Hisia ya uvimbe ndani ya nyonga na kuchomoza kwa uvimbe ukeni-
Makala hii imejibu swali la, kuonekana kwa uvimbe kwenye uke wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuhisi uvimbe upo dani ya uke au kuhisi uzito ndani ya nyonga, kuchomoza kwa nyama ukeni wakati wa haja kubwa na kutokwa kabisa na nyama/uvimbe kupitia uke. Maelezo ya makala hii imejikita kuelezea tatizo linaloleta dalili hii linalofahamika kwa jina la kitabibu kama 'Uterine prolapse'
Utangulizi
Kuhisi kitu kizito kwenye nyonga au uvimbe wakati wa kujisaidia au kuhisi kitu kinachomoza ukeni wakati wa kujisaidia ni hali inayojitokeza kwa wanawake walio na umri mkubwa na haswa kwa wale waliokwisha za watoto wengi. Hali hii hutokea pale endapo misuli ndani ya nyonga haina uwezo tena wa kushikiria ogani zilizo ndani. Ndani ya uzazi kuna via mbalimbali ikiwa pamoja na rektamu, uke, kizazi, mrija wa urethra, utumbo mpana na utumbo mwembamba n.k
Visabaishi
Kuchomoza kwa shingo ya kizazi kwenye uke - soma zaidi kwa kubonyeza hapa
Kuchommoza kwa misuli ya uke kwenye uke
Kuchomoza kwa utumbo mpana(enterocele) kwenye uke
Kuchomoza kwa kibofu cha mkojo kwenye uke
Kuchomoza kwa mkundu kwenye uke
Dalili
Dalili kwa wanawake wengi huwa hazionekani kwa mara nyingi, endapo zitaonekana huwa kama zifuatazo;
Maumivu wakati wa kujamiana
Kujitokeza kwa uvimbe ukeni
Kuhisi kuna uvimbe ukeni
Hisia za shinikizo ndani ya nyonga
Kuhisi kamaumekalia mpira
Kukauka kwa uke
Kutoa majimaji ukeni
Kupata shida wakati wa kutoa haja kubwa(konstipesheni)
Maumivu nyuma ya mgongo
Kuchomoza kwa nyama kwenye uke
Maumivu nyuma ya mgongo
Vihatarishi
Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi(ugonjwa wa obeziti)
Kunyanyua vitu vizito(kufanya kazi ya kunyanyua vitu vizito
Madhaifu ya misuli ya kuzaliwa nayo
Kuondolewa kuzazi
Kupata haja ngumu kwa muda mrefu
Kuwa na umri mkubwa
Komahedhi
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kwa uchunguzi zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile
Wasiliana na daktariw a ULY CLINIC kwa kubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.
Comments