Miguu kuwaka moto
Ni hali ya kuhisi miguu kuwa ya moto na inauma, hali hii huweza kuwa ya maumivu madogo au makali na wakati mwingine unaweza ukakosa usingizi kabisa wakati wa usiku kwa sababu ya maumivu. Baadhi ya visababishi vya miguu kuwaka moto huweza kuambatana na moja kuhisi miguu inachoma kama sindano au mwiba na mbili kupata ganzi au vyote viwili.
Ingawa uchovu au maambukizi kwenye ngozi huweza kusababisha miguu kuwaka moto kwa mda mfupi na kubadilika mwonekano wake wa kawaida(rangi), kuumia kwa mishipa ya fahamu ya neva huwa ni sababu kuu ya kusababisha miguu kuwaka moto.
Kuumia kwa neva huweza kusababishwa na mambo mbalimbali kama kisukari, ulevi wa pombe wa kupindukia, sumu aina Fulani, upungufu wa madini na vitamin (vitamin B), au maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Vifuatavyo ni visababishi vya miguu kuwaka moto kwa undani zaidi;
Visababishi vya miguu kuwaka moto ni
Ulevi wa kupindukia(pombe)-( ugonjwa wa kutumia pombe)
Ugonjwa wa Charcot marie tooth
Kutumia dawa za kutibu saratani
magonjwa sugu ya figo
Udhaifu wa mishipa ya neva
Matumizi ya madawa
Ugonjwa wa mishipa ya fahamu kutokana na kisukari
Upungufu wa homoni ya tezi shingo
Upungufu wa vitamin mwilini(kama vile vitamin B)
Wakati gani umwone daktari?
Mwone daktari endapo
Maumivu ya miguu yamekuja ghafla
Maumivu hayo hayaishi licha ya kujipatia tiba nyumbani
Kama unakidonda mguuni ambacho kina dalili ya kupata maambukizi
Kama unapoteza fahamu kwenye miguu
Au endapo maumivu yanaendelea kupanda juu zaidi.
Matibabu ya miguu kuwaka moto
Matibabu ya miguu kuwaka moto hutegemea visababishi, kila kisababishi kina aina yake ya matibabu. Kitu cha kwanza kabisa ni kufahamu nini kilichosababisha maumivu hayo ili uweze kupata matibabu sahihi. Utahitaji kuchukuliwa historia ya tatizo lako na kufanyiwa vipimo hospitali ili kutambua kisababishi kipi haswa kinachosabaisha miguu yako kuwaka moto.Endapo unahitaji kujua zaidi kuhusu matibabu husika basi endelea kusoma kwenye kila kipengele cha visababishi.
Comments