top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

20 Novemba 2024, 08:13:20

Image-empty-state.png

Pombe na ujauzito

Je matumizi ya pombe wakati wa ujauzito yana umuhimu?


Kuacha matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata madhaifu ya kuzaliwa kwa kichanga na matatizo kadhaa yanayoweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito.


Madhara haya ya pombe huweza kuathiri akili ya mtoto na kupelekea uwezo duni wa mtoto kujitambua na dalili zingine ambazo huashiria Mtoto chapombe au Mtoto pombe. Kutokana na Shirika la Afya Duniani, madhara ya pombe yanayoambatana na dalili na viashiria fulani yanaongezeka sana. Pombe imekuwa ikitumiwa vibaya sana wakati wa ujauzito ukilinganisha na dawa zingine za kulevya.

Dalili za mtoto ambaye mama alikuwa akitumia pombe kwa kiasi kikubwa

Dalili hizi hufahamika pia kama dalili za mtoto chapombe.

  • Udumavu (kutokuwa vema kabla na baada ya kuzaliwa)

  • Mtindio wa ubongo

  • Udhaifu wa kuzaliwa wa kichwa na uso

  • Magonjwa ya moyo

  • Tabia zisizoeleweka

  • Matatizo ya mfumo wa fahamu

Kiasi gani cha pombe ni salama kwenye ujauzito?

Hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe kwenye ujauzito kinachotambulika. Ili kulinda usalama wa mtoto ni kutofikiri kutumia pombe kabisa wakati wa ujauzito ama miezi michache unapofikiria kuwa mjamzito.

Je kuna uhusiano wa kiwango cha pombe na matokea mabaya kwa mtoto?

NDIO. Miongoni mwa wanawake waliokunywa pombe nusu glasi ya pombe kila siku, 1/3 ya watoto walikuwa chapombe, 1/3 walionyesha madhara ya usumu ya pombe kabla ya kujifungua, na 1/3 waliobaki walikuwa kawaida. Kundi jingine lililotumia mililita 30 hadi 70 za pombe kila siku, asilimia 10 ya watoto walikuwa na dalili za mtoto chapombe, hivyo hata kiwango kidogo cha pombe kimekuwa kikisababisha tatizo la mtoto chapombe . Matumizi ya pombe kwa kiasi kidogo bado yamekuwa yakihusika kusababisha mtoto kuwa na IQ kidogo na matatizo ya kujifunza kwa watoto wenye anatomia ya kawaida.


Je pombe husafilishwa kwenye kitovu cha mtoto akiwa tumboni?

Kemikali ya ethyl iliyo kwenye pombe hupita kwenye kitovu cha mtoto na kuingia kwa kwenye mzunguko wa damu wa mtoto. Kiwango cha pombe kwenye damu ya mama huwa sawa na kile kwenye damu ya kichanga.


Je mama chapombe anatakiwa aache kunywa pombe?

Mama aliyekuwa teja wa pombe (chapombe) anatakiwa apewe msaada wa wataalamu ili kusaidiwa kuacha pombe, madhara ya kujifungua kabla ya muda huongezeka kwa watumiaji wa pombe.

Dalili za kuacha pombe ghafla hutokea wakati gani wa ujauzito?

Dalili za kukatisha matumizi ya pombe huanza kuonekana mapema pale mtu anapoacha kutumia pombe, mara nyingi ndani ya masaa 4 hadi 12. Hata hivyo inawezekana dalili za kuacha kutumia pombe kuonekana siku chache baadae.


Mtu asipopata tiba hufikia kilele cha dalili ndani ya masaa 48 na zinaweza kuendelea kwa miezi 3 hadi 6, wakati huu huwa kuliko awali. Dalili na viashiria vinavyoonekana hujumuisha kutetemeka, wasiwasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, shinikizo la damu la juu, kutokwa jasho, kichefuchefu, kukosa usingizi na hutegemea utegemezi wa pombe na hali ya mgonjwa.


Mara ujauzito unapotambuliwa kuacha kutumia ama kupunguza husaidia kuondoa madhara kwa mtoto?

Kemikali ya ethyl na ethanol iliyo kwenye pombe hupita kwenye kitovu na kuingia kwenye damu na ubongo wa mtoto. Inafikirika kwamba madhara hutokana na sumu iliyo kwenye pombe na mazao ya uchakataji wa pombe mwilini. Kuacha au kupunguza kutumia pombe mara ujauzito unapotambuliwa huweza kupunguza matatizo ya kuzaliwa kwa mtoto hata hivyo kuna uwezekanowa kutotokea kwa madhara. Hivyo tafiti zaidi zinatakiwa kufanyika ili kuonyesha usahihi wa jambo hili.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

20 Novemba 2024, 08:27:36

Rejea za dawa

  1. Bailey BA, et al. Prenatal alcohol exposure and miscarriage, stillbirth, preterm delivery, and sudden infant death syndrome. Alcohol Res Health 2011;34:86–91.

  2. Denny CH, et al. Trends in alcohol use among pregnant women in the U.S., 2011–2018. Am J Prev Med 2020;59:768–9. 10.1016/j.amepre.2020.05.017 [DOI]

  3. National Council for Mental Wellbeing. Substance use disorders and the person-centered healthcare home. Washington, DC; 2010. https://www.thenationalcouncil.org/wp-content/uploads/2020/01/National_Council_SU_Report.pdf?daf=375ateTbd56

  4. Denny CH, et al. Consumption of alcohol beverages and binge drinking among pregnant women aged 18–44 years—United States, 2015–2017. MMWR Morb Mortal Wkly Rep 2019;68:365–8. 10.15585/mmwr.mm6816a1 [DOI]

  5. Barbosa C, et al, Dowd WN. Alcohol consumption in response to the COVID-19 pandemic in the United States. J Addict Med 2021;15:341–4. 10.1097/ADM.0000000000000767 [DOI]

bottom of page