top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

ULY CLINIC

Jumamosi, 12 Agosti 2023

Ugonjwa wa PID

Ugonjwa wa PID

PID ni ugonjwa unaotokea sana kwa wanawake waliowahi kuathiriwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa. Asilimia kubwa husababishwa na vimelea vya gonorrhea na chlamydia (wanaosababisha kisonono na pangusa). Ugonjwa huu huweza kubabisha tatizo la kutopata mimba, kati ya wanawake 8 walio ugonjwa huu mwanamke 1 huweza kupata ugumba.

 

Mara baada ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa na kutotibiwa , vimelea hawa hupanda katika mfulko wa kizazi na hatimaye kufikia katika mirija ya uzazi, wanapokuwa katika mfumo wa kizazi kinga ya mwili huamka kupambana nao. kemikali mbalimbali hutolewa kutokana na mpambano huo na ikiwa ugonjwa umekaa kwa mda mrefu basi kemikali hizi zinazotolewa huharibu kuta za mfuko wa kizazi na kusababisha michomo na mishikamao ya ukuta wa uzazi, mirija ya mayai na viungo vingine vilivyo kwenye uzazi na hivo inasababisha kuwa vigumu kwa mimba kutungwa au kukua katika kuta hizo

 

Je ni kwa jinsi gani mtu anapata maambukizi haya?

Kwa sababu ugonjwa huu ni matokeo ya kutotibiwa kwa magonjwa ya zinaa(sexually transmitted infection) basi njia zinazomuweka mtu hatarini ni kushiriki tendo la ndoa na mtu aliyeathirika na vimelea hivo. Mambo yafuatayo yanaweza kumweka mwanamke hatarini zaidi

 

  • Kupata na kutotibiwa kwa magonjwa ya zinaa

  • kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

  • Kuwa na mpenzi mwenye wapenzi wengi

  • Kuwa na historia ya ugonjwa huu kabla ya sasa

  • Kujisafisha kwenye kuma kwa maji au vidole

  • Kutumia uzazi wa mpango hasa kwa kuwekewa vifaa kwenye kizazi

 

Jinsi gani unaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa huu

Njia pekee ya kuondokana na ugonjwa huu ni kuacha kufanya ngono zembe, ngono kwa njia ya mdomo na mkunduni ni vihatarishi oia vya kupata ugonjwa huu. Endapo umepata mpenzi basi ni vema mkapima na kuangalia kama anamaabukizi ya ugonjwa huu atibiwe kwanza au tumia kondomu unaposhiriki tendo la ndoa.Pia punguza mtandao kwa kuwa na mpenzi mmoja tu mwaminifu aliyepima unaweza kujikinga na ugonjwa huu.

 

Dalili za PID ni zipi?

Mwanamke anaweza asijitambue kwamba anaugonjwa huu kwa sababu unaweza usiwe na dalili au dalili zinajionesha kidogo sana na hivo kwa kuchukuliwa historia na dakitari pamoja na uchunguzi wa awali (physical examination) na vipimo vingine unaweza kujulikana kama umeathilika na ugonjwa huu. Ikiwa dalili zipo basi unaweza kuwa na dalili kati ya zifuatazo;

  • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

  • Homa (lakini hutokea kwa mtu mwenye maaambukizi ya awali, ugonjwa ukiwa sugu mgonjwa huwa hapati dalili hii)

  • Uchafu usio wa kawaida kutoka ukeni na hutoa harufu mbaya

  • Maumivu au kutokwa damu wakati wa tendo la ndoa

  • Hisia za kuungua wakati wa kukojoa

  • Kutokwa na damu katikati ya kipindi cha hedhi

 

Je yapo matibabu ya ugonjwa huu?

Ndio yapo matibabu ya ugonjwa huu, matibabu huwa mazuri endapo ugonjwa utatibiwa mapema. Mara utapoanza matibabu dalili zinaweza kutoweka lakini unatakiwa kumaliza dozi uliyopewa. Madhara yaliyosababishwa na ugonjwa huu kwenye kizazi huwa hayaondoki na mtu anapochelewa matibabu madhara yanaendelea kuwa makubwa kama kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai na kuleta makovu katika kizazi

 

Madhara mengine yatokanayo na ugonjwa huu ni yapi?

Madhara makubwa yatokanayo na ugonjwa huu ni

  • Kufanyika kwa makovu nnje na ndani ya kizazi yanayosababisha kuziba kwa mirija ya uzazi

  • Mimba kutunga nnje ya kizaziectopic pregnancy)

  • Ugumba (infetility)

  • Maumivu sugu ya tumbo chini ya kitovu /maumivu yasiyoisha

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

12 Agosti 2023, 17:06:13

Rejea za mada hii:

1. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). Pelvic Inflammatory Disease. ACOG Patient Education Pamphlet, 1999.

2. Westrom L and Eschenbach D. In: K. Holmes, P. Sparling, P. Mardh et al (eds). Sexually Transmitted Diseases, 3rd Edition. New York: McGraw-Hill, 1999, 783-809.

bottom of page