top of page
Writer's pictureDr. Benjamin Lugonda, MD

Dawa-kinga ya UKIMWI

Updated: Nov 6, 2021

Je, kuna kinga ya maambukizi ya UKIMWI?


UKIMWI ni kifupisho cha Upungufu wa KInga MWIlini, hutokea miaka kadhaa baada ya maambukizi ya VVU au Virusi Vya Ukimwi . makala hii imeandikwa mahususi kujibu swali la kuhusu kinga ya UKIMWI.


Je kuna kinga ya UKIMWI?


NDIO kuna dawa zinazoweza kukukunga kupata maambukizi ya VVU zinafahamika toka miaka ya 2004 kinga hizi ni vidonge vya dawa vinavyofahamika kama PEP na PrEP


PEP ni nini?


Katika mada hii, PEP ni kifupi cha neno tiba Post Exposure Prophylaxis, ikiwa ina maana ni dawa ya kukinga kupata maradhi baada ya kukutana na kihatarishi. PEP hutengenezwa na dawa zinazotumika katika kudhoofisha maambukizi ya VVU kwa jina la ARV'S


Kwa Tanzania PEP hutumika kwa wafanyakazi wa afya mfano waliojichoma sindano ya mgonjwa mwenye VVU n.k, watu waliobakwa na makundi mengine.


Soma zaidi kuhusu PEP, kina nani wanatakiwa tumia PEP na inatumikaje kwa kubonyeza hapa.


PrEP ni nini?


Umeshawahi waza kwenda kushiriki ngono na mwathirika wa VVU?


PrEP ni kundi la dawa zenye uwezo wa kukukinga dhidi ya maambukizi ya chanzo cha VVU kinachofahamika na ni miongoni mwa za kudhoofisha makali ya VVU mwilini yaani ARV’S.


Baadhi ya dawa za PrEP ni zipi?


Dawa za PrEP zinazofahamika ni

  • Truvada huundwa na mchanganyiko wa Tenofovir disoproxil fumarate and Emtricitabine (Truvada)

  • Descovy huundwa na mchanganyiko wa Tenofovir alafenamide and Emtricitabine

  • Truvada na Descovey hutumika kama kinga ya VVU kwa watu wasio na VVU wanaoedna kushiriki ngono na mwathirika wa VVU, descovey pia hutumika kukinga maambukizi ya VVU kwa wale wanaoshiriki matumizi ya sindano ya dawa za kulevya kwa kuchoma kwenye mishipa ya damu.


Ni wakati gani ushiriki ngono baada ya kutumia PrEP?


Kuna aina mbili za matumizi, unaweza kutumia kila siku au kutumia wakati unataka kwenda kushiriki ngono.


Matumizi ya kila siku

  • Kwa kushiriki ngono ya uke kwa uume au ume kwa uke au kushiriki sindano za madawa ya kulevya utahitajika kutumia PrEP kwa siku 21 ili iweze dawa ifikie kiwango chake cha juu kabisha kukukinga na maambukizi

  • Endapo unashiriki ngono ya uume kwa njia ya haja kubwa utahitaji kutumia kwa siku 7 ili dawa ifikie uwezo wake wa juu kabisa kabla ya kushiriki ngono


Matumizi wakati wa mahitaji


PrEP huweza kutumika wakati unahitaji mfano mpango wa matumizi wa 2-1-1 hutumika kwa watu ambao wanaoenda kushiriki ngono na mwathirika wa VVU ambao unatumia vidonge viwili (2) masaa 2-24 kabla ya kwenda kushiriki ngono, baada ya hapo utatumia kidonge kimoja (1) masaa 24 toka umekunywa dozi ya kwanza na kisha utatumia kidonge kimoja(1) masaa 24 baada ya kunywa dozi ya pili


Kumbuka: PrEP huwa haitumiki kama mbadala wa PEP


Je, PrEP inauhakika wa kukinga maambukizi ya VVU?


NDIO, endapo utatumia PrEP ipasavyo kama ulivyoelekezwa na mtaalamu wa afya, dawa zitakukinga kupata maambukizi kwa asilimia 99.


Je, PEP inauhakika wa kukinga maambukizi ya VVU?


Hakuna tafiti zinazoonyesha uwezo wa PEP kwa asilimia dhidi ya kukinga maambukizi ya VVU, hata hivyo endapo utatumia dawa kwa jinsi ulivyoelekezwa na ndani ya masaa 72, PEP ina uwezo wa kukukinga kupata maambukizi ya VVU hata hivyo si kwa asilimia 100.


Unapokuwa unaendelea kutumia PEP hakikisha unatumia njia zingine za kukukinga na maambukizi ya UKIMWI. Soma zaidi kwa kubonyeza hapa


Maudhi ya dawa za PEP na PrEP ni yapi?


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hizi na ambayo hupotea baada ya siku kadhaa kupita ni

  • Kuharisha

  • Kichefuchefu na kutapika

  • Uchovu mkali wa mwili

  • Maumivu ya tumbo

  • Maumivu ya kichwa

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.


Rejea za mada hii

  1. CDC. About PEP. CDC. https://www.cdc.gov/hiv/basics/pep/about-pep.html. Imechukuliwa 24.11.2020

  2. CDC. On demand PrEP. CDC. https://www.cdc.gov/hiv/basics/prep/prep-effectiveness.html. Imechukuliwa 24.11.2020

  3. WHO. Post-exposure prophylaxis. https://www.who.int/hiv/topics/prophylaxis/en. Imechukuliwa 24.11.2020

  4. ULYCLINIC. Dawa za PEP. https://www.ulyclinic.com/dawa-pep.Imechukuliwa 24.11.2020

  5. HIV gov. https://www.hiv.gov/hiv-basics/hiv-prevention/using-hiv-medication-to-reduce-risk/pre-exposure-prophylaxis. Imechukuliwa 24.11.2020

  6. ULY CLINIC. UKIMWI. https://www.ulyclinic.com/ukimwi. Imechukuliwa 24.11.2020

1,785 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentários


bottom of page