top of page
Writer's pictureDr. Benjamin Lugonda, MD

Hadithi maarufu kuhusu Visababishi vya saratani


Imeandikwana madaktari wa uly clinic

Hadithi na misemo ya kuogofya inasambaa kwenye mitandao kuhusu visababishi vya saratani kwa binadamu, hasa kuhusu dawa za kuzuia kwapa kutoa jasho, kula sukari nyingi husababisha saratani. Watu wamekuwa wakiogopa sana kuhusu hadithi hizi na kusababisha wajizuie na matumizi ya vitu hivi

Kwenye sehemu hii tumezungumzia baadhi ya imani hizi ambazo zinaenea na kukanusha kwa kutumia maelezo ya sayansi na tafiti mbalimbali zilizofanywa na zinazofanyika

Hadithi. Dawa mafuta ya kwapa(deodorant) husababisha saratani ya chuchu/maziwa

Ukweli.Hakuna ushahidi wa kisayansi unaotoa jibu kuwa matumizi ya mafuta ya kuzuia kwapa kutoa jasho husababisha saratani ya chuchu au maziwa, hii ni kutokana na maelezo ya shirika la tafiti la National cancer institute na mashirika mengine yanayofanya tafiti

Baadhi ya taarifa zinasema kwamba deodorant huwa na kemikali sumu aina ya alumiam ambayo huweza kufyonzwa kwenye kwapa au chuchu haswa wakati wa kunyoa kwapa na hivyo kuweza kusababisha saratani. Maelezo haya hayajafanyiwa utafiti zaidi na kuja najibu la uhakika kwamba mafuta ya kuzuia kwapa kutoa jasho husababisha saratani.

Watu wenye saratani hawatakiwi kula sukari, kwa sababu sukari husababisha saratani kukua haraka

Ukweli. Sukari haifanyi saratani ikue haraka, kila seli ya binadamu inahitaji sukari ili iweze kukua na kuendesha shughuli zake ikiwa pamoja na seli za saratani. Kuwepo kwa sukari nyingi kwenye seli haimaanishi husababisha seli hizo kukua haraka au kusambaa. Kinyume chake ni kweli pia kuunyima mwili sukari hakufanyi saratani isikuwe na kusambaa.

Huu uvumi umetokana na kipimo kinachoitwa PET ambacho hutumia aina Fulani ya mionzi sukari, ili kuangalia chembe ambazo zina saratani. Chembe zenye saratani hufyonza kwa wingi sukari aina hii kwa sababu hutumia nguvu nyingi. Hapa ndipo wataalamu wengi wamejichanganya kwa kusema seli za saratani zinapenda sukari, ukweli ni kwamba seri za saratani zinahitaji nguvu nyingi kwa sababu zinakuwa haraka na hivyo hufyonza sukari hiyo kwa wingi.

Ingawa kuna ushahidi kutoka kwenye tafiti kwamba kula sukari kwa wingi kunaweza kusababisha saratani kama saratani ya mrija wa kimeleo cha chakula(oesophagus). Sukari nyingi pia huweza sababisha mtu kuongezeka uzito na kumletea kihatarishi cha magonjwa ya kisukari na mishipa ya damu kwenye moyo ambapo mtu mwenye kisukari anahatari ya kupata aina Fulani za saratani.

Hadithi. Watu wema hawapati saratani

Ukweli. Watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na saratani na hawajatenda mabaya, ingekuwa watoto wanazaliwa wakiwa hawana saratani na wanapata tu wakishaanza kutenda mabaya basi usemi huu ungekuwa wa ukweli. Kimsingi ni kwamba saratani inaweza kutokea kwa mtu yeyote awe mkubwa au mdogo au kichanga, na awe anatenda mema au mabaya.

Hadhithi- Saratani inaambukizwa

Ukweli- Saratani haiambukizwi kwa kumshika mtu, unaweza kukaa na mgonjwa wa saratani na usipate saratani.

Ingawa saratani yenyewe haiambukizwi, kuna baadhi ya visababishi vya saratani vinaambukizwa haswa virusi wa Human papilloma na Hepatitis B na C ambao huenezwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kujamiiana ama kushika majimaji yenye virusi hao.

Ongea na dr wako ili kujua namna ya kujikinga na virusi hawa

Kwa maswali na elimu kuhusu Afya unaweza kutuuliza tukakupatia taarifa zilizofanyiwa tafiti. Endelea kusoma mada zetu zingine kwa kubonyeza Tafutachochote hapa kisha andika unachotaka kuelewa


34 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page