Mjamzito huanza kuhisi mtoto akicheza tumboni kuanzia wiki ya 16 hadi 20, hata hivyo baadhi ya wanawake huwahi au kuchelewa kuhisi tofauti na wiki hizi.
Dalili za kucheza kwa mtoto tumboni huweza kuchanganywa na mijongeo mbalimbali katika tumbo hivyo wajawazito wengi hushindwa kutambua katika wiki za mwanzo za ujauzito.
Kucheza kwa mtoto tumboni ni ishara muhimu inayoonesha kuwa mtoto yu hai na mwenye afya njema.
Dalili za mtoto kucheza tumboni
Wajawazito hueleza kuwa hisia za mtoto kucheza tumboni huweza kuelezewa kwa namna zifuatazo;
Mjongeo mithili ya kuogelea kwa kitu tumboni
Mijongeo mithili ya kutembea kwa kitu tumboni
Mijongeo mithili ya mpwito
Mijongeo mithili ya mdundo
Mijongeo halisi ya miguu na mikono ya mtoto katika hatua za mwisho za ujauzito
Nini unapaswa kufahamu zaidi kuhusu dalili za mtoto kucheza tumboni?
Kucheza kwa mtoto tumboni ni ishara muhimu inayoonesha kuwa mtoto yu hai na mwenye afya njema.
Endapo hauhisi mijengeo ya mtoto au imepungua kasi fika katika kituo cha huduma za afya kwa uchunguzi zaidi.
Rejea za mada
Fetal Movement – When You feel Baby kick.webmd.com. https://www.webmd.com/baby/fetal-movement-feeling-baby-kick. imechukuliwa 03.07.2023
How does it feel when a baby moves during pregnancy? Medical news today. https://www.medicalnewstoday.com/articles/what-does-it-feel-like-when-baby-moves. imechukuliwa 03.07.2023
Common Pregnancy Complaintsand Questions. Medscapehttps://emedicine.medscape.com/article/259724-overview#a1. imechukuliwa 03.07.2023
Comments