-
Giving birth by vaginal. https://www.whattoexpect.com/pregnancy/labor-and-delivery/vaginal-birth/. Imechukuliwa 12.09.2020
-
What to expect during a vaginal delivery. https://www.healthline.com/health/pregnancy/intrapartum-care-vaginal-delivery. Imechukuliwa 12.09.2020
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
-
Kijifungua kwa njia ya kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji ujauzito uliopita
-
Huduma za kliniki wakati wa ujauzito
-
Namna ya Kujua tarehe ya kujifungua