Je hali yako ya rhesus ni nini
Mama anapoenda hosptali kwa mara ya kwanza kabisa anapokuwa mjamzito hupata fursa ya kupima vipimo mbalimbali kama wingi wa damu , kundi la damu( A,B, AB au O) na hali yake ya rhesus yaani rhesus (positive ama Negative) chanya ama hasi
Rhesus hurithiwa na hutengenezwa na vinasaba. Vinasaba hivi hutengeneza protini inayoitwa D antigen. Ukiwa ni rhesus chanya(+) maana yake ni kwamba unayo protini hiyo katika chembe zako nyekundu za damu na ukiwa rhesus hasi(-) maan yake hauna protin hiyo kwenye damu
Watu wengi duniani huwa ni rhesus chanya
Ni vip hali yako ya rhesus inamdhuru mtoto?
Madhara kwa mtoto yanatokea endapo mama ni rhesus negative tu na anabeba mtoto ambaye ni rhesus positive, mtoto huyu hurithi rhesus chanya kutoka kwa baba yake.
Kama damu ya mtoto itagusana na ya mama wakati wa kujifungua, kinga yako ya mwili(mama) itaamsha chembe hai za ulizi dhidi ya damu ya mtoto na itaweka kumbukumbu ili kufanya mashambulizi baadae endapo mama atabeba mimba nyingine ya mtoto mwenye rhesus chanya, lulinzi huo hukaa mwilini kwa mda mrefu sana na hutunza kumbukumbu. Kwa mimba ya kwanza mama atajifungua vema tu
Mama atakapopata ujauzito mwingine basi chembe hizi na chemikali hizo hupita katika kondo la mama na kuingia kwa mtoto na kumshambulia hatimaye kufa kama asipopata matibabu haraka. Mambo haya hutokea kwa sababu mtoto anaonekana kama kitu kigeni katika mwili wa mama
Hivyo wamama wengi wenye tatizo hili huwa na historia ya kuwa na mtoto mmoja na mimba zinazofuata zote mtoto hufia tumboni
soma zaidi kwenye website yetu bonyeza hapa
Kommentare