Je naugua mafua ya aleji au kirusi cha influenza?
Mafua ni ugonjwa unaowapata watu wengi sana duniani, hutokea kwenye umri wowote ule kama watoto watu wazima na wazee. Baadhi ya watu aina Fulani huweza kupata dalili kali na madhara makubwa kutokana na mafua. Makala hii imejikita kutofautisha mafua ya virusi na mafua ya aleji ili kusaidia kufahamu na kuchukua hatua za matibabu mara unapougua;
Dalili
Mafua ya virusi huwa na dalili gani
Mafua ya kirusi cha Infuenza huwa na dalili ambazo ni
Homa ya ghafla na kutetemeka
Misuli kuuma na maungio ya mwili
Maumivu ya kichwa
Uchovu mkali sana wa mwili
Kuziba kwa pua na kuchuruzika kwa mafua
Hisia za kuwa na homa
Mafua ya aleji huwa na dalili za
Kutokuwa na homa
Kuziba kwa pua
Kuchuruzika kwa mafua kutoka puani yenye rangi nyeupe membamba na yenye kunata
Visababishi
Mafua ya virusi husababishwa na virusi na husambazwa kwa njia ya;
Matone ya majimaji kutoka kwenye chafya au makohozi ya mtu mwenye mafua.
Mafua ya aleji husababishwa na
Vumbi la miili ya mende, kunguni, vumbi la wanyama na poleni za maua
Kuonekana kwa dalili
Mafua ya virusi
Dalili za mafua ya virusi huonekana ghafla na hudumu kwa wiki moja angalau
Mafua ya aleji
Huonekana wiki kadhaa hadi miezi na hutegemea mtu amekaa kwa muda gani kwenye viamsha aleji
Kinga
Mafua ya virusi
Kinga yake ni kuchomwa chanjo ya kirusi cha influenza
Mafua ya aleji
Kinga ya mafua haya ni kuepuka viamsha aleji au kufanya mambo yafuatayo
Kusafisha kapeti au kuondoa kapeti ndani ili kupunguza vumbi na uchafu wa wadudu kama mende n.k
Kutumia AC ili kupunguza vumbi la fangasi ndani ya nyumba
Matibabu
Mafua ya virusi
Watu hupona mara nyingi bila matibabu
Kupumzika, kunywa maji ya kutosha na matumizi ya panado kupunguza homa kwa wagonjwa wenye dalili kali
Kujifukiza ili kuzibua pua endapo umeshauriwa na daktari wako kunaweza saidia dalili zisiwe kali
Mafua ya aleji
Hutibiwa kwa matumizi ya dawa za kuweka kwenye pua
Matumizi ya dawa jamii ya antihistamine
Matumizi ya dawa za kuzibua pua
Kijifukiza ili kuzibua pua endapo umeshauriwa na daktari wako
Soma zaidi kuhusu mafua ya aleji au mafua ya virusi na tatizo la kupiga chafya mara kwa mara kwa kubonyeza mada husika
Rejea za mada hii
https://journals.lww.com/tnpj/Citation/2008/09000/Diagnosing_Rhinitis__Viral_and_Allergic.5.aspx#. Imechukuliwa 12.11.2020
Flue vaccine safety information. https://www.cdc.gov/flu/prevent/general.htm. Imechukuliwa 12.11.2020
Cold, flue or allergy. https://newsinhealth.nih.gov/2014/10/cold-flu-or-allergy. Imechukuliwa 12.11.2020
Can allergies cause a fever?. https://www.medicalnewstoday.com/articles/321502. Imechukuliwa 12.11.2020
Comments