Je ni kawaida kichanga kujamba?
Jibu:

Kujamba kwa mtoto ni tendo la muhimu na la kiafya. Maziwa anayonyonya kichanga hushambuliwa na bakteria waliotumboni na hivyo kuzalisha gesi ambayo inaweza kusababisha muungurumo wa tumbo na kujamba.
Kama mtoto akijamba humaanisha vitu vingi, baadhi yake ni:
Amekula chakula na ameshiba
Mfumo wake wa mmeng'enyo wa chakula unafanya kazi vema
Ni dhahiri kuwa mtoto akiacha kujamba huweza kuashiria madhaifu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula au kutopata chakula cha kutosha.
Kama kichanga ananyonya vema, hana homa na anajamba sana, haina haja ya kuhofu kwani ni hali ya kawaida.
Kama kichanga akipata dalili za hatari (ambazo zimeorodheshwa sehemu nyingine katika tovuti hii) mkimbize hospitali haraka kwa uchunguzi na tiba.
Коментарі