top of page
Writer's pictureDr.Sospeter Mangwella, MD

Chakula Huzuia Vimbe za Fibroid ndani ya Ukuta wa Uzazi

Updated: Feb 10, 2019


Vyakula gani huzuia au hupunguza ukuaji wa fibroids?


Fibroids ni vimbe ndani ya ukuta wa uzazi ambao hukua kwa kutegemea uzalishwaji wa vichechezi mwili vya oestrogen na progesterone, vimbe hizi hutokea sana kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 35-45. Mwili ukiwa unazalisha kwa wingi vichochezi hivi basi Vimbe hizi hukua haraka na kusababisha matatizo. Mwanamke ambaye mzunguko wake wa hedhi unaelekea kukoma--koma hedhi (kufikia mwisho-kuanzia miaka 45 na kuendelea) endapo alikuwa na vimbe hizi basi hupotea kwa sababu vichochezi hivyo huwa vipo kwa kiwango kidogo sana kuweza kukuza Vimbe hizo.


Vichochezi hivi hutengenezwa kutoka kwenye vitu gani?


Vichochezi hivi hutengenezwa kwa kutegemeana na wingi wa mafuta mwilini mwako, hivo vyakula vyote vinavyoongeza mafuta mwilini vinamchango wa kutengeneza hormoni hizo na endapo matumizi ya mafuta yanakua makubwa basi Vimbe hizi pia hukua kwa haraka.


Nini cha kufanya?


Kula vyakula visivyo vya kusindikwa

  • Vyakula vingi vya kusindikwa huwa na kemikali zinazochochea ukuaji wa vimbe na huweza kuchochea ukuaji wa Vimbe/Fibroids. Vyakula vya asilia kama matunda na mboga mboga huwa hazina madhara kama vyakula vya kusindikwa.

  • Ulaji wa nyama nyekundu huhusika pia na ukuaji wa vimbe hizi kwa kuwa nazo huchangia utengenezaji wa vichochezi mwili vya estrogen

  • Kula vyakula vya mbegu kama mbegu za mimea jamii ya kunde kama vile kunde maharage, soya, na vyakula vya soya visivyo chachushwa ambavyo huwa na kiwango kikubwa cha hormoni za estrogeni

  • Jaribu kutumia dawa za mitishamba kusinyaza Vimbe hizi; ingawa hakuna utafiti wa kisayansi wa kuonesha kwamba miti shamba huzuia /kupunguza vimbe hizi lakini inapendeza endapo utatumia dawa hizo ambazo zinaonekana kupunguza wingi na uzalishaji wa hormoni aina ya estrogeni inayo chochea kukua kwa vimbe /fibroids.

  • Tumia Juisi ya zabibu

  • Kula Vyakula vya omega 3 kwa wingi kama samaki aina ya sangara (tilapia) n.k (ingia katika blog ya website hii usome kuhusu mafuta ya omega 3)

  • Pia jaribu kupunguza uzito kwa sababu uzito mkubwa huendana na kiwango cha mafuta mwilini na mafuta haya huchangia kwenye utengenezaji wa hormoni za estrogen

Je unajua kuna dawa asilia pia zinaweza kusinyaza vimbe za fibroid? Wasiliana na daktari wako au ma Daktari wa uly clinic kupitia namba zilizo chini ya tovuti hii

175 views0 comments

Recent Posts

See All

Commentaires


bottom of page